Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,904
Wakati akijenga hoja ya kuteta usafirishaji wa gesi kuja Dsm, Rais alisema kwamba mkoa wa Dar unachangia 80% ya pato la Taifa. kwa hiyo, alimaanisha kwamba kama kila mkoa utang'ang'ania rasimali zake Dar ndo itafaidika kuliko mikoa yote. Kwa maoni yangu Rais amepotoshwa na washauri wake. Kwa sababu zifuatazo;
Walipa kodi wengi wa nchi hii wana makao makuu yao Dar lakini shughuli za uzalishaji wao na watumiaji wa bidhaa zao wako nchi nzima. Nitatoa mifano michache.
1) Bakhresa (Bilionea no 1mwenye kampuni zaidi ya 300) analipa kodi hapa Dar kutokana na biashara zake za mikate, mafuta ya kupikia, ice cream nk. Lakini ngano na alizeti iliyotumika kuzalisha bidhaa hiyo haijazalishwa hapa Dar, imetoka mikoani. Pili, watumiaji wa bidhaa hiyo siyo wa Dar tu, ni nchi nzima. Ila kodi analipia hapa Dar.
Mengi anapolipa kodi kwa biashara ya maji, coca cola analipia TRA Dar, ilipo makao makuu ya IPP. Lakini maji yake yananywewa na watz kutoka mikoa yote. Na kiwanda cha maji si lazima iwe Dar.
Vituo vya Tv, Radio,magazeti nk wanalipa kodi hapa Dar, lakini walaji wa bidhaa yao ni nchi nzima. TV inaoneshwa nchi nzima, magazeti yanasomwa nchi nzima. Nimetoa mifano michache tu.(soma mchango wa great thinker mmojawapo in Blue)
By Ndachuwa
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iko Arusha lakini kwa kuwa Big Tax payer faili liko DSM; Leopard Tours nayo ni Big Tax Payer faili liko DSM; Tanzania Breweries wana plant Arusha na Mwanza faili liko DSM, Tanga Cement Big Tax payer faili liko DSM, Twiga Cement big tax payer faili liko DSM, Mabenki yote mafaili yako DSM ukiacha Community banks. Hili litarekebshwa na sheria ya majimbo 2016
Kwa hiyo, hoja hii ya Mkapa ( miaka ya nyuma) na Kikwete majuzi kuwa Dsm inachangia 80% ya pato la Taifa ni upotoshaji wa wazi ama ni uvivu wa kufikiri wa wasaidizi wao wanaohusika.
Nawasilisha.
Walipa kodi wengi wa nchi hii wana makao makuu yao Dar lakini shughuli za uzalishaji wao na watumiaji wa bidhaa zao wako nchi nzima. Nitatoa mifano michache.
1) Bakhresa (Bilionea no 1mwenye kampuni zaidi ya 300) analipa kodi hapa Dar kutokana na biashara zake za mikate, mafuta ya kupikia, ice cream nk. Lakini ngano na alizeti iliyotumika kuzalisha bidhaa hiyo haijazalishwa hapa Dar, imetoka mikoani. Pili, watumiaji wa bidhaa hiyo siyo wa Dar tu, ni nchi nzima. Ila kodi analipia hapa Dar.
Mengi anapolipa kodi kwa biashara ya maji, coca cola analipia TRA Dar, ilipo makao makuu ya IPP. Lakini maji yake yananywewa na watz kutoka mikoa yote. Na kiwanda cha maji si lazima iwe Dar.
Vituo vya Tv, Radio,magazeti nk wanalipa kodi hapa Dar, lakini walaji wa bidhaa yao ni nchi nzima. TV inaoneshwa nchi nzima, magazeti yanasomwa nchi nzima. Nimetoa mifano michache tu.(soma mchango wa great thinker mmojawapo in Blue)
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iko Arusha lakini kwa kuwa Big Tax payer faili liko DSM; Leopard Tours nayo ni Big Tax Payer faili liko DSM; Tanzania Breweries wana plant Arusha na Mwanza faili liko DSM, Tanga Cement Big Tax payer faili liko DSM, Twiga Cement big tax payer faili liko DSM, Mabenki yote mafaili yako DSM ukiacha Community banks. Hili litarekebshwa na sheria ya majimbo 2016Kwa hiyo, hoja hii ya Mkapa ( miaka ya nyuma) na Kikwete majuzi kuwa Dsm inachangia 80% ya pato la Taifa ni upotoshaji wa wazi ama ni uvivu wa kufikiri wa wasaidizi wao wanaohusika.
Nawasilisha.