Rais amepotoshwa, si kweli kuwa mkoa wa Dar unachangia 80% ya pato la taifa. Kwa sababu;

Ni kweli kuwa Serikali inakusanya mapato mengi sana Dar lakini kwa issue ya 80% Mkuu wa kaya ali-exaggerate hizo percentage
 

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iko Arusha lakini kwa kuwa Big Tax payer faili liko DSM; Leopard Tours nayo ni Big Tax Payer faili liko DSM; Tanzania Breweries wana plant Arusha na Mwanza faili liko DSM, Tanga Cement Big Tax payer faili liko DSM, Twiga Cement big tax payer faili liko DSM, Mabenki yote mafaili yako DSM ukiacha Community banks. Hili litarekebshwa na sheria ya majimbo 2016
 
we jamaa unatunga maneno,sijui hata huko kwenye tv wanatumia vigezo gani kukualika.hebu tutajie japo makampuni hamsini ya huyo bakharesa ili tuone kama una hakika na unachokiongea.
Mimi nawashauri msichukulie kila kitu kwa mtazamo wa kisiasa. Hapa tuko ktk jukwaa la kiuchumi. Hoja ya msingi ni Bakhresa ni mlipa kodi mkubwa kuliko wote hapa nchini. Analipia Dar, haimaanishi kwamba kwa kuwa ofisi zake ziko Dar Bidhaa zake zote zinatoka dar na zinatumika Dar. Hapa Rais amepotoshwa. unakubali au unakataa.
 

Asante great thinker. Naona umekuja na data nyingi kujaziliza hoja yangu. Mtu mwenye akili ya kuelewa hapa ameelewa. Labda mbishi.
 

kwa nini mnashdwa kufikiria hoja nzima mnafikiria nusunusu nyie ndo mnapotosha sasa.
 

usijitapishie mwenyewe tena mkuu..hoja yako yenyewe iko kisiasa umeiweka kama ulivyochangia jana itv malumbano ya hoja... nashukuru vijana wengi walikuwa kinyume na wewe teh teh....... wewe unafikiria kisiasa badala ya kiuchumi..na sijui kama umewahi kufika mtwara au unakujua arusha,moshi =chadema
 

Heshima mbele mkuu Mikael P Aweda, Hilo la kusema Bakhresa analipa Kodi sikubaliani nalo na wala sidhani kama Bakhresa analipa kodi inavyotakiwa. Tanzania ni nchi ya ajabu sana TRA wana ofisi zao za kodi kwa Bakhresa huu ni ufisadi. Haiwezekani TRA wakawafuata wafanyabishara kwa kuwafungulia ofisi za kulipia kodi zao. Huu ni upuuzi na upumbavu wa serikali iliyo dhaifu. Kwa nini wasiwe wanalipia TRA kwenyewe? Tangu lini Bill Gates akawa na ofisi za kulipia kodi kwenye ofisi zake?
 
hata samsung ni walipa kodi wazuri huko korea japo waraji wa bidhaa zao wako mpaka rufiji.
Sasa hapa sijui umewakilisha nini hasa.

kama amesoma hapa ni wazi ataelewa kikwete alichomaanisha ingawa naichukia hii serikali kupenda kufanya dar ndio kila kitu, nadhani sasa maendeleo yawafuate watu huko mikoani badala ya kila bidhaa kuja kutengenezewa dar es salaam
 

Kibe Jana ktk malumbano ya hoja kati ya wachangiaji karibu 30 ni wachangiaji 3 tu waliomuunga mkono Rais na sera yake ya kuleta gesi Dar. Unapotosha kwa makusudi. Turudi kwenye mada.
 

Mkuu,
Tuko pamoja. Nimesema kwamba ni mmoja wa tajiri mkubwa lakini sijasema ni mlipa kodi no 1. Hoja yangu ni kwamba bidhaa yake inatumika nchi nzima na rasimali zinatoka mikoa yote halafu wakubwa wanasifu Dar tu.
 
hata samsung ni walipa kodi wazuri huko korea japo waraji wa bidhaa zao wako mpaka rufiji.
Sasa hapa sijui umewakilisha nini hasa.

Mkuu hapa tunazungumza ndani ya nchi mmoja. Bidhaa inayouzwa nje ya nchi huwa ni case tofauti kabisa. Kwa mfano, serikal inajua mauzo yanayofanywa nje ya nchi kila mwaka kama ya dhahabu, Tazanite, pamba, ngozi nk. Japokuwa taarifa zimechakachuliwa kifisadi lakini wanayo. Kwa hiyo, tusichanganye mada. Ni vitu 2 tofauti.
 
Asante mkuu huo mfano unamtosha huyu kilaza.Ungeongoza na nokia.Wengine kwa kuandika Mabata wanaweza.
hata samsung ni walipa kodi wazuri huko korea japo waraji wa bidhaa zao wako mpaka rufiji.
Sasa hapa sijui umewakilisha nini hasa.
 
Ni ukweli kuwa mazao ghafi lazima yapelekwe Dar ambako tayari kuna viwanda na baadaye kusambaza bidhaa mikoani. Tatizo nini?
 
Mimi sina shida hata kama Dar itachangia zaidi ya 80% ya uchumi, pointi hapa ni kwamba sisi wote ni watanzania na tz ni moja na tuna haki sawa ya maendeleo. sasa kama kila kitu utawekeza Dar, vipi kuhusu mikoani? kwangu mimi huu ndo ubaguzi tofauti hata na wanamtwara kama ilivyosemwa kuwa ni wabaguzi. Ndo maana jamaa (national officers) wamegoma kuhamia Ddm, they only think of Dar, imagine!!
 
Si 300 ni zaidi ya 300. Ninakupa taarifa za uhakika. Siyo vizuri kutaja majina ya watu lakini ninafahamiana kwa karibu sana na watu wenye nafasi kubwa ktk makampuni ya Bakhresa.


Aweda,
Unaongelea 'products' au kampuni? Kama ni products naweza kukubali. Kampuni za Bakhresa hazifiki 300. Kampuni zake zimeorodheshwa zote katika tovuti yake, hazifiki hata 20. Kwa uhakika zaidi chungulia HAPA, kama walivyoandika wenyewe wenye kampuni zao.
 
Nakupinga bakhresa hamiliki makampuni 300.

Wewe kumiliki kampuni unakuelewaje? Hata ukiwa na hisa 3 ni mmiliki........jaribu kusoma porfolio investment ndio utamjua Bkhressa ni nani......sio mikate na lambalamba tu......ana hisa mpaka Coca Cola
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…