Rais anakopa imekuwa nongwa, sasa kaanza kukusanya za ndani ili asikope mmeanza kulia. Rais fanya unavyojua, hawa ndio wanadamu!

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Mama, hawa ndio wanadamu, ulikopa ili mzigo wa Kodi usiwe mkubwa kuhudumia maendelea, angalau uu-suspend kwa muda au Kwa vijikodi vidogo vidogo, tuhudumie mikopo ya muda mrefu, kuliko kutulima Kodi ya ghafla.

Wenye nongwa wakaongea ooohhh, tuna hela nyingi, mbona sijui nini,nchi yetu tajiri.

Sasa umeanza msako wa Kodi wa ndani kwa ndani Tanzania ili wale wa falsafa ya Ndungai kwamba tukamuane wajue maana yake nini, wameanza kulia tena.

Mama kanyaga twende. Watakuelewa tu, watu hushukuru baadae, hata Nyerere wanaimba juhudi zake baada ya kufariki. Chameleone, mwanamuziki wa uganda aliimba, wanashukuru ukishaenda.
 
Kuishi kwa shemeji yako na unalala sebuleni ndiyo tatizo lilipo
 
Hii nchi ni kama ina laana. Haatukustahili kua na uongozi kama huu
Wewe hata kumnunulia nguo za ndani mkeo umeshindwa, familia yako huwa inakunanga hivyo hivyo kwamba tuna libaba la hovyo hovyo tu
 
Mama amesababisha uongozi wa wanawake kushuka thamani.
Sio kwa kukopa huku na bado tozo iko pale pale.
Kwani wengine walifanyaje?
Au tatizo ni matumizi?

Maana wanawake tunajuana. anaweza kukopa anunue dela la shughuli badala ya kuwekeza ili izalishe. 🤔
 
Ye si alisema hataki kodi za dhulma.
 
Kuna wanasiasa wajinga wajinga wanalalamikia mikopo.
Badsla yake wawahamasishe wananchi majimboni mwao walipe kodi.
 
Hiyo miradi unayoiona Kila Kona ingegharamiwaje? Nyerere alikataa kukopa, aliiacha nchi kama shimo la taka, usafiri wa basi mwanza Dar siku mbili, dar kagera karibu wiki. Maofisi ya umma wanaandikia mifuko ya simenti, Ofisi zimejaa popo,
Kupanga ni kuchagua
 

Naunga mkono hoja ,wafanyabiashara wanakwepa sana kodi ,imagine unaenda kununua vitu dukani vya hata laki 6 ,wanaandika tu general vifaa vya ujenzi elfu 50 basi.

Watu wanaolipa kodi vizuri ni wafanyakazi(PAYE) kabla hata haijaingia bank ishalimwa.
 
Dada yako katangulia chumbani? Ni mboga ya mtu hiyo
Ukitoa hoja/uzi,penda kupokea yote.Unayoyatarajia na usiyoyapenda.Kujibujibu hovyo kwenye uzi ni kupania jambo na kuonesha ulemavu.Tulia na ujibu vizuri kwa akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…