Rais anakopa imekuwa nongwa, sasa kaanza kukusanya za ndani ili asikope mmeanza kulia. Rais fanya unavyojua, hawa ndio wanadamu!

Hapo kwa shemeji bado wanaangalia tv sebuleni, yaani Leo utalala muda umeenda, kulala kwako mpaka waondoke sebuleni utandike godoro
Kwa kuwa wewe na dada yako mna share mume mmoja basi unadhani kila mmoja yupo kwenye hilo kundi.
 
Akili yako fupi sana.
Watanzania wanachosema ni kwamba, Tanzania ina rasilimali nyingi nyingi nyingi sana, lakini bado akili za Viongozi wetu pamoja na wewe zile zisizoweza kusimamia vizuri hizi rasilimali ili kuwaletea maendeleo Watanzania.

Kama mtu mmoja mwenye akili timamu anasema akipewa Bandari moja tu ya Dar es salaam anaweza kuitumia kuhudumia Nchi zote za Afrika Mashariki, inakuwaje sisi tuna Bandari za Mtwara, Dar es salaam, Tanga, lakini pia tuna Mbuga za wanyama,madini, bahari, misitu, mlima Kilimanjaro nk. lakini bado tupo kwenye wimbi la umaskini.
Hili ni tatizo.
 

Hata Japan wanakopa.. Magufuli alikopa....kila Rais anakopa..la muhimu mikopo itumike Kwa malengo sahihi
 
Mama anatupikia nyama sisi watoto tunataka maharage ili tuvimbiwe
Mwacheni mama afanye anachokiona kinafaa kwetu
 
Raslimali tu haitoshi kuwa tajiri, hata wewe baba au Babu yako Wana mashamba huko na mifugo, lakini bado masikini, au na wewe utaanza kulaumu wazazi wako kwa kumiliki ekari 500 na n'gombe 5000, lakini nyie bado masikini?

Hiyo gesi unadhani unaweza kuichimba kama unavyochimba shimo la choo?, Maendeleo sio kama mana jangwani
 
Nani alimwambia aache kukusanya 20,000 za matching guys kwenye masoko rasmi yaliyotengwa Kwa kuiboresha vitambulisho vyao Nchi nzima?

Unaposhauriwa, Changanya na zako-JK.
 
Nani alimwambia aache kukusanya 20,000 za matching guys kwenye masoko rasmi yaliyotengwa?

Unaposhauriwa, Changanya na zako-JK.
Administration cost za hiyo Kodi ni kubwa kuliko unachopata, unaenda na kundi la mgambo 100, kukusanya laki mbili, halafu unawalipa posho hao mgambo shilingi laki tano, bado usafiri na chakula
 
Administration cost za hiyo Kodi ni kubwa kuliko unachopata, unaenda na kundi la mgambo 100, kukusanya laki mbili, halafu unawalipa posho hao mgambo shilingi laki tano, bado usafiri na chakula
Kwa kuacha kukusanya hizo 20,000 ameacha kulipa mgambo?

Mbona mgambo wako pale pale, na ukusanyaji wa Kodi hizo wanakusanya viongozi wa masoko rasmi wakisimamiwa na watumishi wa halmashauri au Jiji husika.

Pia, usimjibie Rais, acha apokee ushauri, Kodi ya matching guys ilikuwa moja ya idea Bora kabs kupata pesa ya haraka.
 
Idea ya hovyo kabisa ya huyo populist aliyejifia.

Ungetaka nisimjibie Rais ungemuandikia kwa anuani ya ikulu
 
UVCCM hawezi kuelewa haya mambo.
 
Idea ya hovyo kabisa ya huyo populist aliyejifia.

Ungetaka nisimjibie Rais ungemuandikia kwa anuani ya ikulu
Atarudi pale pale, matching guys wamesharudi barabarani, na soon utasikia wanakusanya hzo 20,000.
 
Atarudi pale pale, matching guys wamesharudi barabarani, na soon utasikia wanakusanya hzo 20,000.
Haina shida, kinachofanyika Kila bidhaa inaongezewa Kodi bandarini kabla haijatoka.

It's better kui-withhold hiyo Kodi kwa maana ya kwamba muagizaji ailipe bandarini au kiwandani kabisa kwa kuwa inawezekana bidhaa ikauzwa kimagendo.
 
Tena awanyooshe kweli kweli,Mtzn sio mtu wa kumchekea
 
Hata Japan wanakopa.. Magufuli alikopa....kila Rais anakopa..la muhimu mikopo itumike Kwa malengo sahihi
Magufuli alikopa lakini kwa asilimia kubwa aliweza kudhibiti ufisadi, tofauti na sasa ambapo Mafisadi wanagawana fedha za mikopo hata kabla hazijatua Nchini.
 
Akili kama hizi ndizo zilizotufikisha hapa tulipo.
Rasilimali za Nchi ndo utajiri wa Nchi, kule uarabuni wana visima vya mafuta, wanauza mafuta wanajenga Nchi zao.
 
Magufuli alikopa lakini kwa asilimia kubwa aliweza kudhibiti ufisadi, tofauti na sasa ambapo Mafisadi wanagawana fedha za mikopo hata kabla hazijatua Nchini.

Unaongea hoja zaidi ya tatu Kwa pamoja...

Hoja ya kwanza ... Umuhimu WA kukopa....

Hoja ya pili ..ufisadi wa pesa zilizo kopwa...

Hoja ya Tatu ..alivyokopa Magufuli ilikuwa sawa...


Ntakujibu hoja moja hapo ya tatu..

Ilikuwaje sawa?wakati hata taarifa Tu haikuwa sahihi...tulikuwa hatuambiwi tunakopa wapi na kiasi gani Kwa matumizi gani ...kuficha ficha ndo kunapelekea ufisadi ambao huwezi hata kuujua...

Twende na hoja no 2...Je kweli Magufuli alidhibiti ufisadi?..
Wewe unajua gharama halisi za ujenzi wa airport ya chato?..bajeti Yake ?ilitangazwa wapi?Bunge lipi la bajeti lilipitisha?kampuni iliyojenga ilitokea wapi? Huo mfano mmoja tu
 
Bado ujabebewa afu tatu yako ya kula mchana ndo mana kisedemnede.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…