Mawazo yako ni mazito sana, Hivyo inabidi tufanye vyote, tuongeze mishahara, tupunguze kodi, tutoe ruzuku nk.
Lakini kwa ukubwa huu athari kwa mapato ya serikali yatakuwa makubwa ambayo inaweza isiwe rahisi sana kufanya vyote.
Nadhani ni vyema tuchague moja ambalo litasaidia wananchi kwa kipindi hiki na tusiathiri sana mapato ya serikali
Ilikuwa ni makosa makubwa kuondoa ruzuku kwenye bei za pembejeo wakati asilimia kubwa ya wakulima wetu bado wadogo.
Kupunguza kodi kwenye mafuta hiyo inakuwa kama temporary measure kwa kama miezi sita 3/6 ijayo kustabilize price na kupunguza ongezeko ya bei kiholela.
Kazi moja kubwa ya serikali ni kuhakikisha kuna price stability, to control inflation, kuhakikisha kuna chakula nchini kwa bei wanazoweza wananchi kuzimudu na kuhakikisha shughuli za uchumi zinaendelea.
Ilitakiwa serkali kuhamasisha wakulima walime kilimo cha kisasa, kwa ufanisi Ukizingatia kilimo kinategemewa na 75% ya wananchi wa Tanzania. Serikali ingejikita zaidi kutafuta masoko ya uhakika ya nje kupata foreign currency, soko la ndani lipo la uhakika.
Kujitosheleza kwa chakula kwa soko la ndani, ziada kuuza nje kungeongeza ajira na mapato ya serikali kupitia kodi mbalimbali. Wangerudisha pesa yao ya ruzuku na pesa nyingine zaidi.
Sera rafiki, mfano unaweza kuwakopesha wakulima mbolea wakiuza mazao yao wanalipa.
Muhimu serikali kuwa serious na kuwa na sera rafiki na mikakati madhubuti ya muda mrefu kuendeleza kilimo.
Tunasema kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa ila hatufikirii hata tunamaanisha nini? Maana halisi ya haya maneno.
Bila uti wa mgongo kwa binadamu huwezi kusimama, kutembea, kufanya vitu vingi muhimu, kufikiri sawasawa, ku- control mwili wako, utapooza.
Bila kilimo cha kisasa hapa TZ, kukifanya kilimo kipaumbele kwa vitendo siku zote tutakuwa tunazunguka palepale.
Sera rafiki, incentive kwa wawekezaji wa viwanda vya mbolea,viwanda vya kutengeneza matrekta, vifaa vya umwagiliaji, uzalishaji wa mbegu zenye viwango, na pembejeo nyingine hapa nchini vingesaidia sana kukuza hii sekta.