Pre GE2025 Rais anazipa Simba na Yanga pesa kila goli (Goli la Mama), anazitoa wapi? Msigwa ajibu "Pesa anazotoa ni ndogo"

Pre GE2025 Rais anazipa Simba na Yanga pesa kila goli (Goli la Mama), anazitoa wapi? Msigwa ajibu "Pesa anazotoa ni ndogo"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Mmesikia majibu ya Semaji la Serikali Msigwa?

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amemjibu kuhusu hpla za 'Goli la Mama' kwa timu za mpira wa miguu za Simba na Yanga ambazo hutolewa kama motisha baada ya kufunga goli kwenye michuano ya Kimataifa

Hahahaahaha!

Msigwa hadi ametia huruma aiseee. Kweli huu ni wizi wa pesa za umma! Hayo mafungu yanatengwaga chini ya kifungu kipi kwenye bajeti ya Serikali inayopitishwa na Bunge? Hayo mafungu yanawekewa shilingi ngapi kwa mwaka wa fedha na zinatumikaje? Aisee kweli hii nchi kodi za wananchi zinatumika vibaya!

Watanzania amkeni kwa kweli. Hamstahili hata kukosa maji ya bomba ila kuna watu wanatumia vibaya fedha zenu wapendavyo.
 
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amemjibu kuhusu hpla za 'Goli la Mama' kwa timu za mpira wa miguu za Simba na Yanga ambazo hutolewa kama motisha baada ya kufunga goli kwenye michuano ya Kimataifa

Majibu mazuri sana toka kwa Msigwa kuna nyumbu hata hawajui kuwa Rais anafungu kama hilo wanafikiri labda ni Mwenyekiti wa Chadema huyo. Yaani Rais akose pesa za kusaidia jamii kweli? Basi Urais utakuwa hauna maana kabisa. Rais anafungu lake kwa kizungu wanasema Vote.
 
Ukiona mtu kaulizwa umekula nini halafu anaanza kukuambia historia ya kilimo na manufaa yake, majembe na mbolea yanauzwa wapi hapo jua tu kuna jambo🐼
Katika kujibu ni lazima utoe pia ufafanuzi ili kuelewaka zaidi ila nyumbu kama nyinyi hamuwezi kuelewa!
 
Majibu mazuri sana toka kwa Msigwa kuna nyumbu hata hawajui kuwa Rais anafungu kama hilo wanafikiri labda ni Mwenyekiti wa Chadema huyo. Yaani Rais akose pesa za kusaidia jamii kweli? Basi Urais utakuwa hauna maana kabisa. Rais anafungu lake kwa kizungu wanasema Vote.
Acha uzwazwa wewe! Hilo fungu lipo kwenye kifungu kipi cha bajeti iliyoidhinishwa ba Bunge? Linawekewa shilingi ngapi kwa mwaka wa fedha?

Hizo pesa zinatumikaje? Huu ni wizi wa pesa wa pesa za walipakodi wa hili Taifa.

Yaani mimi pesa yangu ninayoipata kwa jasho inaenda kulipia magoli ya simba na yanga? Tena hata bila Bunge kuidhinisha?

Huu ni wizi tu kama wizi mwingine.
 
Majibu mazuri sana toka kwa Msigwa kuna nyumbu hata hawajui kuwa Rais anafungu kama hilo wanafikiri labda ni Mwenyekiti wa Chadema huyo. Yaani Rais akose pesa za kusaidia jamii kweli? Basi Urais utakuwa hauna maana kabisa. Rais anafungu lake kwa kizungu wanasema Vote.
Dah
 
Mbona kajibu vizuri sana.
kajibuje vizuri? ameulizwa ni zake binafsi hajatoa majibu!

Alipaswa kusema hizo pesa zipo kwenye kifungu kipi cha Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge na alipaswa kusema kama ni za umma au la?

Alipaswa kusemwa pia kifungu hiko kama kipo kinawekewa kiasi gani?

Kumbuka hakuna fedha za Rais nchi hii. Fedha zote ni za wananchi (Kodi za Wananchi) na zinapaswa kutumika kwa namna Ilivyoidhinishwa na Bunge tu kwenye Bajeti ya Serikali.
 
Hahahaahaha!

Msigwa hadi ametia huruma aiseee!

Kweli huu ni wizi wa pesa za umma!

Hayo mafungu yanatengwaga chini ya kifungu kipi kwenye bajeti ya Serikali inayopitishwa na Bunge?

Hayo mafungu yanawekewa shilingi ngapi kwa mwaka wa fedha na zinatumikaje?

Aisee kweli hii nchi kodi za wananchi zinatumika vibaya!

Watanzania amkeni kwa kweli! Hamstahili hata kukosa maji ya bomba ila kuna watu wanatumia vibaya fedha zenu wapendavyo.
Kama hujawahi kufanya kwenye mashirika makubwa huwezi kujuwa hili, hata CEO wa kampuni anakuwa nafungu lake la entertainment au matumizi ya kukarimu ni sehemu ya budget ya ofisi ya Rais sasa ukubwa wa budget hiyo inategemea na ukubwa. Hakuna mtu anachukua pesa kwenye fungu lingine huyu mwandishi anaendeshwa na hisia haelewi mifumo ya serikali au makampuni makubwa.
 
kajibuje vizuri? ameulizwa ni zake binafsi hajatoa majibu!

Alipaswa kusemwa hizo pesa zipo kwenye kifungu kipi cha Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge na alipaswa kusema kama ni za umma au la?

Alipaswa kusemwa pia kifungu hiko kama kipo kinawekewa kiasi gani?

Kumbuka hakuna fedha za Rais nchi hii. Fedha zote ni za wananchi na zinapaswa kutumika kwa namna Ilivyoidhinishwa na Bunge tu kwenye Bajeti ya Serikali.
Sasa wewe unajuwa budget ya ofisi ya Rais?? wewe unaona jumla tu huwezi kuona kila kifungu kwenye budget ya ofisi ya Raisi, kuna mpaka ya nguo, wafanyakazi, chakula na mabalaa yote mpaka simu ni humo humo kwenye budget ya ofisi ya Raisi, Hapa zingatia Ofisi ya Rais sio Raisi
 
Back
Top Bottom