Pre GE2025 Rais anazipa Simba na Yanga pesa kila goli (Goli la Mama), anazitoa wapi? Msigwa ajibu "Pesa anazotoa ni ndogo"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Acheni longolongo. Semeni fedha hizo zip kwenye kifungu kipi kilichoidhinishwa na Bunge kwenye bajeti ya Serikali?

Semeni pia kifungu hicho kilichoidhinishwa kwenye hiyo Bajeti kilitengewa kiasi gani?

Kumbuka hizi ni pesa za walipakodi sio pesa za kampuni binafsi.
 
Wewe IQ yako ndogo sana nenda kasome au inawezakana maisha yamekupiga sana, unajuwa bugdet inatengenezwa vipi? Kwanini usisikilize siku budget inavyosomwa uletewe wewe hapa kama nani? Budget inapitishwa na wabunge sio wewe sasa kama unashida mfuate mbunge wako muulize hivi ngapi mlipitisha.
 
Bajeti ya nchi ni issue ya Umma.

Ndo mana inapitishwa Bungeni kwenye mjadala wa wazi ili umma uone.

Wakati wa Bajeti huwa vinasomwa kifungu kwa kifungu na pesa zilizotengwa. Msigwa anapaswa kututajia kifungu rasmi kinachotumika kutoa fedha hizo na anapaswa pia kusema kifungu hicho kilitengewa kiasi gani ili wananchi wajue pesa zao zinavyotumika.

Kumbukeni hizi ni pesa za Umma( Kodi za Wananchi) na sio pesa zake binafsi. Hivyo majibu ya msigwa sio majibu amepuyanga tu.
 
Ukiona mtu kaulizwa umekula nini halafu anaanza kukuambia historia ya kilimo na manufaa yake, majembe na mbolea yanauzwa wapi hapo jua tu kuna jambo🐼
Umenikumbusha mwalimu mmoja kwa Sasa ni R.I.P

Huyu mwalimu ndie alikua mwalimu wa chakula pale uboyzn Katika moja ya shule kongwe Zaidi Tanzania by then.

Iliibuliwa wizi/upotevu wa viroba vya Michele na maharage, mafuta na sukari n.k binafsi nilishuhudia wizi usiku wakatupa kiroba kimoja kwa kua nilijua peke angu nikaenda kuita watu tukakuta kiroba kimetaifishwa.

Yule mwalimu kwenye kikao Cha shule alipo takiwa kujibu akaanza kuongea akisema DINNING HALL NI CHAFU HATUFANYI USAFI, PIA TUNAINGIA DANNING HALL NA NDALA,BUKTA, WENGINE HAWAVAI T-SHIRT ZA SHULE AKAENDELEA KUSEMA KUNA WATU HAWAOGI, DOMMITORIES NI CHAFU HATUFAGII N.K πŸ˜…πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜…

watu Waka anza kuzomea akaambiwa ajibu hoja za upotevu/ wizi wa chakula store sio kutugeuza mazuzuπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒ
 
Wewe unadhani zile nguo anazovaa ananunua kwa pesa yake? acha ujinga hata taasisi kubwa za mabenki CEO ana budget ndio maana kuna wakati wanaitisha futari tu mkubwa anaalika wageni unadhani anachota tu Bank.
 
Pesa za uma unalipa hata kodi wewe? Budget inasomwa, wabunge wanapitia kama hawaridhika wanaijadili budget kifungu kirekebishwe au hapana shida hujui au unakurupuka tu hapa. Budget ni ya ofisi ya Raisi sio ya msemaji hana access ya budget ofisi sio yake. Gombani ubunge ukalinde pesa za umma.
 
Swali ameulizwa Msigwa na alipaswa kulijibu yeye mwenyewe kwa Ufasaha.

Labda huwajui Viongozi wa Afrika. Huwa wana Tabia ya kupiga simu kwa Mawaziri wao wa Fedha na hata Benki kuu kuagiza waletewe hela tena zikiwa taslimu.

Fuatilia documentary ya Mobutu wasaidizi wake walivyosema namna alivyokuwa anafanya. Na kwenye haya ndo wizi wa fedha za umma unatokea wa kutisha

Rais anaweza mwambia msaidiz wake mwambie Gavana wa BOT alate Bil 1, Msaidizi wake akatoa maagizo ziletwe Bil 2 ( akaweka cha juu Bil 1 ya kwake) na Gavana akatoa Bil 3 akaweka Bil 1 yake pia

Wanaouliza haya maswali wanajua hii michezo na wanajua fedha hizi hazipo kwenye mifumo rasmi kama ilivyoidhinishwa na Bunge kwenye Bajeti.

 
Acha kuzunguka. Sema hapa hilo fungu la Rais limetengewa kiasi gani kwenye Bajeti ya mwaka huu?
 
Ninalipa sana kodi. Nina kampun zangu mbili hapo Tanzania na kwa mwezi nalipa karibu Mil 50 kwenye kodi tu.
 
Ndio maana nimesema wewe huna exposure, watu hawaibi hivyo kijinga jinga wala huwelewi mfumo wa pesa zinavyotoka. Acha ujuaji jifunze kama unataka nitakupa somo ila ukitaka kuleta chuki tu basi wewe piga kelele tu.
 
Kwenye mtihani unambiwa point uweke juu halafu maelezo yanafuata. Huyu jamaa ameaza na maelezo mengi ambayo hayana msingi.
 
Acha kupuyanga. Jibu swali uliloulizwa
Sasa swali wewe unayejiona una hoja kumbe ujinga. Budget imepitishwa na bunge unataka nikjibu nini? wewe unadhani kuna fungu limeandikwa Goal la Mama? acha ujinga kuna kitu kwenye budget kinawekwa Other miscellaneous. sasa jiongeze
 
Reactions: UCD
Unajua fungu la Responsibility Allowance ambazo zinatolewa kwa viongozi wakuu wa serikali? Na unajua Rais ana Vote yake? Unabisha wakati hujui lolote!! Tatizo unajifanya unajua wakati kichwani ni zero brain.
 
Hii nchi kweli ina pesa, halafu lini mpira umekuwa huduma za kijamii?!
 
Wabunge wana mfuko wa Jimbo... Rais ana mfuko wake pia wa jamii. Usitake kujua una tsh ngapi πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…