Habari wanajamvi!
Nazungumzia Rais kushitakiwa amalizapo muda wake (kama alifanya makosa akiwa madarakani).
Asili ya sisi Waafrika (watu weusi) ni kupenda kukomoana, majungu na visasi.
Inawezekana kabisa ukiwa madarakani ukafanya/ukasimamia jambo kwa mujibu wa taratibu lakini kwa kufanya hivyo ukagusa/ ukaharibu maslahi au mipango ya wengine.
AU unaweza kujistarehesha na hawara wa mtu bila kujua siku wakishika madaraka wao basi kwisha habari yako.
Sheria hii inafaa kwa jamii zilizostaarabika na kuelimika,sio kama huku kwetu ambako WASOMI NDIO WAJINGA WAKUU.
Nasisitiza Rais asibughudhiwe pindi amalizapo wakati wake, aachwe apumzike.
Mimi mwandishi itikadi yangu sio tu ni CCM, bali ni timu MAGUFULI