Rais asibughudhiwe pindi amalizapo wakati wake, aachwe apumzike

Ikiwa raisi akimaliza hawezi kupandishwa mahakamani au kuhukumiwa ni sawa na kutoa leseni ya kufanya utakavyo wakati ukiwa madarakani. Nadhani hiki ndio kinachotokea kama matokeo ya kuwa na sheria za kichovu kama hizi.
 
Mkuu upo sahihi 100% katika jicho lililostaarabika, ila kwa jamii zetu huwa tuna ushamba wa kumkomesha fulani kama alikugusa maslahi yako hata kama alitenda hivyo kihali.
Hivyo mstaafu anaweza ingia jela kwa kuundiwa tu zengwe
Penye haki zengwe halina nafasi! Kiongozi muadilifu ana kinga ya wanyonge ambao ndio wengi watamlinda kufuatana na sheria zile zile alizozifuata akiwa madarakani!
 
Je, hizi jamii zetu unaziita za kishamba hazizalishi pia baadhi ya viongozi wa shamba ambao hawatumii madaraka wanayopewa kikatiba na wananchi kwa manufaa ya umma, badala yake wanatumia madaraka hayo kuwakomoa wananchi ambao hawawapendi? Au upande wa pili wa hoja yako wanaoijua ni wasomi peke yake!?
 
Tanzania madarakani/ uongozi ni ajira na sio utumishi
 
Kwamba wasomi huku kwetu ndiyo wajinga wakubwa,hawa akina prof nani ndiyo viongozi wa ujinga,haya bwana.
 
Je. Yeye akiwa mtaafu ni ruksa kubughuzi walioko madarakani kiasi cha kuwalia njama kama anaziweza hizo njama?
 
Je. Yeye akiwa mtaafu ni ruksa kubughuzi walioko madarakani kiasi cha kuwalia njama kama anaziweza hizo njama?
Mstaafu ana haki kama raia mwingine yeyote! Anaweza kushitaki na pia kushtakiwa.
Katiba ya wenzetu South Africa hailindi wahalifu na ndio maana Rais wao mstaafu Zuma alifungwa jela na kesi lukuki zinamgoja!
 
Yahani unataka rais aje apuyangepuyange aguvuluge vuluge kila kitu alafu ahachwe tu kisa alikuwa kiongozi mkuu. Alafu unategemea nchi ya namna hiyo inaweza ikatoboa ktk maendeleo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…