Rais aunde tume mbili kuchunguza shutuma za watu kudhulumiwa mali zao awamu iliyopita pamoja na kifo cha Hayati Dkt. Magufuli

Rais aunde tume mbili kuchunguza shutuma za watu kudhulumiwa mali zao awamu iliyopita pamoja na kifo cha Hayati Dkt. Magufuli

Nimemsikia Raia Samia anasema watahakikisha wanakusanya kodi halali na sio ya dhuluma na huko nyuma amekemea TRA kunyang'anya watu mitaji na hela zao kwa kisingizio cha kodi.

Hapa tuseme ukweli kuwa tuhuma kuwa miaka mitano iliyopita watu 'wamedhulumiwa' na kunyang'anywa hela zao' zimezagaa sana.

Sasa je, ukweli ni upi?

Waliofanya hivyo walipokea kweli maagizo kutoka juu au wengine walisingizia 'maagizo kutoka juu'kuendesha ujambazi?

Nafikiri hili ili tuweze kulijua ukweli wake ingeundwa tume ya kuchunguza na kuweka ukweli wote wazi ili ijulikane kiasi gani kilidhulumiwa, kilienda wapi?

Kina nani walihusika? Walipewa kweli maagizo au walifanya ujambazi tu wenyewe? Tume iwe ya wazi kabisa na media ziwepo wakati watu wanahojiwa.

Ingine ni Tume ya kuchunguza kifo cha JPM.

Je, ingewezekana kuepuka?Kulikuwa na uzembe? Mkono wa wa mtu? Kama mkono wa mtu walikuwa wanataka nini? Wapo wapi?
  • Kama ni uzembe, je tumeweka mazingira ya kutukutokea tena uzembe huo?
  • Zilikuwepo tetesi aliwahishwa Nairobi dakika za mwisho. Je, why Nairobi?
  • Why hizo facilities za Nairobi hazipo hapa nchini huko Mzena au Muhimbili?
  • Nani anahusika na uzembe huo?
  • Lolote la kujifunza? La kulifanyia kazi?
Binafsi naona hizi tume mbili ni muhimu mno kama kweli kama Taifa tumedhamiria kwenda mbele bila kurudi nyuma, vinginenevyo historia ina kawaida ya kujirudia.

Tujifunze. Turekebishe
Sijawahi kupata ushahidi wa Magufuli kukimbizwa nairobi bai ni innuendo to. Kipindi hicho hospitali ya Nairobi ilikuwa na Rais au Waziri mkuu wa zamani wa Sumalia ambaye alifariki pale. Kwa populairty ya Magufuli haingekuwa raihisi apite uwanja wa ndege wa JNIA hadi afike Wilson Airport na kuhamishiwa Nairobi Hospital bila watu kujua!
 
Na huu ndio ukweli wenyewe.Au nasema uongo ndugu zangu?
Hizo tuhuma za kifo ni uzushi tu man.Hivi kwa ulinzi wote ule ikiwemo helicopter angani kama tupo iraq hio nafasi wangepatia wapi.
Mwache Mungu asikie maombi ya wengi yaliyofanana.
 
Back
Top Bottom