Rais avunja rasmi tume ya Warioba

Rais avunja rasmi tume ya Warioba

Lifuatalo ni Tangazo la Rais Jakaya Kikwete alilotoa leo hii:

TANGAZO LA SERIKALI KUHUSU KUVUNJWA KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

Mhe. Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katika kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kwa Tangazo la Serikali Na.110 la Mwaka 2012.

Tume ilikusanya maoni na kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imewasilishwa kwenye Bunge Maalum.

Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 3, Rais amepewa mamlaka ya kuvunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa Bungeni.

Mnamo tarehe 18 Machi, 2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum. Kutokana na hatua hiyo, na kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano alivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19 Machi,2014 kwa Tangazo la Serikali Na.81 la tarehe 21 Machi, 2014.

Hivyo kwa Tangazo hilo, shughuli zote za Tume ya Mabadiliko ya Katiba zimemalizika rasmi tarehe 19 Machi, 2014.

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
Dar es Salaam.

25 Machi,2014
 
Anaivunja Tume aliyoiunda lakini ameshindwa kukubaliana na walichokikusanya kutoka kwa wananchi.
 
Sawa, Aivunje tu lakini machufuko yatakayotokea atawajibishwa,
ameogopa tume inaweza kuitwa na ku clrify alichokisema JK bungeni ambapo aliiponda tume na maoni yake...sasa nadhani wajumbe watalazimishwa kujadili rasimu akiyoiwasilisha JK badala ya Warioba.
 
Kivipi labda? fafanua.

Sio ufafanuliwe kila kitu...Hapo hata wewe mwenyewe unaweza kujifafanulia kuwa tuna viongozi wa kipumbavu wanaoongoza watz wapumbavu pia...Vinginevyo nchi za watu huwezi kuchezea watu kirahisi hivo halafu ukabaki salama
 
Kwani si alishasema tangu siku ile anafungua bunge!! Alisema baada ya tume kukabidhi rasimu basi itakuwa imefikia ukomo
 
Kama kuvunjwa ipo kikatiba nayo ni habari?
 
baada ya kusikia ataitwa bungeni kujibu mipasho ya muimba taarabu aliyechukua backpack ya mwanafunzi akidhani parachuti...
 
Kama Raia wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,ama kama Waziri mkuu msitaafu au kama Jaji mstaafu n.k

Na kama mwenyekiti mstaafu wa tume ya kukusanya maoni ya rasimu ya katiba mpya.
 
Kwa tangazo hilo Warioba tayari kazibwa mdomo maana ataongea kama nani sasa?
Hii si sawa nadhani kuna jambo zaidi tusubiri.

Hajazibwa mdomo Mkuu, anaweza kuongea kama mwananchi wa kawaida, kiongozi mzoefu, au "aliyekuwa m/kiti wa tume" ya mabadiliko ya katiba. Waliozibwa mdomo ni wabunge wa ccm wenye mrengo wa Warioba!
 
suluhisho ni kuireject rasimu itayopitishwa ya ssm kwenye referendum

Sheria ya mabadiliko ya katiba inakataza kupiga kampeni kwa wananchi kuikubali au kuikataa! Hicho kifungu ni shida kwa wananchi wa kawaida, vyama vya siasa na kijamii, vyombo vya habari ikiwemo vya tbccm!

Ni shida!
 
Hapa ndo naona wakati muafaka wa jaji kufunguka kama Raia wa kawaida na kama Waziri mkuu mstaafu,na kama Jaji.......!!!

Watamvika uasi, sio watu wakawaida hao. Ila nguvu ya umma yaweza kumlinda .

Kila kinachofanyika ktk mchakato huu kiliratibiwa mapema. Ingekuwa vigumu kuwaeleza wadanganyika wakaelewa. Sasa wanajionea wenyewe 'live'. Ni wakati mwafaka chama kikikuu cha upinzani kuanza maandalizi ya ushambuliaji....nina maana ya kutoa tamko rasmi kuongoza umma kuchukua hatua thabiti dhidi ya waujumu katiba mpya...magamba.
 
Warioba angekuwa kijana wangembadika tuhuma kibao...ikiwemo na tamaa ya madaraka. Sasa hawana mahali pa kuanzia. Kiburi walicho nacho Nape na Mwigulu si bure...wako tayari kuliangamiza taifa. Ni neema ya Mungu..jeshi liwe upande wa umma vinginevyo hawana jinsi. Nape na Mwigulu watatumia jeuri ya chama ( fedha) na kutumia policecccm kufanya wanavyotaka.
 
Heri ameivunjilia mbali, warioba alijiona mungu mtu sana
 
Back
Top Bottom