Rais avunja rasmi tume ya Warioba

Rais avunja rasmi tume ya Warioba

Rais Jakaya Kikwete amevunja rasmi tume ya kukusanya maoni ya katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph warioba. Hii ni kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 81 la Machi 21 mwaka huu.

====

TANGAZO LA SERIKALI KUHUSU KUVUNJWA KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

Mhe. Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katika kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kwa Tangazo la Serikali Na.110 la Mwaka 2012.

Tume ilikusanya maoni na kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imewasilishwa kwenye Bunge Maalum.

Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 3, Rais amepewa mamlaka ya kuvunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa Bungeni.

Mnamo tarehe 18 Machi, 2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum. Kutokana na hatua hiyo, na kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano alivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19 Machi,2014 kwa Tangazo la Serikali Na.81 la tarehe 21 Machi, 2014.

Hivyo kwa Tangazo hilo, shughuli zote za Tume ya Mabadiliko ya Katiba zimemalizika rasmi tarehe 19 Machi, 2014.

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
Dar es Salaam.

25 Machi,2014

hiyo ndiyo magamba ;;;; warioba warioba
 
Yote hiyo ni kuogopa kujibiwa na warioba mbona kafanya haraka sana kuivunja?nchi hii bana viongozi wake kama wendawazimu Rais anazungumza kama mpiga debe.
 
Sikutegemea mtu mwenye hadhi ya umod hum kutoa mawazo ya aina anayotoa. Poa lakini tuwe wakweli linapokuja suala la maoni ya wananchi.
 
Tusimlaumu sana kikwete,tuwalaumu walimpendekeza kuwa rais.kikwete kama yeye ameonyesha uwezo wake wa mwisho kiutawala.Hata ukipiga gitaa musiki hachezi tena,kwa kweli tumpongeze hapa ndio mwisho wa uwezo wake jamani.Nashangaa sana watu wanaongea sana na kumlaumu sana.alafu wengine wanasema anacheka tu ukimwona.Ni kweli.kwa fikra zake za kutatua na kupambanua mambo kwake hapo amefika mwisho wa reli[kigoma].Kikwete alijua kabisa kuwa mwisho wa kutoa maoni ya katiba ulishapita na yeye alikwenda pale Dodoma kama kama raia wa Tanzania na pia mwenyekiti wa ccm taifa na sio Rais.kwani alivyoongea inamaanisha hivyo.Tuzidi kuomba Mungu atuongoze.kumbe wenzetu wa Ghana ni wastaarabu sana kidemokrasia kuliko Watanzania.
 
Iwapo CCM itafanikiwa mipango yake kwa kufanya mawazo na matakwa ya CCM kuwa ya nchi,basi gharama ya ujinga na upuuzi wetu wote kwa kukubali hayo itakuwa juu yetu na vizazi vyetu.
 
Back
Top Bottom