Kaveli
JF-Expert Member
- Dec 4, 2012
- 5,443
- 8,903
nimekuletea hoja ya ambaye hakukaa darasani akafua umeme na kusambaza kwa wanakijiji, rais JPM akamuona akamkaribisha Ikulu lakini hakupewa kamisheni ya taifa alipewa zawadi ya kunywa chai na pesa, jiulize kwanini?
nikasisitiza zaidi ya mara kibao kuanzia post yangu ya kwanza tufanyeje kwa kuwa nchi yenu/yetu sote na kabla ya yote tusome sheria iliyopo kwanza alafu tujue tunacho kitaka kipo kwa mujibu wa sheria za nchi au tunaomba kwa hisani ya... ikimpendeza?
Je kama hakuna sheria basi tuombe itungwe sheria au twende kwa hisani? au tuendlee kualikwa ikulu watu wa kawaida kupiga picha na kunywa chai?
au zianzishwe tuzo kama za wasanii kwa ajiri ya mnao wataka?
sina cha kuongeza... tuendelee kupiga zumari kama hujui unacho kitaka na namna ya kukitafuta, watanzania tuna maisha yetu na ndio yanaonekana ktk maisha ya wengi kuanzia kuandika, kuongea, anavyoishi nk upatishida kumtambua mtanzania...
NB:
et mganga wa kienyeji ni mtu wa kawaida, usiyo yajua ktk nchi/taifa yatakusumbua sana na utaendelea kuitawenzio wa kaiwaida au kujifananisha nao wakati sio kweli...
Tuendelee kuondoa umbumbu ktk vichwa vyetu... kingereza chako kizuri sana na kikusaidie kupitia ile sheria na sharia mbalimbali za nchi ili ukiwa unachangia usichangie kama mtu usiyejua unacho andika...
Nchi inaongozwa kwa miongozo, kanuni, taratibu na sheria mbalimbali...
una ambiwa soma hutaki soma hutaki... soma sheria na taratibu hutaki una angaika watu wakawaida, hao unao waita wakawaida wanapewaje nguvu na sheria? sheria ina watambua au imewasahau? tufanyeje kama hawa onekani popote, wewe una ruka tu wakawaida, unaishia hapo hapo wakawaida...
wenzako hawa hapa... walalamishi wenzio wasio taka kusoma hata nusu ya mstali wa maandishi yaliyo andikwa kwa ajiri ya mustakhabari wa taifa lao, lakini ni wa kwanza kupiga kelele kwa kuhisi wanafahamu yote na wakiambiwa wapitie miongozo hawataki kazi kubisha, sishangai ndio watanzania rahisi kuwatambua
Askofu Gwajima: Nchi imekosa maono, kila Rais anakuja na lake, ipo siku tutajuta
Ila ana point, acheni ushabiki, ikiwa kila Rais akija anafanya yake, au anaacha ya mtangulizi wake na kufanya mengine mapya, ni hatari sana, sbb kuna mambo ni uti wa mgongo wa nchi, sasa ukikuta labda haijakamilika na kuiacha njiani, ni kukosa mipango ya maendeleo endelevu Kama Jiwe aliacha...www.jamiiforums.com
Ndgu Kijakazi aliwahi kusema jambo... nami nikasema jambo kuongezea kuwa "mtanzania anaeleweka" hakupi shida kumtambuaView attachment 2189603
1. Unauliza yule mwananchi aliyefua umeme (locally) na kuusambaza kwa wanakijiji, ni kwanini JPM alimuita Ikulu na kuishia kumtuza 'pesa' na 'chai' tu badala ya kamisheni ya Taifa?!! nakujibu kama unavyopenda kusikia: ni kwasababu Sheria hairuhusu. Sasa nikuulize, just by common sense, Sheria ni misaafu kwamba haiwezekani kuzirekebisha ama kuziboresha?
2. Nadhani 'public opinion' yaweza kuwa miongoni mwa vyanzo vya utunzi wa Sheria mpya na maboresho ya sheria zilizopo, na hizi online platforms (kama Jf) ni sehemu ya mkusanyiko wa public opinion. Decision makers kwa maana ya serikali na watunga sera & sheria hupita na kusoma maoni ya wananchi mitandaoni.
Siredi hii ya Rebecca yaweza kuwa chachu na mwanzo wa safari towards law reforms kuhusu utoaji wa tuzo hizi na kamisheni za kitaifa ambazo kwa jinsi zilivyo sasa zinaonekana kubagua wanufaika.
Hivyo, acha kung'ang'ania tu kwamba "sheria hairuhusu" au ''sheria haipo" and blah blah. Kama jambo linakuwa na tija kwa jamii, na sheria ya kulihusu haipo, sio dhambi kulitazama kwa taswira chanya ili kulirasmisha kwa manufaa ya umma. Na kwa muktadha huo ndipo siredi hii inajaribu kuchokoza fikra kwamba huko mashinani kuna watu wanajitolea michango inayogusa jamii moja kwa moja, kwanini serikali isiwatazame watu wa aina hiyo so that to motivate other like minded people? aidha kwa kutunga sheria ama kurekebisha sheria zilizopo zihusuzo masuala hayo.
3. Unasema kuwa nchi inaendeshwa kwa miongozo, kanuni, taratibu, na sheria. Ni sahihi, na ni vyema sana kuspark hiyo mentality ya utawala wa sheria kwenye jamii. Natambua kwamba katika misingi ya kisheria, kosa moja halihalalishi kosa jingine, lakini nakuuliza: Ni lini Serikali yetu (na serikali za kiafrika at majority) tuliweza kujivunia 'utawala wa sheria'? Law compliance in Tanzania bado ni changamoto kubwa sana. Nakupa mfano: Rais wa Tanzania yupo nje ya mipaka ya nchi lakini anafanya uteuzi wa watumishi wa umma wa Tanzania. Nitajie ni sheria gani ama ni Ibara ipi ya Katiba ya JMT inayompa mamlaka Rais kufanya majukumu hayo akiwa nje ya mipaka ya JMT?
4. Siredi inajaribu kuhoji kwanini kusiwepo tuzo za kitaifa kwa watu kama huyo kijana aliyefua umeme akasambazia wanakijiji; huyu mganga wa kienyeji aliyejitolea kujenga madarasa mawili ya shule ya umma; na wengineo wa namna hiyo. Wewe unapinga siredi kwa kuleta mifano ya Rais Obama kumpa tuzo makamu wake; mfalme wa Saudia kumpa tuzo Rais Trump; Rais Kikwete kumpa tuzo mama Maria Nyerere; na unaongezea mifano ya honorary academic awards kupinga siredi hii. What the heck!!
5. Nashauri, hebu jaribu kurelax na punguza lugha za kukaripia na kukera. Nadhani, kuitana 'mbumbumbu' si lugha yenye afya. Tuelimishane kwa staha na utulivu wa akili.
6. Nasisitiza tena mawazo yangu kwamba kwa kuendelea kushikilia hiyo mifano yako ya tuzo kwa viongozi; na honorary academic awards, basi bado hujaielewa mantiki halisi ya uzi huu.
-Kaveli-