Rais Biden ashauriwa kutogombea uraisi wa Marekani, sababu analiaibisha na kulivua nguo taifa lake

Rais Biden ashauriwa kutogombea uraisi wa Marekani, sababu analiaibisha na kulivua nguo taifa lake

6 Pack

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2022
Posts
2,819
Reaction score
5,996
Niaje waungwana,

Kusema ukweli kwa hali aliyofikia raisi wa Marekani mhe. Joe Biden, ni vizuri akashauriwa au akajishauri mwenyewe kuacha kugombea uraisi wa Marekani ili apate muda wa kwenda kupumzika nyumbani kwake na wajukuu zake. Ikiwa ataruhusiwa kuendelea kugombea na pengine akashinda, basi nitaamini kuwa Marekani ni nchi inayoweza kuongozwa hata na Chid Benz kikubwa tu awe mzawa na mwenye ushawishi.

Haiwezekani nchi yenye uchumi mkubwa, teknolojia kubwa na vyombo vyenye ueledi mkubwa wa kijeshi, kiuchumi, kielimu na kiintelejensia waongozwe na mtu ambae husahau jambo kila baada ya dakika 3 au 5 kupita. Inasemekana hufikia mahali hadi ya kuwasahau mawaziri wake mwenyewe. Waziri wake wa mambo ya nje anamwita Obama na muda mungine akikutana na Obama anamwita Clinton.

Juzi alikuwa katika mkutano wa G7 na viongozi wenzake. Wakati wakiwa wamesimama wakiangalia askari wa miamvuli wanavyoshuka kutoka juu, ghafla yeye (Biden) akawatoka wenzake na kuelekea upande ambao haueleweki. Baada ya mkewe kuona hali hiyo ikabidi amuwahi kwenda kumshtua kwamba huko unapoelekea ni kichakani (ni bustan yenye majani marefu mithili ya kichaka) akamuonesha walipo wenzake, ndo akarudi tena pale alipokuwa amesimama na kuendelea na sherehe yao.

Hiyo tisa, kumi na pale alipofanya kituko kingine katika ikulu ya white house. Wakati walipokuwa wanasherekea yeye na viongozi waandamizi wa ikulu, yeye akawa anatoa machoni mithili ya mtoto anaejaribu kufuatilia kitu asichokijua. Ghafla akataka kuwachomoka ili aelekee anapopajua yeye ndo watu wa karibu wakamtuliza, huku yeye akionesha wazi kusahau kinachofanyika pale 😂😂😂

Hizo picha 3 za juu ni za mkutano wa G7 jinsi alivyowatoka na jinsi mkewe alivyomrudisha katika kundi. Na hizo picha 2 za nchini na jinsi alivyotoa macho kuangalia asichokielewa na pia akitaka kuwatoka watu waliokuwepo katika sherehe hizo.

Nina imani kwa haya anayoyafanya Biden kama yangefanywa na raisi wa nchi yoyote ya Afrika, basi raisi huyo angeandamwa na vyombo vyote vya kimataifa. Ni kama alivyodhalilishwa raisi wa Sudan kwa kuambiwa kuwa kajikojolea hadharan nk.

images (3).jpeg
images (4).jpeg
images.jpeg
images (6).jpeg
images (7).jpeg
 
Trump huwa anamtania sana Biden huwa nacheka kweli😀

Ila kiukweli naungana na wewe Biden apumzike kwa usalama wa afya yake I wish Blinken aingie mzigoni kwenye kuufukuzia Urais binafsi nafikiri anafaa kabisa kuwa Rais wa U.S
Kweli kabisa. Angalau angempisha Blinken agombee kwa faida ya nchi yao. Miaka 4 imeisha, hakuna cha maana alichofanya zaidi ya kusinzia tu ofisini.
 
Kuna maraisi huwa wanawekwa mbele kama picha yenye spika ila mamlaka yanatoka somewhere else. Kuna umri binadamu akifikisha hawezi kuwa na control hata ya familia yake anajiachia tu mitoto iamue lolote sembuse nchi, ucontrol mifumo ya wizara zote na kuzitolea maamuzi?.
 
Mambo mengi muda haitoshi...


Cc: Mahondaw
Kweli kabisa, muda haitoshi hata kusoma na kurekebisha ulichoandika.

Kuhusu Joe Biden, huyo jamaa ni msanii sana kama hamjamjua. Na ana akili timamu almost all the time.

Ni kweli ana tatizo la uzee, lakini wakati mwingine huwa anafanya makusudi ili kutafuta mkogo wa vyombo vya habari (huku kwetu Bongo tunaita kutafuta kiki).
 
Back
Top Bottom