Rais Biden ashauriwa kutogombea uraisi wa Marekani, sababu analiaibisha na kulivua nguo taifa lake

Rais Biden ashauriwa kutogombea uraisi wa Marekani, sababu analiaibisha na kulivua nguo taifa lake

Wasi wasi wangu asije kusahau na kujikuta ameamuru Vita vya Nuklea kati ya Marekani na Urusi.
Hata hivyo nchi zilizoendelea kama Marekani wana mifumo imara ya Uongozi hata kama kiongozi ni dhaifu bado hakuna kinachoharibika!
 
Mmeshindwa kumshauri mama yenu mnahangaika na mataifa ambayo hata kura hampigi na hamna faida nayo
 
Yes ni kweli, lakini anayoyafanya hasa akiwa ugenini hayaleti picha nzuri kwa taifa lake. Ikizingatiwa kuwa Marekani ni nchi inayoaminiwa kuwa na watu wenye akili kubwa ulimwengu. So haifai kuongozwa na mtu wa aina ya Biden ambae mara nyingi hua hajui anachokifanya mpaka akumbushwe.
 
Mmeshindwa kumshauri mama yenu mnahangaika na mataifa ambayo hata kura hampigi na hamna faida nayo
Hata wewe unaweza kumshauri, sio lazima sisi wote tuandike kitu kimoja.
 
Biden hafai kuendelea kuongoza taifa kubwa na lenye nguvu kama Marekani. Ipo siku ataamrisha majeshi yake yaje yaivamie Tanzania akifikiri kuwa sisi ni warusi. Maana ana tatizo kubwa la kupoteza kumbu kumbu.
Lakini ana watu waliobobea kwenye kumshauri
 
Ni wapi palipoandikwa kuwa Kamara ni mke wa Biden mkuu?
Kwenye mada umesema kuwa mke wake ndie aliyemrudisha baada ya kuona anaenda sehemu sio ila kwenye picha anaonekana Kamara ndie anayemrudisha
 
Marekani kuna vijana wa hovyo kweli mpaka wanawapa nchi Macyborg, huyu Biden inaonekana alishakufa kitambo hili linalotembea ni Robot Mtu tu (Cyborg)
 
Lakini ana watu waliobobea kwenye kumshauri
Hiyo ndio bahati yake. Laiti ingekuwa hawa viongozi wetu wa kiafrika ambao mara nyingi hawashauriki basi hilo kwao lingewezekana.
 
Kwenye mada umesema kuwa mke wake ndie aliyemrudisha baada ya kuona anaenda sehemu sio ila kwenye picha anaonekana Kamara ndie anayemrudisha
Hapana sisi wote tumekosea. Alikuwa ni waziri mkuu wa Italy anaitwa Giorgia Meloni. Kamara anaonekana katika hizo picha 2 za chini ambazo sherehe yao ilifanyikia white house.

Marekani na mataifa makubwa yalioendelea hawana utaratibu wa viongozi wa juu serikalini kama vile raisi na makamu wake waende nje ya nchi katika ziara moja ambayo ingeweza kuhudhuriwa na kiongozi mmoja tu huku mungine akibaki nyumbani kuendelea na majukumu ya taifa.
 
Marekani kuna vijana wa hovyo kweli mpaka wanawapa nchi Macyborg, huyu Biden inaonekana alishakufa kitambo hili linalotembea ni Robot Mtu tu (Cyborg)
Imagine nchi yenye muamko wa vijana wasomi, wazalendo na wenye muamko inakwenda kupewa wazee ambao, hata zile shughuli za kitandani mpaka akumbushwe na mkewe ndo ajue kuwa kuna kunaniliu.

Hii si dharau kwa nchi na vijana wa taifa lao. Ni kama kile walichofanya wanaijeria.
 
Biden umri n tatzo...
..Mutuulize babu yako mwenye miaka 81 kama unaweza kufanya vikao 10 kwa siku.
Ndomaana anatakiwa ashauriwe ili akapumzike na wajukuu nyumbani. Asing'ang'anie kuongoza nchi kama baadhi ya viongozi wetu wa kiafrika.

Ameshatawala miaka minne, lakin umri na afya yake vinaonekana kukataa yeye kuendelea kutawala. Basi awaachie vijana wengine waje waisogeze nchi kwa kasi ya maendeleo.

Sio kung'ang'ania kufadhili vita mbali mbali halaf China wakipiga hatua anakimbilia kutaka kuweka vikwazo, wakati yeye uchumi wake anauelekeza vitani.
 
Amesahau hadi kutuma kombora Yukrein
We subiri siku asahau na kupeleka makombora ya nyuklia North Korea badala ya kuyapeleka South Korea, hapo ndo watapojua kwamba mzee amebaki na mwili tu ila akili tayari imeshaondoka zake 🤣🤣
 
We subiri siku asahau na kupeleka makombora ya nyuklia North Korea badala ya kuyapeleka South Korea, hapo ndo watapojua kwamba mzee amebaki na mwili tu ila akili tayari imeshaondoka zake 🤣🤣
Kitakacho fata ni Misiba na matanga
😂😂
 
Back
Top Bottom