Rais Biden, kwa Afrika anza na Rais Magufuli na Mwinyi wa Zanzibar

Rais Biden, kwa Afrika anza na Rais Magufuli na Mwinyi wa Zanzibar

Kwa Afrika Tanzania ni kituo kikuu cha Amani na uwajibikaji, tunayo Demokrasia na mihimili inayojitegemea ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika.
Wezi wa kura ukiokubuhu!! Kutesa na kupoteza watu!! Kubambikia watu makosa hasa wale wanaojitolea kuikosoa Serikali kwa nia njema kabisa ya kujenga nchi.

Biden ni mcha Mungu as a person; hatataka kabisa kusikia hizi story za chaguzi za Africa - hasa za M7 na genge lake na sisi wa TZ tunavyoibaka demokrasia.
 
Yaani BIDEN usicheke na kima, Tanzania tumeshuhudia vyombo vya ulinzi na usalama vilivyokuwa vikiua watu hadharani mtaani.
Tumejionea kwa macho udanganyifu mkubwa na wizi wa kura.

Deogratias Mutungi Tanzania nzima hamna Mhaya wa hovyo kama wewe.
BIDEN KAANZA KWA KUZUIA MAANDAMANO YA WANANCHI. NDIYO UJUE MAANDAMANO NI HARAMU SIYO HAKI
 
Yaani BIDEN usicheke na kima, Tanzania tumeshuhudia vyombo vya ulinzi na usalama vilivyokuwa vikiua watu hadharani mtaani.
Tumejionea kwa macho udanganyifu mkubwa na wizi wa kura.

Deogratias Mutungi Tanzania nzima hamna Mhaya wa hovyo kama wewe.
Umekosea. Yupo tena anaenda kwa jina kama hilo. Huyu ni wa id feki lakini yule anafahamika. Nadhani hilo jina lina shida. Jina lenye maana ya tajiri! Kuna dhana kuwa ili kutajirika sharti kuiba. Kwa hawa kupata uteuzi sharti kujitoa ufahamu!
 
Yaani BIDEN usicheke na kima, Tanzania tumeshuhudia vyombo vya ulinzi na usalama vilivyokuwa vikiua watu hadharani mtaani.
Tumejionea kwa macho udanganyifu mkubwa na wizi wa kura.

Deogratias Mutungi Tanzania nzima hamna Mhaya wa hovyo kama wewe.
Umempa bwana Mtungi za uso ...hahahaha hiyo sentence ya mwisho sio poa!
 
Biden ni mtetezi mkubwa sana wa demokrasia ya ukweli.
Secretary of State Blinken ni mwanausalama aliye mfuasi mkubwa mno wa misimamo ya B. Obama kuhusu Afrika na demokrasia yake.

Biden ni mwiba mkali kwa wanaokandamiza demokrasia na haki za binadamu( anaunga mkono ndoa za jinsi moja na haki za LGBT.
Na Biden ana mtazamo kama huu.
 
Angekuwa mtetezi wa demokrasia angepinga mitandao kumfungia trump..maana ndio demokrasia.
Wewe wa wapi wewe? Apinge mitandao kumpiga pini huyo chizi aliyechochea watu wafanye vurugu kwani na yeye ni muumini wa political violence?
 
Salaam JF,

Baada ya Rais Biden kuapa Jana Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa mawasiliano ya kwanza ya simu yatakayofanywa na Rais Biden ni kati yake na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, bila Shaka kigezo na hoja kuu ni kwa jinsi utawala wa Canada unazingatia sheria, Demokrasia na uwajibikaji kwa Wananchi wake na taasisi zake.

Kwasababu kinachofanyika Canada na Tanzania ni sawa, Aidha misimamo ya Sasa ya JPM na uwajibikaji wake kiuchumi na kifursa kwa Wananchi wake.

Pia uwezo wa Rais mpya wa Zanzibar Dkt. Mwinyi anayeonesha alama ya uwajibikaki na Mapinduzi mapya katika ustawi wa amani uchumi, nashauri na kuomba iwe sababu muhimu ya Ubalozi wa Marekani Tanzania kuyatambulisha yote haya kwa Biden ili mazungumzo yanayofata yawe kati ya Rais Biden na viongozi wetu hawa Wazalendo.

Kwa Afrika Tanzania ni kituo kikuu cha Amani na uwajibikaji, tunayo Demokrasia na mihimili inayojitegemea ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika.

Aidha historia ipo wazi kati yetu na Marekani, Kwa Mantiki hiyo Tanzania ipewe kipaumbele zaidi katika mawasiliano ya awali na Rais Biden kwa manufaa ya nchi na Africa kwa ujumla kiuchumi, Kisiasa na kijamii nina imani ili litatimia hivi karibuni.
Baiden hawezi kuongea na watu ambao hawataki kuhimiza watu wanawe mikono wameacha wageni kuingia bila kupimwa wameingiza corona ya kutosha Tanzania imeanza kuua watu kwa speed
 
Back
Top Bottom