vvti engine
Senior Member
- Nov 15, 2018
- 188
- 209
Nukuu yako tu ya mathayo 28:19 imekukataa.Mwenyewe Bwana yesu alijua mipaka ya utume wake.
Kwa hiyo alisema:
1. Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:24).
2. Wakati mwanamke mmoja asiyekuwa mwana wa Israeli alipokuja kwa Yesu Kristo kuomba baraka zake, Yesu akakataa na zaidi ya kukataa aliwatusi wasiokuwa Waisraeli. “Akasema si vyema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia m’mbwa.” (Mathayo 15:26, Marko 7:27).
3. Hao thenashara (kumi na mbili) Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, katika njia ya mataifa msiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie. Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
(Mathayo 10:5-6).
4. Baadhi ya Wakristo mnadhani kwamba wakati Waisraeli wote wamefikishiwa ujumbe, kisha makabila mengine pia yahubiriwe.
Lakini dhana hii si sahihi bali ni kinyume cha mafundisho ya Bwana Yesu.
Yeye amesema kwamba:
“Lakini watakapo wafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawambia, hamtaimaliza miji ya Israeli hata ajapo mwana wa Adamu. (Mathayo 10:23).
5. Bwana Petro mwanafunzi wa Yesu Kristo aliwahubiri wasiokuwa Waisraeli. Wanafunzi wengine, baada ya kupata habari hii walimpinga Bwana Petro kwa kosa lake. Biblia inasema kwamba:
“Basi mitume na ndugu waliokuwako katika Uyahudi wakapata habari ya kwamba watu wa mataifa nao wamelipokea neno la Mungu. Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye, wakisema, uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao. “ (Matendo 11:1-3).
6. Aya za Biblia zifuatazo zinaeleza kwamba Bwana Yesu alikuwa mfalme na mtawala wa Mayahudi. (Mathayo 2:6, 27:29, 27:42, Yohana 1:49. 7.
Bwana Paulo ambaye ni mpinzani na mhalifu (anti Christ) wa Bwana Yesu, baada ya kuchukia alianza mahubiri nje ya Wasiraeli.
Biblia inasema kwamba:
“Hata Sila na Timotheo walipoteremka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na bila neno, aliwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo ,walipopingana naye na kumtukana Mungu akakung'uta mavazi yake, akawaambia, damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu, mimi ni safi; tangu sasa ninakwenda kwa watu wa mataifa. (Matendo 18:5-6).
Baadhi ya Wakristo mnayo shauku ya kugonganisha aya za Biblia. mnasema kwamba Bwana Yesu aliagiza kwamba
“Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi.” (Mathayo 28:19).
1. Najibu kwamba aya hii inapinga maagizo yote ya Bwana Yesu yaliyotajwa juu. Kwahiyo haiwezi kuwa agizo la Yesu wala aya ya Injili.
2. Ya pili aya hii imeandikwa mwishoni mwa Injili ya Mathayo, na nitathibitisha baadaye kidogo kwamba aya za mwanzo na za mwisho za kila kitabu ni za kuongezwa baadaye. Aya zile siyo aya sahihi za Biblia.
3. Ya tatu katika aya 28:19 ya Mathayo neno mataifa limetumika kwa maana ya mataifa ya Israeli.
Kama Biblia inavyosema kwamba:
“Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu. (Luka 2:1).
Kaisari Augusto alikuwa mtawala wa Roma tu. Hakuwa na mamlaka yoyote nje ya nchi yake juu ya ulimwengu.
Katika aya hii amri iliyotolewa kwa ajili ya ulimwengu na ya nchi ya Roma tu iliyokuwa chini ya utawala wa Kaisari wala siyo ulimwengu wote.
Hivyo ndivyo inavyoeleweka kauli ya Bwana Yesu aliposema: “Enendeni mkawafanye mataifa yote (ya Waisraeli) kuwa wanafunzi. (Mathayo 28:19).
Warumi 1:15-17. Mwamini Yesu uende mbinguni acha kuufanya moyo wako kuwa mgumu.Mwenyewe Bwana yesu alijua mipaka ya utume wake.