Hili kombe la VPL ni dogo sana.
Dar es Salaam Young Africans ambao wamechukua kombe mara nyingi kuliko Simba na mara ya mwisho wakalichukua kwa miaka minne mfululizo, hawajawahi kumwita hata katibu kata kwenda kuwakabidhi.
Rais aliyepita alikuwa Yanga damu lakini hajawahi kualikwa na wanayanga kwenda kukabidhi kombe.
Kifalsafa hii ya Rais kwenda kukabidhi kombe la VPL ambalo linashindaniwa kila mwaka na lazima timu moja ya Tanzania ishinde halijakaa vizuri.
Je mwakani Singida united wakichukua kombe ataitwa Rais kuja kukabidhi?
TFF wanatengeneza' precedence ' ambayo inaweza kuchafua hali ya hewa baadaye kwa timu zingine kuheshimawa zaidi kwa sababu ya unazi na zingine kudharauliwa.
Hayati Mwalimu Nyerere kwa wale wasoi jua Historia alipewa kadi namba moja Yanga lakini hadi anafariki hajawahi kuonyesha dalili ya unazi wake Yanga.
Siasa za Inchi hii zilianzia kwenye vilabu vya mpira wa miguu na hasa Yanga.
Harakati za kuikomboa Inchi toka kwa Wakoloni zilianzia Yanga.
Simba ilikuwa ya Wahindi na Waarabu (angalia rangi zao).
Kuna siku moja mshabiki wa SIMBA alimwendea Nyerere na kumwomba awaambie Yanga wabadili rangi ya jezi zao kwa sababu zinafanana na za TANU. Nyerere alimwambia , wewe mjinga sana, Yanga tuliwakuta na rangi zao, labda ungeniomnba sisi TANU tubadili rangi zetu.
Ingefaa sana kama Simba wangeshinda kombe la Africa ingekuwa haki Serikali yote kuhamia Uwanja wa taifa kupokea kombe.
Unaweza kuigawa inchi kwa kiongozi mkuu kushabikia klabu za mpira kwani ushabiki wa mbira ni tabaka sawa na matabaka ya Dini, kabila au hata vyama vya Siasa.