Rais Dkt. John Pombe Magufuli Mgeni Rasmi Sherehe Za kukabidhi Kombe Kwa Bingwa Wa VPL Leo Tarehe 19/05/2018

Rais Dkt. John Pombe Magufuli Mgeni Rasmi Sherehe Za kukabidhi Kombe Kwa Bingwa Wa VPL Leo Tarehe 19/05/2018

Cybercrime

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2014
Posts
3,246
Reaction score
1,113
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatarajia kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kukabidhi kombe kwa bingwa wa ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2017/2018. Rais Magufuli atawakabidhi Simba 'Sports Club' maarufu kama Wekundu wa Msimbazi leo mara tu baada ya mchezo wao dhidi ya timu ya Kagera Sugar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mchezo wa Simba na Kagera utaanza majira ya saa nane kamili mchana.
Tujitokeze kwa wingi , tuungane na Rais wetu kunogesha shamra shamra za wana msimbazi.

Shughuli ni watu, Karibuni sana.
 
saa tano tu nitakuwa nimeshatinga uzi wangu wa simba nakuja taifa, leo raha tu, tena kombe tunakabidhiwa na presidaaa, acha kabisa
 
Akizungumzia madeni ya watumishi wa umma ntafurahi sana
 
saa tano tu nitakuwa nimeshatinga uzi wangu wa simba nakuja taifa, leo raha tu, tena kombe tunakabidhiwa na presidaaa, acha kabisa
Halafu kesho tuwasikie mnalalama vyuma vimekaza wapumbavu wakubwa, mtu anawatesa halafu anawatumia TFF kuteka akili za mazuzu pumbavu kabisa.

Nashauri Magu akamatie hapohapo mpaka Watanzania wapate adabu.

Maana hakuna nchi duniani yenye raia mizigo kama Tanzania. Mmeshasahau dhiki zote tunazoletewa na watu hawahawa sasa mwaenda kufurahia nini? Hopeless kabisa.
 
Majitu yana chuki binafsi na roho mbaya tu. Bakini na roho mbaya zenu lakini Wekundu wa Msimbazi tunakabidhiwa kombe jipya la VPL champion na mheshimiwa Rais.

Hata wenye chuki zenu kwa Rais mjinyonge tu maana haisadii atakuwa Rais wenu hadi 2025 na mtakomaa hadi roho zitaota kutu. Tuzidi tu kumwombea Mungu amlinde na kumweka hai.

Magufuli nyoosha wazembe na wanaoishi kwa akili za kushikiwa na mafisadi. Pumbaf zao yamejaa chuki tu.
 
ingekuwa Azam Tv hawaoneshi live asingeenda. anafosi aonekane kwenye TV tu hakuna jipya. nilipanga leo niende uwanjani lakini hata jezi yangu ya Simba sivai.


Hata ikiwa Azam wasingeonwsha TBC1 huwa inamfata kila kona ingeonesha live.
BTW uende au usiende, uvae jezi au usivae haisaidii kitu matokeo yake utaumia na roho yako ya chuki kwa Magu lakin huyo ndo Rais wako hadi 2025
 
Halafu kesho tuwasikie mnalalama vyuma vimekaza wapumbavu wakubwa, mtu anawatesa halafu anawatumia TFF kuteka akili za mazuzu pumbavu kabisa.

Nashauri Magu akamatie hapohapo mpaka Watanzania wapate adabu.

Maana hakuna nchi duniani yenye raia mizigo kama Tanzania. Mmeshasahau dhiki zote tunazoletewa na watu hawahawa sasa mwaenda kufurahia nini? Hopeless kabisa.
TFF wamwalike au wasimwalike, akabidhi kombe au asikabidhi hakutalainisha vyuma vyako. Jifunze kuishi kulingana na wakati
 
Yaani simba wanaroho mbaya hadi mto msimbazi wameamua kuupitishia kwenye eneo LA yanga na huwa unamwaga kwenye uwanja wao Kaunda unakua kama bwawa LA samaki na leo wanapewa kombe na presdaa

Acheni roho mbaya simba
 
Hili kombe la VPL ni dogo sana.
Dar es Salaam Young Africans ambao wamechukua kombe mara nyingi kuliko Simba na mara ya mwisho wakalichukua kwa miaka minne mfululizo, hawajawahi kumwita hata katibu kata kwenda kuwakabidhi.
Rais aliyepita alikuwa Yanga damu lakini hajawahi kualikwa na wanayanga kwenda kukabidhi kombe.
Kifalsafa hii ya Rais kwenda kukabidhi kombe la VPL ambalo linashindaniwa kila mwaka na lazima timu moja ya Tanzania ishinde halijakaa vizuri.
Je mwakani Singida united wakichukua kombe ataitwa Rais kuja kukabidhi?
TFF wanatengeneza' precedence ' ambayo inaweza kuchafua hali ya hewa baadaye kwa timu zingine kuheshimawa zaidi kwa sababu ya unazi na zingine kudharauliwa.
Hayati Mwalimu Nyerere kwa wale wasoi jua Historia alipewa kadi namba moja Yanga lakini hadi anafariki hajawahi kuonyesha dalili ya unazi wake Yanga.
Siasa za Inchi hii zilianzia kwenye vilabu vya mpira wa miguu na hasa Yanga.
Harakati za kuikomboa Inchi toka kwa Wakoloni zilianzia Yanga.
Simba ilikuwa ya Wahindi na Waarabu (angalia rangi zao).
Kuna siku moja mshabiki wa SIMBA alimwendea Nyerere na kumwomba awaambie Yanga wabadili rangi ya jezi zao kwa sababu zinafanana na za TANU. Nyerere alimwambia , wewe mjinga sana, Yanga tuliwakuta na rangi zao, labda ungeniomnba sisi TANU tubadili rangi zetu.
Ingefaa sana kama Simba wangeshinda kombe la Africa ingekuwa haki Serikali yote kuhamia Uwanja wa taifa kupokea kombe.
Unaweza kuigawa inchi kwa kiongozi mkuu kushabikia klabu za mpira kwani ushabiki wa mbira ni tabaka sawa na matabaka ya Dini, kabila au hata vyama vya Siasa.
 
Back
Top Bottom