Kuna ukweli wa baadhi ya unayoyasema, ila umekwenda mbali sana na kuwa extremist. Nakukumbusha tuu urejee kukuwa kiviwanda na kiuchumi kwa China kumesababishwa na nini kama siyo FDI (Foreign Direct Investiment). Uchumi wa China hadi mwaka 1978 ulikuwa wa kudhibitiwa na serikali na ulikuwa ni mdogo kuliko uchumi wa Italy, na kitu kikubwa walichokuwa wana export ni gazeti la Guoz Shudian! Ni kwa kufika kwa Deng Xiaoping na kuufungulia uchumi kwa kuruhusu foreign investment ndipo uchumi ukaanza kukuwa hata kufikia 9.0 kwa miaka zaidi ya 20. Hakuna sababu nyingine yeyote isipokuwa foreign invcestment. Lakini FDI inataka pia kuwepo na discipline, nidhamu, ndiyo ifanikiwe. Wachina walifanikiwa kwa vile walikomesha rushwa kweli kweli, hivyo kila mwekezaji alikuwa anafuata sheria na kulipa kodi kama ipasavyo. Wakati huo huo, Wachina wenyewe wakawa wanatazama na kuiga yale yanayofanywa na wageni katika Nyanja zote. Nakumbuka kuna wakati Uchina ilinunua kiwanda kidogo cha pikipiki Italy mwaka 79-80. Wakapeleka mafundi wao wakakikongoa chote wakakihamishia China. Leo hii hakuna anayemshindwa Mchina kwa ku export pikipiki duniani! Hivyo ni makosa kusema uwekezaji wa kigeni hauna manufaa, bali ni sisi wenyewe ndiyo hatufuati masharti ya kufanya FDI ifaulu. Mtu anayechukuwa 10% na kuacha nchi iwe shamba la bibi...unategemea nini?
Ndiyo maana huu mwanzo wa magufuli unaweza kutupeleka mbali sana kama ukidumishwa kwa miaka mingine 20.