Tetesi: Rais Dkt Magufuli kufanya ziara nchini China

Tetesi: Rais Dkt Magufuli kufanya ziara nchini China

China ni washiriki wetu kihistoria hivyo ni sahihi kwake kwenda huko, isitoshe China hawana tabia ya kuingilia mambo yako ya ndani kama walivyo wa magharibi. Sijui haki za binadamu mara ushoga sijui nini

Ila wanaifadhili sana CCM nu kuwasaidia kukandamiza democracy
 
HIYO SAFARI ATAWAKILISHWA NA JK
Kwa mujibu wa duru muhim ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje, Mheshimiwa Rais anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini China baadae mwezi huu.

Katika ziara hiyo Pamoja na matukio mengine Mhe Raisi atashiriki mazungumzo na kusaini makubaliano mbalimbali juu ushirikiano wa China na Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Kadhalika Mheshimiwa atatunukiwa Shahada ya juu ya heshma toka chuo kikuu kimojawapo mashuhuri Jijini Beijing.
 
JK alimtaka uyo wa kwenye avatar yako!hakua na uweledi wa kumuibua JPM,husu ni faida ya vita panzi tu,Mungu alishapanga aje mtu makini manake Jk alishafanya ikulu shamba la bibi!sijui anajionaje akiwa msoga jinsi jamaa anavyopambana na wale aliokua anawalinda kwa hali na mali.Ritz moja naye hasikiki kabisa saivi,jpm noma sana japo inshu ya zenji kaboronga na itamcost kwy legacy yake
Sasa JPM ameibuliwa na nani kama sio JK? Amemkata Lowasa angeshindwaje kwa Magufuli kumkata akamuweka Membe?
 
Usinilazimishe nikudharau kama Mh.Jussa Ladhu alivyomdharau Mpanju.Ziara pekee ninazoweza kuzihesabu kama ziara zenye tija kwangu ni zile zilizofanywa na Mwl.Nyerere(R.I.P)za kwenda Uingereza "kufuatilia Uhuru wa Tanganyika".

Zaidi ya hapo sioni cha Maana toka kwa hao unaowaabudu.Kama ni suala la uwekezaji,hakuna uwekezaji wowote uliowahi kufanywa na mgeni ukaleta tija kwa Taifa letu.Uwekezaji unaokomba Rasilimali zetu huku Taifa likiambulia Mlabaha wa 3% kwangu mimi sioni kama ni jambo la kujivunia kiasi cha kupongeza ziara za ng'ambo.

Iko wapi mikataba 17 iliyisainiwa Ikulu baina ya Uchina na Tanzania? Imeleta tija gani kwa Taifa letu? Wachina hao unaowashabikia ndiyo walioligeuza Taifa letu kuwa " dampo"la kutupia kila aina ya bidhaa feki toka uchina kwa kisingizio cha kukuza biashara kati yetu.Leo hii hadi baadhi ya member wa jf wapo hatarini kutoweka jukwaani kwa sababu ya kutumia "vifaa feki" vya kichina.

Sijaona mchango wa maana ulioletwa na Uchina,zaidi sana Wachina ndiyo wanaonufaika na kandarasi za miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo inafadhiliwa na Mataifa mengine,Wachina wanatajirika zaidi toka kwetu kuliko sisi tunavyopokea toka kwao.

Kuna ukweli wa baadhi ya unayoyasema, ila umekwenda mbali sana na kuwa extremist. Nakukumbusha tuu urejee kukuwa kiviwanda na kiuchumi kwa China kumesababishwa na nini kama siyo FDI (Foreign Direct Investiment). Uchumi wa China hadi mwaka 1978 ulikuwa wa kudhibitiwa na serikali na ulikuwa ni mdogo kuliko uchumi wa Italy, na kitu kikubwa walichokuwa wana export ni gazeti la Guoz Shudian! Ni kwa kufika kwa Deng Xiaoping na kuufungulia uchumi kwa kuruhusu foreign investment ndipo uchumi ukaanza kukuwa hata kufikia 9.0 kwa miaka zaidi ya 20. Hakuna sababu nyingine yeyote isipokuwa foreign invcestment. Lakini FDI inataka pia kuwepo na discipline, nidhamu, ndiyo ifanikiwe. Wachina walifanikiwa kwa vile walikomesha rushwa kweli kweli, hivyo kila mwekezaji alikuwa anafuata sheria na kulipa kodi kama ipasavyo. Wakati huo huo, Wachina wenyewe wakawa wanatazama na kuiga yale yanayofanywa na wageni katika Nyanja zote. Nakumbuka kuna wakati Uchina ilinunua kiwanda kidogo cha pikipiki Italy mwaka 79-80. Wakapeleka mafundi wao wakakikongoa chote wakakihamishia China. Leo hii hakuna anayemshindwa Mchina kwa ku export pikipiki duniani! Hivyo ni makosa kusema uwekezaji wa kigeni hauna manufaa, bali ni sisi wenyewe ndiyo hatufuati masharti ya kufanya FDI ifaulu. Mtu anayechukuwa 10% na kuacha nchi iwe shamba la bibi...unategemea nini?
Ndiyo maana huu mwanzo wa magufuli unaweza kutupeleka mbali sana kama ukidumishwa kwa miaka mingine 20.
 
Kwa mujibu wa duru muhim ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje, Mheshimiwa Rais anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini China baadae mwezi huu.

Katika ziara hiyo Pamoja na matukio mengine Mhe Raisi atashiriki mazungumzo na kusaini makubaliano mbalimbali juu ushirikiano wa China na Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Kadhalika Mheshimiwa atatunukiwa Shahada ya juu ya heshma toka chuo kikuu kimojawapo mashuhuri Jijini Beijing.
Wachina nao wameanza kuiga uchawi wa wazungu wa tunuku, toa msaada, saini mikataba. Sasa jamani JPM kaingia juzi anatunukiwa nini tena?

Mwaka ule ilisainiwa mikataba 26 katika oparesheni Okoa dogo na sasa tena mikataba ya Oparesheni badili MCC, tutakoma.

Sijui wakikumbuka ile meli yao ya uvuvi itakuaje? any way JPM aombe tu msamaha waishane.

Wachina nao wameanza kuiga uchawi wa wazungu wa tunuku, toa msaada, saini mikataba. Sasa jamani JPM kaingia juzi anatunukiwa nini tena kama si yale yale ya kutaka kumchanganya kumchanganya na matuzo, manishani, mashahada
?

Mwaka ule ilisainiwa mikataba 26 katika oparesheni Okoa dogo na sasa tena mikataba ya Oparesheni badili MCC, tutakoma.

Sijui wakikumbuka ile meli yao ya uvuvi itakuaje? any way JPM awawahi awaombe tu msamaha waishane.
 
Afikapo huko pia namuombea ashawishike kuiga mbinu wanazotumia wenzetu kupambana na wahujumu uchumi kwa maana ya kupeleka muswada bungeni na kupitishwa sheria kali na zitakazo tekelezwa.Pia sheria ieleze huyo mtoa hukumu akibainika ameleta huruma kwa namna yoyote ile afanywaje.Hapo hakuna atakae kua tayari kufa ili mwenzake aishi
 
Baada ya kelele zooote hapo kwenye mikataba ndiyo mtamuona ngosha kuwa hana tofaut na wenzake
 
Tafadhali sana mumshauri JPM asiende na gari China ili kubana bajeti maana China ni mbali.
 
Mwambieni plz asipande melii maana somalia watamuweka kwapanii
 
Yaani kuna watu wanalipwa kusifia kila kitu, hata chembe ya fikra hakuna,
 
Akishapewa shahada ya heshima ya kichina, basi tena, atakuwa fake kama bidhaa za kichina. Yale yale
Kwa taarifa yako hata Wamarekani wenyewe wanatumia bidhaa za kichina. Uchaguzi ni wako mwenyewe ukitaka fake utapata fake na ukitaka genuine ndio utakayopata kutoka china
 
CCM wamebadilishia gia angani awamu hii bakuli haliendi tena kwa wazungu linaenda kwa wachina, sijui watatuambia ni msaada au zawadi?! maajabu hayaishi nchi hii.
Mkuu hebu jaribu kusema " nchi yetu ina kilakitu hatutaki hiyo misaada ya MCC' huku umebana pua na kuangalia juu kidogo halafu nipe majibu
 
Marekani wanaogopa sana kasi ya china katika kuliteka bara la Africa. Wamegundua kuwa utawala wa sasa hautalinda sana maslahi yao ndio maana wanaleta zengwe. China wao ni opportunistic kwa sababu wamecheza game Na kuiwini serikali ya ccm kwenye uchaguzi wa Zanzibar pale waliposema uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa huru na haki. Waliyasema hayo wakati nchi za magharibi na Europe zimepinga na kusema kinyume chake. China wamefurahi sana kususa kwa marekani ili wao wale.
 
Tunataka mikataba ya uwazi na ipelekwe Bungeni
Hilo ndilo muhimu ingawa upo wasi wasi mkubwa juu ya mikataba ya viongozi wetu kupelekwa bungeni kwani sio utaratibu wa chama chao.Hatuna hofu kubwa kuwa raisi Magufuli kuweza kuingia mikataba ya kifisadi ila ni wakati sasa wananchi kufahamishwa kupitia bunge lao mikataba yote ya kimataifa inayoingiwa na serikali yao.Inatia shaka na hofu kubwa pale raisi anapoingia mikataba zaidi ya ishirini mara moja na yote kuwekwa siri kwa wananchi.Tutakuja kustuka nchi imewekwa rehani.Tulimsikia akiwa Rwanda kuwa hotuba aliyoitoa huko kwa lugha ya kiingereza ingekuwa ya mwisho vinginevyo zitakazofuata zitakuwa kwa lugha ya taifa letu yaani kiswahili.Kwangu naunga mkono uamuzi huo.Nasema aende ila ajihesabie na siku za kuwepo huko zisiwe nyingi na msafara usiwe mkubwa.
 
Back
Top Bottom