Wawili hawa nawajua vyema sana. Mmoja ni kaka yangu na mmoja ni kama mtoto wangu. Maalim Seif Sharrif Hamad nilimkuta UDSM. Akaniacha miaka kadhaa pale yeye akimaliza mapema. Maalim, kama ilivyokuwa kwangu na kwa Zitto, alikula shavu la kiserikali mara tu baada ya kumaliza Chuo Kikuu. Taratibu tamu kama zabibu zilikamilishwa wakati wa masomo yetu. Na si sisi tu, wengi tu nawajua na wamepita njia hizo.
Kuanzia hapo kwenye kula shavu la kiserikali, Maalim Seif na Zitto hawakuwahi na hawatakuwa wapinzani. Hawana tofauti yoyote na mtani wangu Benard Membe. Kila walifanyalo kwenye maigizo na mwamvuli wa upinzani ni ubatili mtupu. Hivi hamzioni tofauti zao na wengineo? Maalim Seif alikuwa Waziri Kiongozi kule Visiwani na Makamu wa Pili wa Rais. Amerejea tena kwenye Umakamu. Kwanini yeye tu? Yeye ni mtiifu kwa mfumo.
Mnajua kwanini Zitto, pamoja na kutishia na kutangaza mara kwa mara akiwa CHADEMA, hagombei Urais? Hataki kujiharibia. Hataki kugombana na wazazi na walezi wake. Ndiyo maana anajiweka mbali na Urais na kuzuga kama vile anamuunga mkono mgombea mwingine wa upinzani. Nchi ina mambo sana hii. Kitendo cha Zitto na Maalim Seif kukubali kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa kule Zanzibar, kwangu mimi, hakinishangazi. Nawajua nje ndani hawakuwahi kuwa wapinzani.
Mwaka 2020 hakukuwa na uchaguzi, kulikuwa na uchafuzi!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam