Rais Dkt. Samia azindua ujenzi wa meli nne za mizigo, Bandari ya Kigoma | 20 Julai, 2026

Rais Dkt. Samia azindua ujenzi wa meli nne za mizigo, Bandari ya Kigoma | 20 Julai, 2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Rais Samia Suluhu Hassan, leo Julai 20, 2026, amezindua rasmi mradi wa ujenzi wa meli nne za mizigo katika Bandari ya Kigoma, hatua inayolenga kuimarisha usafirishaji wa mizigo katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika.

Uzinduzi huo umefanyika wakati wa ziara ya Rais Samia mkoani Kigoma, ambapo amesema mradi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuboresha miundombinu ya uchukuzi na kuongeza ufanisi wa huduma za bandari ili kuchochea biashara na ukuaji wa uchumi.

Soma Pia: Rais Samia anawaapisha Viongozi Wateule, Ikulu Dar es Salaam | 01 Julai, 2026

Meli hizo zinatarajiwa kuongeza uwezo wa kusafirisha mizigo ndani na nje ya Tanzania kupitia Ziwa Tanganyika, huku zikirahisisha shughuli za kibiashara kati ya Tanzania na nchi jirani zinazotumia ziwa hilo, ikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Zambia.

Mradi huo unasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na unatarajiwa kuimarisha nafasi ya Bandari ya Kigoma kama kitovu muhimu cha usafirishaji na biashara katika ukanda wa Maziwa Makuu.
 
Hio ingefanywa hata na waziri tu angetosha! Safari ya Rais ina cost sana.
 
Sijasikia KAULI yake yoyote ILA Nimesikia yule MBUNGE wa Tatu kuwa na elimu Ndogo Bungeni akilindima.

JE raia ameisha KUJUA Hana mvuto tena so anaogopa KUONGEA mbele ya HADHARA?
 
Mi niliona clip tu anaongelea vijana wanakula sana chips yai sijui zege sasa nguvu zinapungua za kuchakata..sasa sijui ndio ilikuwa sehemu ya uziduzi huo maana sikuendelea hata kusikiliza.
 
Huyo mchakata Pumba sijawahi na sidhani kama nitawahi kumsikiliza,Huwa nikipita mtandaoni nikiona clip zake nascroll fasta nisije kuona Aibu!
 
Back
Top Bottom