Sun Zu
JF-Expert Member
- Mar 16, 2022
- 636
- 1,819
Ofisi ya Rais wa Ufilipino imeripoti kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Rodrigo Duterte, baada ya kupokea ombi kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Duterte alikamatwa Jumanne katika Uwanja wa Ndege wa Manila alipowasili kutoka Hong Kong, kwa mujibu wa serikali ya Ufilipino.
Duterte anakabiliwa na tuhuma za “uhalifu dhidi ya ubinadamu” kutokana na kampeni kali ya kupambana na Dawa ya kulevya wakati wa uongozi wake.
Kulingana na hati ya kukamatwa, kampeni yake maarufu kama “vita dhidi ya dawa ya kulevya”, alipokuwa Rais kutoka 2016 hadi 2022, iliwanyima washukiwa “haki ya mchakato wa kisheria” na ilisababisha vifo vya maelfu ya watu, wakiwemo watoto.
Akijitetea dhidi ya ripoti za uwezekano wa kukamatwa kwake, Duterte hapo awali alisema kuwa alifanya “kila kitu…kwa ajili ya watu wa Ufilipino”.