Rais Duterte wa Ufilipino Akamatwa, kupelekwa ICC

Rais Duterte wa Ufilipino Akamatwa, kupelekwa ICC

Sun Zu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2022
Posts
636
Reaction score
1,819
Ofisi ya Rais wa Ufilipino imeripoti kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Rodrigo Duterte, baada ya kupokea ombi kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Duterte alikamatwa Jumanne katika Uwanja wa Ndege wa Manila alipowasili kutoka Hong Kong, kwa mujibu wa serikali ya Ufilipino.

Duterte anakabiliwa na tuhuma za “uhalifu dhidi ya ubinadamu” kutokana na kampeni kali ya kupambana na Dawa ya kulevya wakati wa uongozi wake.

Kulingana na hati ya kukamatwa, kampeni yake maarufu kama “vita dhidi ya dawa ya kulevya”, alipokuwa Rais kutoka 2016 hadi 2022, iliwanyima washukiwa “haki ya mchakato wa kisheria” na ilisababisha vifo vya maelfu ya watu, wakiwemo watoto.

Akijitetea dhidi ya ripoti za uwezekano wa kukamatwa kwake, Duterte hapo awali alisema kuwa alifanya “kila kitu…kwa ajili ya watu wa Ufilipino”.
 
Duterte wakati wa utawala wake alishindwa kula na kipofu. Aliendesha operations zake huku akiwadindia mataifa makubwa ikiwemo US so kwa sasa hana mtetezi. Mtu kqma Netanyau haguswi kwa sababu mataifa yanajua ukimkamata umenunua ugomvi na US. Kibaya zaidi kakamatwa na utawala wa nchi yake
 
Kwamba alipambana na biashara ya dawa za kulevya halafu tena anatakiwa na mahakama ya ICC? Sijaelewa, kwa maneno mengine, ICC inaona ni sahihi kua na magenge ya wafanya biashara wa dawa za kulenya?
Angefuata sheria. Duterte alikuwa anaua hovyo mno.
 
Kwamba alipambana na biashara ya dawa za kulevya halafu tena anatakiwa na mahakama ya ICC? Sijaelewa, kwa maneno mengine, ICC inaona ni sahihi kua na magenge ya wafanya biashara wa dawa za kulenya?
Alipambana kwa njia amabzo si za hakikabisa kwa kibinadanu

yaan yeye akiambiwa mtu fulani anauza madawa shaba tu
alienda mbali alikuwa anawaua hadi mateja wenye alosto kali ambao walihitaji REHAB but yeye aliwapiga shaba tena anawapiga shaba hadhalani mbele ya wazazi wao
 
Duterte mjinga sana. Alikuwa anasema wazi kwamba anataka kuua watu. Kaacha ushahidi kibao.
Duterte angeomba ushauri wa polisi wetu ambao mtu akifa utasikia "mtuhumiwa alikuwa akikataa kutii amri halali ya polisi hali iliyofanya polisi kutumia risasi ya moto na kumlenga mguuni ila kwa bahati mbaya mtuhumiwa alifia njiani akikimbizwa hospitali"..... au "Mtuhumiwa alijirusha kutoka kwenye gari lililokuwa kasi"...
 
Back
Top Bottom