Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema anaamini kuwa mwenzake wa Urusi anatafuta njia ya kukomesha vita alivyoanzisha Ukraine, na kwamba "hatua muhimu" itachukuliwa.
Alisema mtazamo wake kutokana na mazungumzo ya hivi majuzi na Vladimir Putin ni kwamba alitaka "kumaliza mzozo huu haraka iwezekanavyo".
Ukraine imekomboa tena sehemu kubwa ya eneo lake mwezi huu.
Kiongozi wa Uturuki alionyesha kuwa mambo yalikuwa "magumu" kwa Urusi.
Bw Erdogan alizungumza kuhusu kuwa na "majadiliano ya kina" na Bw Putin katika mkutano wa kilele nchini Uzbekistan wiki iliyopita.
Katika mahojiano na shirika la utangazaji la Marekani PBS, kiongozi huyo wa Uturuki alisema alipata hisia kwamba rais wa Urusi anataka kumalizika kwa haraka kwa vita.
"Kwa kweli ananionyesha kwamba yuko tayari kukomesha hili haraka iwezekanavyo," Bw Erdogan alisema.
"Hayo yalikuwa maoni yangu, kwa sababu jinsi mambo yanavyoenda hivi sasa ni shida sana.
"Pia alisema "mateka" 200 hivi karibuni watabadilishwa kati ya pande hizo mbili.
Hakutoa maelezo zaidi ya nani atajumuishwa katika ubadilishaji huo wa wafungwa.