Rais hapaswi kufanya kazi za kawaida za Rais akiwa nje ya nchi


Sawa mkuu. Naheshimu maoni yako.

Heights and levels.
 
Kama uteuzi huo umeanza tarehe 29 Oktoba 2021 na Rais Samia ameondoka nchini kwenda Scotland tarehe 30 Oktoba 2021 na kuwasili tarehe 31 Oktoba 2021, kwa akili za kawaida Rais Samia alifanya uteuzi huo akiwa wapi mkuu?
Usihoji sana akili zetu, maana zingine kama mahindi ya popcorn kwenye moto.
 
Kama uteuzi huo umeanza tarehe 29 Oktoba 2021 na Rais Samia ameondoka nchini kwenda Scotland tarehe 30 Oktoba 2021 na kuwasili tarehe 31 Oktoba 2021, kwa akili za kawaida Rais Samia alifanya uteuzi huo akiwa wapi mkuu?

Mkuu, press release ya uteuzi inaonesha Rais amefanya huo uteuzi akiwa Glasgow, Scotland. Huu ni mkoa mpya wa Tanzania labda?

Uteuzi anaofanya Rais unaweza kuwa na immediate effect (unaanza mara moja), retroactive effect (unaanza tarehe ya nyuma) au prospective effect (unaanza tarehe ya baadaye). Kama leo (November 2) Rais anakuteua kuwa msaidizi wake na uteuzi huo unaanza November 5 haina maana kwamba the President traveled into the future to appoint you. Uamuzi huo ameufanya leo!
 
Reactions: Ame

Kikatiba, anakuwa ceremonial. Kazi zote za kila siku za Rais wa JMT wakati huo zinafanywa na Kaimu Rais!
 
Wewe mataga leo hii ndio umejua kuichambua katiba ya nchi?
 
Aliteua mkurugenzi wa TANESCO akiwa New York tena ile siku alikua anahutubia New York.

Chifu Hayaga hapa Tanzania tumepigwa.

Haya mambo ya mabadiliko ya nchi awaachie mabeberu, hiyo sio tatizo kwetu kabisa

Ama ndio condoo anawapeleka kondoo wenzake kunyonyesha, bendera fuata upepo na sisi tuonekane tumo.
 
Una shida ya uelewa wa kutojua kutofautisha baina ya uteuzi na tarehe ya kutangazwa uteuzi.
 
Kuna mahala nilisoma article ya jamaa anaitwa Joseph Magata akisema Rais Samia hakuhitaji kiapo cha urais.

Kwa maana take Philip Mpango sasa hivi anafanya kazi zote za urais na hajaapa kiapo cha urais.

Mamaka hiyo ilitoka kwenye RAIA MWEMA


 
Una shida ya uelewa wa kutojua kutofautisha baina ya uteuzi na tarehe ya kutangazwa uteuzi.

Wewe ndiyo una shida!

Kila executive action inatambulishwa na vitu viwili vikubwa: Time and place. Ndiyo maana press releases zote huonesha hivi vitu viwili.
 
Aiseeeee !!! bila shaka uteuzi uliofanyika ni batili
 
Kuna makala moja ilitembea sana mitandaoni mwezi Julai mwaka juu ichambua mambo haya.

Makala yenyewe hii hapa



Kkkk
anda
Na hapo ndio umemaliza kujadiliana na "uliyemtuhumu kuwa na uelewa mdogo" ?

Yaani hivyohivyo tu basi ?

Mmmh....
Haya boss, uwe na wakati mwema.
 
Unajichanganya au hauupendi ukweli.Kukasimisha.Unaipenda keki uendelee kuiangalia huku unataka kuila?
 
Kulingana na katiba uko right kabisa; rais akiwa nje anakuwa anafanya mambo ya nje tu, yale ya ndani yanafanywa na Makamu wa rais. Wakati wa Nyerere, kifungu hicho cha katiba kilitumiwa na Jumbe kuwaweka watu kizuizini akitumia power za urais wakati Nyerere akiwa nje ya nchi.

Tanzania ya siku hizi ni kanyaga twende tu, katiba na sheria ni kitu kimoja, na powers ppamoja na ulaji ni kitu kingine.
 
😍
 
Lakini hiyo kwa Afrika haiwezekani
 
Mabadiliko ya tabia ya nchi ni tatizo la wote, ni suala mtambuka. Ni changamoto isiyozingatia mipaka mkuu.

Tena athari zake ni kubwa zaidi kwa sisi tusiojiweza kuliko wale wenzetu.
Sio tatizo kabisa kama una pesa na nguvu duniani. Mkataba unaowekewa mkazo ni ule wa France sijui wa 2005, ule wa KYOTO wa 2001 ulikwamia wapi?
 
Maana yako umejipotosha, Makamu wa Rais kufanya majukumu ya Rais hakuna maana ameshakuwa Rais, kuwa Rais ni mpaka aapishwe ili kukamata nafasi hiyo.

Kwasasa Tanzania ina Rais mmoja tu, SSH wether awe nje ya nchi au ndani, tofauti ndogo ni pale akiwa nje from 24hrs haruhusiwi kisheria kutimiza majukumu yake kama Rais japo hili halimuondolei sifa ya kuwa Rais kisheria.
 
Soma vizuri Katiba. Kaimu Rais (au Kaimu yeyote yule) hawezi KUTENDA kitu kipya, hawezi kuteua hawezi kufukuza. Labda hiyo katiba mpya yenu iseme hivyo, Rais Tundu Lissu akiwa Belgium Kaimu Rais wake Peter Msifwa amteue Professor Assad awe Mkurugenz i wa NDC?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…