Tanzania ni taifa la kistaarabu sana - hata kipindi cha kudai Uhuru ustaarabu ndio uliotawala badala ya matumizi ya nguvu.
Sasa baada ya kuingia kwa vyama vingi vya siasa, na baada ya kupata maendeleo ya ktk sekta za mawasiliano hususan matumizi ya simu za mikononi - umejengeka utamaduni mbaya wa kutukana, kudhihaki, kunanga, au kubeza jitahada za viongozi wa juu wa Serikali.
* Cdm jiulizeni hivi ikitokea TAL akawa Rais mtapenda atukanwe? JE, mtakubali?
* ACT Wazalendo - hivi ikitokea mkapata Rais kesho mtapenda atukanwe au kudhihakiwa? JE, mtakubali?
* CUF - hivi ikitokea IHL akawa Rais kupitia chama chenu mtakubali atukanwe au kukejeliwa? JE, mtakubali?
* Kwa vyama ambavyo sijavigusa - ikitokea mkapata Rais kupitia vyama hivyo mtakubali atukanwe au kukosolewa bila staha? JE, mtakubali?
Vivyo hivyo kwa wanaccm na wapenda amani nchini hatupendi kuona Rais akidhihakiwa, kutukanwa au kukosolewa bila staha. Tujitahidi kufikisha kero zetu kwa viongozi very diplomatically ataelewa, tujitahidi kutumia simu zetu kwmtizamo usioumiza mwingine ataelewa.
Hatuna nchi nyingine - hii ndiyo nchi tuliyozawadiwa na Mungu. Lkn pia kwa wasaidizi wa Rais jitahidini kutambua kero za kijamii na kuzitafutia suluhu haraka au kuzifikisha kwa Rais mapema kabla hazijaleta taharuki.
Kukawia kupata majawabu ya kero za kijamii ni kumchonganisha Rais na wananchi wake. Changamkeni.l
Msakila Kabende Msakila
Kigoma.