Rais Hussein Mwinyi ataiunganisha Zanzibar na Bara

Amezaliwa ndani ya muungano, ameishi Zanzibar na Bara, alikuwa mbunge Bara na Zanzibar, na amekuwa Waziri wa Wizara ya Muungano. Ni mtu sahihi sana kuinganisha vema Unguja na Pemba kisha Zanzibar na Bara.

Ni kijana mwenye weledi, utu na muono wa mbali sana.

Kama atashindwa yeye kuwaunganisha wazanzibar na kuiunganisha Zanzibar na Bara, basi muungano utakuwa na safari ndefu sana kutengemaa.

Na anaendelea kuwauwa na kuwafunga wazanzibari

Aendeleze uvamizi tu na majeshi yake ya Tanganyika na yale ya kukodi kutoka Burundi
 
Ataiunganisha zanzibar? Kwa mabavu na blackmailing.
Free Mazrui chaguo la watu.
 
Tiba ya kudumu ya muungano ni serikali moja, na sii hizi 2 ama 3 za Warioba

Ila Hussein Mwinyi ni hatua kubwa ya kulinda muungano wetu, kuiunganisha na kuibadilisha Zanzibar
Thank you. Tutaokoa gharama kubwa sana pia
 
Tiba ya kudumu ya muungano ni serikali moja, na sii hizi 2 ama 3 za Warioba

Ila Hussein Mwinyi ni hatua kubwa ya kulinda muungano wetu, kuiunganisha na kuibadilisha Zanzibar
Mtaendelea kuota ZANZIBAR hamtoipata kamwee machogoo
 
Sawa, lakini Maalim Seif pia angeturudisha nyuma sana kama angefanywa ashinde. Dunia yote ya wakubwa inaungana sembuse sisi.
Mbona mnagwaya Muuungano wa kisiasa Afrika ya Mashariki kwa kuwaogopa wakenya Maji na mchanga haviwez changanyika ni swali la muda tuu
 
Kwanza apambane na yakhe culture, umwinyi, ukwepaji kodi na uvivu wa wazanzibar
Wazanzibar pamoja na uvivu wao wakifika pale nyinyi machogo hamkufika wivu choyo husda na roho mbaya zenu ndio vilivyotufanya wazanzibar kuwa hivi tulivyo
 
Hata ulaya na marekani walikufa wengi sana hadi kufika pale zilipo Leo. Wanaendelea kufa wengi sana ili kuzibakiza hivi zilivyo Leo.
Hivyo Muungano unadumishwa kwa kumwagwa damu za wazanzibar mbwe wewe???
 
Tiba ya kudumu ya muungano ni serikali moja, na sii hizi 2 ama 3 za Warioba

Ila Hussein Mwinyi ni hatua kubwa ya kulinda muungano wetu, kuiunganisha na kuibadilisha Zanzibar
Hewaa, na hiyo ndio sababu kuu ya kufutwa kwa serikali ya Tanganyika. Iliyokuwa inafuatia kufutwa ni serikali ya Zanzibar ili ibaki Tanzania. Wako watu (maaluni) ambao wanauchelewesha mpango huu.
 
Marekani kuna uchaguzi na matokeo hayajatangazwa ya mshindi hebu tueleze umesikia kwamba kumetokea mauaji,kutekwa,kupigwa, kuuliwa na police kutumia nguvu kwa wananchi na watu kupokonywa fomu kama hapo penu,

Ikiwa huko yalifanyika na nyinyi mnafanya?

View attachment 1621228
Hebu tukumbushe vifo vya akina Lumumba, Samora, Ngwabi, Saadam, Gadaffi, Nkrumah, Rabin, wapalestina.

Lazima tukubadiliane kuwa kila taifa linao vibaraka waliopandikizwa na wakubwa kwa maslahi yao. Ni jukumu letu kuwabaini na kuamua tuwafanye nini tukishawabaini.
 
Hivyo Muungano unadumishwa kwa kumwagwa damu za wazanzibar mbwe wewe???
Miungano yote duniani ina misukosuko mingi sana hasa kama ukitaka kujitoa kwenye muungano huo. Uingereza inapata tabu kujitoa EU, Ireland inapata taabu sana kijitoa Uingereza, Katalunha (Barcelona) inapata taabu sana kujitoa Hispania na hata jimbo la marekani likitangaza kujitenga litapata taabu sana.

Kwanini unaona ni rahisi tuu kwa Zanzibar kujitenga kutoka tanzania? Huu ni ujinga kufikiria hivyo. Wanzanzibar ni wanufaika wakubwa wa muungano huu pengine kuliko hata watanganyika
 
Mleta mada bado sijakuelewa kabisa.
Tumekuwa na muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu 1964, sasa Hussein Mwinyi anakuja kuunganisha nini?

Mahusiano ya kijamii na kitamaduni kati ya Zanzibar na Tanganyika yamekuwepo karne nyingi kabla ya uhuru na hata kabla ya ukoloni, hivyo sio mtu mwenye uwezo wa kuwaunganisha au kuwagawanya wazanzibar na watanganyika.

Yote kwa yote, Hussein Mwinyi sio chaguo la wazanzibar (CCM Zanzibar ilimkataa, wazanzibar wengine hatukumtaka), amewekwa pale kinguvu kwa maslahi ya watanganyika.

Na siku akijaribu tu kuhoji maslahi ya wazanzibar ndani ya muungano huenda ndio utakuwa mwisho wa urais wake, alifanya hivyo Rais Jumbe, kilichompata kilikuwa ni kupoteza urais wake na kuwekwa 'kizuizini' kule Kigamboni kwa zaidi ya miaka 20, na mauti yakamfikia huko huko Tanganyika.

Tanganyika inaifanya Zanzibar ni koloni lake chini ya mwamvuli wa muungano, lakini ipo siku ukoloni huo utafikia kikomo.
 
Nyinyi mna vichekesho vya peke yenu wadanganyika

Kama wazanzibar ndio wanufaika Sasa Kuna dhambi gani wakiwa wenyewe hawayataki hayo manufaa

Yaani mnamwaga damu za watu kwa vile tuu hawataki manufaa mnayowapa? Acheni ulaghai huo

Kisha wacha kuseme uongo Muengereza alipoona Muungano wa Ulaya hauna manufaa nao mbona aliondoka mambo yakaisha? Au waweza niambia waengereza wangapi damu yao ilimwagwa wakati wanajitoa Jumuia ya Ulaya

Mwisho nikwambie Chakubanga wacha kukariri Muungano ni wakigumashi ni kosa kuuita Muungano huu ni Ukoloni wa Mtu mweus dhidi ya Dola huru la ZANZIBAR
Na

UNA MWISHO WAKE
 
Amezaliwa ndani ya muungano, ameishi Zanzibar na Bara, alikuwa mbunge Bara na Zanzibar, na amekuwa Waziri wa Wizara ya Muungano. Ni mtu sahihi sana kuinganisha vema Unguja na Pemba kisha Zanzibar na Bara.

Ni kijana mwenye weledi, utu na muono wa mbali sana.

Kama atashindwa yeye kuwaunganisha wazanzibar na kuiunganisha Zanzibar na Bara, basi muungano utakuwa na safari ndefu sana kutengemaa.
Zanzibar mumeshaivunja sasa mnataka iunganishwe ili iweje wakat hayo mmeyafanya wemyewe kuwa hivyo ilivyo sasa.
 
Miungano yote duniani ina misukosuko mingi sana hasa kama ukitaka kujitoa kwenye muungano huo. Uingereza inapata tabu kujitoa EU, Ireland inapata taabu sana kijitoa Uingereza, Katalunha (Barcelona) inapata taabu sana kujitoa Hispania na hata jimbo la marekani likitangaza kujitenga litapata taabu sana.

Kwanini unaona ni rahisi tuu kwa Zanzibar kujitenga kutoka tanzania? Huu ni ujinga kufikiria hivyo. Wanzanzibar ni wanufaika wakubwa wa muungano huu pengine kuliko hata watanganyika
Wacha kukariri ZUMBUKUKU mumwage damu za wazanzibar ili iwe kafara ya UKOLONI wenu?? Utautaje Mungano wakat hakuna sehemu wazanzibar walikubali kubwa ooooo nyinyi ndio mnanufaiks ni hivi BORA WAZANZIBAR WALE MCHANGA LKN WAWE HURU KULIKO KULA KEKI KTK UTIMWA WENU
 
Amezaliwa ndani ya muungano, ameishi Zanzibar na Bara, alikuwa mbunge Bara na Zanzibar, na amekuwa Waziri wa Wizara ya Muungano. Ni mtu sahihi sana kuinganisha vema Unguja na Pemba kisha Zanzibar na Bara.

Ni kijana mwenye weledi, utu na muono wa mbali sana.

Kama atashindwa yeye kuwaunganisha wazanzibar na kuiunganisha Zanzibar na Bara, basi muungano utakuwa na safari ndefu sana kutengemaa.

Mleta mada bado sijakuelewa kabisa.
Tumekuwa na muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu 1964, sasa Hussein Mwinyi anakuja kuunganisha nini?

Mahusiano ya kijamii na kitamaduni kati ya Zanzibar na Tanganyika yamekuwepo karne nyingi kabla ya uhuru na hata kabla ya ukoloni, hivyo sio mtu mwenye uwezo wa kuwaunganisha au kuwagawanya wazanzibar na watanganyika.

Yote kwa yote, Hussein Mwinyi sio chaguo la wazanzibar (CCM Zanzibar ilimkataa, wazanzibar wengine hatukumtaka), amewekwa pale kinguvu kwa maslahi ya watanganyika.

Na siku akijaribu tu kuhoji maslahi ya wazanzibar ndani ya muungano huenda ndio utakuwa mwisho wa urais wake, alifanya hivyo Rais Jumbe, kilichompata kilikuwa ni kupoteza urais wake na kuwekwa 'kizuizini' kule Kigamboni kwa zaidi ya miaka 20, na mauti yakamfikia huko huko Tanganyika.

Tanganyika inaifanya Zanzibar ni koloni lake chini ya mwamvuli wa muungano, lakini ipo siku ukoloni huo utafikia kikomo.
Ukisema hivyo unakosea. Kwenye kampeni za Hussein kulikuwa na watu wanaohudhuria waliovaa kijani, siku anaapisha ni kijani tupu ilivaliwa. Je, hawa walikuwa akina nani kama halikuwa chaguo lao?

Muungano ni kama jina la mtu, kama wazazi wako walikosea wakakuita jina la Fisi basi utaitwa fisi ukubwani na pengine kwenye maisha yako. Kama waliounganisha Zanzibar na Tanganyika walikosea basi walikosea kwa niaba yetu. Hata wamerekani wanalalamikia muungano wa majimbo na kura za wajumbe, electral college katika chaguzi lakini hawana cha kufanya lazima mgombea afikishe kura 270 walizoamua babu zao.
 
Wacha kukariri ZUMBUKUKU mumwage damu za wazanzibar ili iwe kafara ya UKOLONI wenu?? Utautaje Mungano wakat hakuna sehemu wazanzibar walikubali kubwa ooooo nyinyi ndio mnanufaiks ni hivi BORA WAZANZIBAR WALE MCHANGA LKN WAWE HURU KULIKO KULA KEKI KTK UTIMWA WENU
Najuwa kuwa lawama zenu hamzipeleki kwa Mzee Karume aliyekubali aina hii ya muungano bali kwa Hussein Mwinyi anaeyalinda na kuyaenzi mawazo ya muasisi wenu. Kama mzazi wako alikosea kuchagua mchumba (mama au baba yako) mwenye pumu kwa hiyo amekosea kwa niaba yako, huwezi kuzikataa pumu kama zikikupata . Hussein analinda fikra za mwasisi wenu, kwisha.
 
Back
Top Bottom