Rais Hussein Mwinyi ataiunganisha Zanzibar na Bara

Rais Hussein Mwinyi ataiunganisha Zanzibar na Bara

Amezaliwa ndani ya muungano, ameishi Zanzibar na Bara, alikuwa mbunge Bara na Zanzibar, na amekuwa Waziri wa Wizara ya Muungano. Ni mtu sahihi sana kuinganisha vema Unguja na Pemba kisha Zanzibar na Bara.

Ni kijana mwenye weledi, utu na muono wa mbali sana.

Kama atashindwa yeye kuwaunganisha wazanzibar na kuiunganisha Zanzibar na Bara, basi muungano utakuwa na safari ndefu sana kutengemaa.
Labda aunganishe Mkuranga na Mikocheni B
 
Wapuuzi Kama nyie nawagonga block
Toa hoja sio matusi.

Unatakiwa ufanye utafiti wa kwanini Mzee Karume alikubali muungano wa aina hii, na kwanini wazanzibar wa wakati huo hawakupinga. Lazima tukubali kuwa hata wazee wenu walikuwa na hoja zilizowafanya wakubali muungano wa hivi. Hata mipaka ya vitongoji, mitaa, vijiji, kata, tarafa, wilaya, mikoa, nchi na mabara hatuwezi kuwalaumu babu zetu hata kama leo tunaipenda au hatuipendi.

Kama mzazi wako alikupa jina usilolipenda alikosea kwa niaba yako. Mimi hapa mzazi aliniita Kavulata ingawa mimi sipendi kuitwa jina hilo lakini nitafaje.

Kama kuna hoja ya msingi iwekwe mezani kuliko kutumia nguvu nyingi. Hakuna serikali makini itakayoruhusu muungano uvunjike kwasababu zisizokuwa za msingi.

Tanganyika haizuii Zanzibar kuwa na viwanda, meli, ndege, kukusanya kodi, kuswali, kuoana, kuimba, kucheza mpira, kuchima mafuta kama yapo wala kula urojo. Hakuna mtu anaeleza ubaya wa muungano zaidi ya kulalamika tu. Wengi wao wanazo chuki za mapinduzi wala sio muungano as such.
 
Mbona mnagwaya Muuungano wa kisiasa Afrika ya Mashariki kwa kuwaogopa wakenya Maji na mchanga haviwez changanyika ni swali la muda tuu
Hiyo ndiyo imani walioyonayo wapalestina pia. Siku zitapita nyingi sana.
 
Back
Top Bottom