Zanzibar 2020 Rais Hussein Mwinyi: Niko tayari kufanya maridhiano na vyama vingine

Zanzibar 2020 Rais Hussein Mwinyi: Niko tayari kufanya maridhiano na vyama vingine

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
HABARI: Ninaheshimu maridhiano na matakwa ya Katiba ya kushirikiana na vyama vingine vya siasa katika kuendesha Serikali. Niko tayari kuyatekeleza maridhano kama Katiba ya Zanizbar inavyoeleza - Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar #MwanaHALISIDigital.
=====================

KUMBUKUMBU.

Baada ya uchaguzi wa Zanzibar wa 2015 kufutwa Marekani kupitia shirika lake la misaada la Millennium Challenge Corporation (MCC) ilizuia pesa za mradi wa kupeleka umeme Zanzibar kiasi cha $472m karibu Tshs. Trn. 1. nafikiri hili somo kaliona Rais Mwinyi ndio maana anataka maridhiano.

 
Kwanza aanze kuwatoa akina Mazrui na wenzake, awafidie wale wote waliopoteza maisha yao wakati wa Uchaguzi.

Asisahau kuwafikisha Mahakamani wale wote waliotoa roho za Watu waliokuwa hawana hatia wakati wa Uchaguzi

Kama itawezekana uchaguzi urudiwe.

Free Mazrui and all Political prisoners
 
Sikubaliani na serikali ya mseto moja kwa moja. Kwanza lazima iwepo kamati ya maridhiano kwa kuwatafut a wale wote waliohusika na mauaji au vitendo vya kikatili wachukuliwe hatua. Haiwezekani kuna familia ziameachwa yatima ukimbilie serikali ya mseto.

Tujifunze kupitia South Africa walipo unda kamati ya mariadhiano # Truth and reconciliation committee chini ya Desmond Tutu
 
Sikubaliani na serikali ya mseto moja kwa moja .Kwanza lazima iwepo kamati ya maridhiano kwa kuwatafut a wale wote waliohusika na mauaji au vitendo vya kikatili wachukuliwe hatua .Haiwezekani kuna familia ziameachwa yatima ukimbilie serikali ya mseto.Tujifunze kupitia South Africa walipo unda kamati ya mariadhiano # Truth and reconciliation committee chini ya Desmond Tutu
Hakuna cha uchunguzi wala nini

Nani aliwaambia waandamane na kufanya vurugu

Ebo!, uvunje sherie mwenyewe, janga likupate, halafu lawama ziwaendee wengine

Wangelitii sheria na mamlaka yasingeliwakuta ova.
 
Hakuna cha uchunguzi wala nini

Nani aliwaambia waandamane na kufanya vurugu

Ebo!, uvunje sherie mwenyewe, janga likupate, halafu lawa ziwaendee wengine

Wangelitii sheria na mamlaka yasingeliwakuta ova.
Si ameshinda? sasa aendeshe nchi sio kushinda kwenye mitwitter akisema yupo tayari kwa maridhiano . hahahaaa Lissu atawakung'uta spana za mbali mpaka mnyooke
 
Warudie uchaguzi wote Zanzibar, na waache demokrasia itendeke hapo ndio kutakuwa na maridhiano.

Yani uingie Ikulu kwa wizi halafu utuambie maridhiano, huu ujinga wa mwaka.

Jiuzulu, tufanye uchaguzi halali!

Sasa anategemea kumpata nani?!
 
HABARI: Ninaheshimu maridhiano na matakwa ya Katiba ya kushirikiana na vyama vingine vya siasa katika kuendesha Serikali. Niko tayari kuyatekeleza maridhano kama Katiba ya Zanizbar inavyoeleza - Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar #MwanaHALISIDigital.


Kafufue uliowaua kwanza ndio uunde nao Serikali ya maridhiano
 
Aongoze tu kama babu ali makelele ya nini, Maalim achana nao hao, msimamo ni uleule madai ya uchaguzi mpya wakitaka sawa wasipotaka sawa, hatuna shida ya uongozi kama ni shida hio walikuwa nayo wao, sasa wameshapata uongozi yanini kuangalia upande wa pili, CCM mnalo hilo ni lenu.

Msitafute njia ya kutokea maana ACT wakikubali basi hata dunia itawashangaa na haitawaelewa.
 
Hakuna cha uchunguzi wala nini

Nani aliwaambia waandamane na kufanya vurugu

Ebo!, uvunje sherie mwenyewe, janga likupate, halafu lawama ziwaendee wengine

Wangelitii sheria na mamlaka yasingeliwakuta ova.
Kama ni hivyo anataka maridhiano ya nini na nani kamuomba kuridhiana.
 
Endelea kuota
Yeye na wewe mnaosema mnataka Maridhiano ndio muendelee kuota

Kuiba muibe nyinyi,kudhulumu mdhulumu nyinyi, Sasa mnataka kulaghai watu,nafsi zinawasuta

Kaeni kimya Tu,kwa Wazanzibari Yao yamewaishia,wamemuachilia Mungu

Free Mazrui and all Political prisoners
 
Kwanza aanze kuwatoa akina Mazrui na wenzake awafidie wale wote waliopoteza maisha yao wakati wa Uchaguzi..

Kama itawezekana uchaguzi urudiwe..

Free Mazrui and all Political prisoners

Bottom line:

1. Uchaguzi urudiwe.
2. Fidia kwa wahanga.
3. Kuwajibishwa kwa perpetrators.

Bila hayo na kinuke tu!
 
Back
Top Bottom