Rais huwa hatangazi Utalii

Rais huwa hatangazi Utalii

Hivi director wa hizo movies za Royal Tour ni nani?

Halafu zitakuwa katika mtindo gani?

Single movies, zile za part 1,2&3.. documentary au series?
 
Siyo gumu, mi nafikiri Mama kachukua uamuzi sahihi anavyoona yeye ni sahihi, tumuunge mkono!
Nitamuunga mkono akipanda mlima Kilimanjaro. Aka shoot pale Uhuru peak. Awe rais wa kwanza duniani kufika pale juu.
 
Kikubwa ni Nyota ngoja tuangalie kama itang'aa au laa ndio tunamwomba nyanda wa star tv amulize yale maswali kwenye kipindi chake kile au vp baabu?
 
Kwa sababu ni Mama
Nahisi italeta flavour nzuri na itapendwa

imagine ingekua Jiwe
 
Nitamuunga mkono akipanda mlima Kilimanjaro. Aka shoot pale Uhuru peak. Awe rais wa kwanza duniani kufika pale juu.
asije akathubutu, na akijaribu sisi kama taifa tutapata msiba kwa mara ya pili katika kipindi cha mwaka mmoja...
 
Kwa mara ya kwanza Dunia inaenda kushuhudia mkuu wa nchi, Rais akitangaza utalii.
Rais anapoamua kutangaza utalii maana yake ni kwamba hilo Taifa analoongoza,ni Taifa mfu,ni Taifa lililokufa,ni taifa jipya kabisa chini ya jua,na halina raslimali zozote na wala kitu chochote,sasa inabidi atoke mkuu wa nchi aifahamishe Dunia kuwa taifa analoongoza lina sehemu za utalii.
Na Kwanza hata Kama taifa halina chochote, siyo kazi ya Rais kutangaza utalii.
Zipo strategies za kutangaza utalii, Samatta ni maarufu Duniani kuliko Rais Samia.
Rais anapoenda Location kama msanii wa Bongo movie kutangaza utalii,huo mkosi mzito mno kwa taifa,watalii hawaji Tanzania eti kwa sababu Rais aliwatangazia.
Wanakuja kwa sababu usalama wao utakuwa mkubwa zaidi, huwezi kwenda kutalii kwenye Taifa ambalo kiongozi mkuu wa Chama kikubwa Cha Upinzani ni Gaidi, maana yake ni kwamba hata mawaziri nao ni magaidi.
Kenya inapokea maelfu ya watalii kwa mwaka kuliko Tanza,ni nani alimwona Rais wa Kenya akienda location kutangaza utalii?
Yaani Serikali nzima yenye wasomi wa kada zote haina strategies za kutangaza utalii hadi Rais aende location?
Mbona ni rahisi mno kutangaza utalii kuliko ilivyo rahisi kunywa maji?
Tanzania hii yenye vivutio vyote leo hata Rwanda wameanza kuwazidi kupokea watalii wengi kwa sababu ya strategies.
Rais ataenda Location zote,na mtatengeneza filamu zote na watalii hamtawaona kwa sababu hamna strategies.
Nyie strategies zenu ni kuua Upinzani tu haya mengine zero kabisa.
Hii Nchi watu wa nje wanaiogopa . Imejaa mi corona alafu serikali

inawabembbeleza wale wapuuzi anti vaccines,
 
Tatizo mmejaa ushamba wa Chato! Kwani Samia ndo Rais wa kwanza Duniani kufanya Royal Tour?

Tatizo mmejaa ushamba na mnaonesha wazi wazi mlivyo washamba
.mkuu siku za nyumba nilikuwa nakuheshimu siku hizi nakutumia mashaka uwezo wako wa kujenga hoja,

Umejiuluza Je? ikitokea hii loyola tour haikutoa matokeo chanya au haikufanikiwa,hudhani Raisi atakuwa kwenye wakati mgumu?

Je ikitokea kuna ubadhitifu kwenye hii kitu wabaya wake si watamblack mail na kupeleka kujiuzulu kabla muda
 
Kama hakuna nchi rais anatangaza utalii basi acha tanzania iwe mfano.usipende kuwa negative sana
 
Kwa mara ya kwanza Dunia inaenda kushuhudia mkuu wa nchi, Rais akitangaza utalii.
Rais anapoamua kutangaza utalii maana yake ni kwamba hilo Taifa analoongoza,ni Taifa mfu,ni Taifa lililokufa,ni taifa jipya kabisa chini ya jua,na halina raslimali zozote na wala kitu chochote,sasa inabidi atoke mkuu wa nchi aifahamishe Dunia kuwa taifa analoongoza lina sehemu za utalii.
Na Kwanza hata Kama taifa halina chochote, siyo kazi ya Rais kutangaza utalii.
Zipo strategies za kutangaza utalii, Samatta ni maarufu Duniani kuliko Rais Samia.
Rais anapoenda Location kama msanii wa Bongo movie kutangaza utalii,huo mkosi mzito mno kwa taifa,watalii hawaji Tanzania eti kwa sababu Rais aliwatangazia.
Wanakuja kwa sababu usalama wao utakuwa mkubwa zaidi, huwezi kwenda kutalii kwenye Taifa ambalo kiongozi mkuu wa Chama kikubwa Cha Upinzani ni Gaidi, maana yake ni kwamba hata mawaziri nao ni magaidi.
Kenya inapokea maelfu ya watalii kwa mwaka kuliko Tanza,ni nani alimwona Rais wa Kenya akienda location kutangaza utalii?
Yaani Serikali nzima yenye wasomi wa kada zote haina strategies za kutangaza utalii hadi Rais aende location?
Mbona ni rahisi mno kutangaza utalii kuliko ilivyo rahisi kunywa maji?
Tanzania hii yenye vivutio vyote leo hata Rwanda wameanza kuwazidi kupokea watalii wengi kwa sababu ya strategies.
Rais ataenda Location zote,na mtatengeneza filamu zote na watalii hamtawaona kwa sababu hamna strategies.
Nyie strategies zenu ni kuua Upinzani tu haya mengine zero kabisa.
Acha upumbavu wewe ,Rais Kagame amewahi shiriki kwenye Royal tour ya kuitangaza utalii wa Nchi yake na pia Netanyahu wa Israel amewahi shiriki promotion ya utalii kwenye nchi yake.

Samantha anaweza kuwa anafahamika zaidi lakini asiwe na ushawishi wowote wa maana.

Piga Kazi mama, unadhani wewe mtoa mada na Rais nani anaweza kuwa invited kwenye Royal tour? Hii inahusu watu wenye ushawishi sio kila kima.
 
Askofu Gwajima alitabiri luwa wakishachanjwa kuna uwezekano wengine watageuka kuwa mazombi. Ebu tuzidi kuvuta subira.
Na yale mazombi aliyofufua Gwajima yako wapi?
Tumechoka kuyasubiri, au wewe mmoja wapo?
 
Mimi sioni kama kuna tatizo kama ufanisi utakuwepo.Raisi akifanya hivi sifikirii kuwa inafunga milango kwa njia/namna nyingine pia kutumika.Ni suala la kuanza,kujifunza na kisha kuboresha au kuchagua njia ipi sahihi.
2.Kwanini kila kitu tunapenda kusema akina fulani hawafanyi hivi,angalia akina fulani.Sikatai kuiga au kujifunza jambo lenye tija kwaajili ya maendeleo ni kitu cha msingi lakini haimaanishi kwamba ndio njia pekee.
Watanzania kwenye vitu vingi tukikosoa tunapenda kulinganisha na sehemu nyingine,kwanini tusijifunze pia kutoa maoni ambayo yatakua rahisi kwa mazingira yetu na wengine wakajifunza kwetu? Ni kweli hatuwezi kuanzisha mambo yakafanikiwa mpaka kuiga kila kitu kwa wengine?
3.Haya mambo pia naamini yapo chini ya wizara ambayo pia naamini imekuwepo miaka mingi na inaongozwa na watanzania wengi tu,ambao naamini kwa nafasi yao tangu wizara imeanzishwa wangeweza kufanya kitu zaidi.Badala yake mfumo wetu tumeujenga kwa kila kitu kuwanyooshea vidole maraisi.SILAUMU ILA NAFIKIRI PIA KAMA WATANZANIA KWA UJUMLA TUNATAKIWA KUBADILIKA,TUKIPEWA NAFASI TUZITUMIE IPASAVYO.RAISI NI MWANADAMU,KUNA MUDA ANAWEZA KUWA SAHIHI,KUNA MUDA ANAWEZA ZINGUA!
 
Siyo gumu, mi nafikiri Mama kachukua uamuzi sahihi anavyoona yeye ni sahihi, tumuunge mkono!
Tutamuungaje mkono wakati watu maarufu wako mahabusu, hawezi fanikiwa kama hatendi haki, kama mtangulizi wake alivyo fail mpaka akafa
 
Tumechelewa sana kujitangaza kwa Dunia na kutumia fursa ya utalii Kwa kuingiza mapato makubwa.

Kwa Taarifa yako Tanzania ina vivutio vingi kuliko Misri, Morocco na South Africa ila inapokea watalii wachache sana kwa mwaka compared na hizo nchi.

Stratergy alioanzisha Rais Samia ndo njia tuliyopaswa kuifanya tangu miaka ya huko nyuma. Kwa iyo Rais Samia yuko sawa
Wewe ndio umechelewa kujua
1381032073_img_3359.jpg
 
Back
Top Bottom