Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Mhe. Edward Lowasa alipokuwa Waziri Mkuu alikuwa msimamizi wa TAMISEMI na alitumia vyema nafasi hiyo kujijenga kisiasa na kuwa na network Kila Kona. Mzee Pinda na Mawaziri wengine wakuu waliowahi kuhudumu nchini awakufanya kama Mzee Lowasa. Lowassa alifanya vile Kwa sababu alikuwa amejipanga kuchukua nchi na Kwa mwanasiasa yoyote makini asingeacha kujipanga.
JPM alipoingia Madarakani Jambo la kwanza alilofanya nikurejesha TAMISEMI mikononi mwake. Aliondoa majukumu mengi ya Moja Kwa Moja Kwa Waziri Mkuu na yeye kubaki kuwa mtu wa Mwisho kuamua katika Kila jambo. Alifanya vile Kwa sababu Moja kuu, kuondoa makosa aliyofanya JK kwa Lowasa yasijirudie na asiibuke mtu akadhani kuwa Waziri Mkuu ni njia panda ya Urais.
JPM Kwa sera na mfumo wake aliweza kusimamia TAMISEMI na kuweka jicho Kila mahali ikiwemo kuweka maafisa kata na Tarafa wanazungumza moja kwa moja na ofisi yake,waalimu wakawa wanaripoti kwake nk. Kupitia mfumo wake aliweza kuwaita watendaji wadogo kabisa kwenye utumishi wakafika ofisini kwake Ikulu na kuwahutubia. That strategy iliwork out kwake Kwa sababu alikuwa anawaza ndani ya nchi na taarifa zake zilijikita sana ndani ya mipaka kuliko Nje ya mipaka. Hakuwa na calls wala mipango ya mikutano ndani au Nje ya nchi na mataifa mengine aliaamini wageni wengi na wenye uwezo ni mabeberu na wezi wa rasilimali zetu. Kwa namna alivyotumia muda mwingi kupitia majalada na kupokea taarifa akidai halali it was sahihi kwake kuikumbatia TAMISEMI.
Upande wa pili, Mhe. SSH amejipambanua kama mtu ambaye hadhi ya Urais na mpango wake nikutafuta fursa ndani na Nje ya nchi Kwa malengo ya kupata Fedha na mitaji ya kulisaidia Taifa. Muda wake mwingi anautumia kusoma na kujibu hoja pamoja na kutoa maelekezo Kuhusu masuala makubwa ya kitaifa ya ndani na Nje. Ana wageni wengi Kwa sababu mkarimu na anaalikwa kwingi Kwa sababu amekubali kuifungua nchi. Siyo mtu wakukaa akafanya Kila kitu, ni mtu wakukasimu madaraka na majukumu Kwa waliochini yake. Ni mtu anaamini aliowateua na Kila anachoripotiwa anakiamini.
Kwa mfumo wake huu na kwa ukubwa wa TAMISEMI huku ikizingatiwa unyeti wake Kwa usatawi wa nchi ni vigumu kuisimamia kikamilifu wizara za TAMISEMI.
Lakini pia kuiongoza TAMISEMI kunamkwamisha Waziri Mkuu kuisimia kwa sababu waliopo chini ya TAMISEMI wana muda wa kukutana na Mhe. Rais na wanapigiana simu na Mhe. Rais. Ni vigumu Waziri Mkuu kama mwanadamu na mwansiasa kukubali kumkosoa bosi wake au kuwakosoa Mawaziri wanaoripoti Kwa bosi wake. Anaweza akakosoa akaambiwa MWENYE nchi ndiye aliyelekeza.
Naomba kutoa ushauri Kwa Mhe. Rais kuangalia endapo itampendeza akarejesha TAMISEMI Kwa Waziri Mkuu tunaamini hatotumia TAMISEMI Kwa strategies za Mhe. Lowasa. Katibu Mkuu kiongozi chukua mawazo haya yachakate yanaweza kusaidia TAMISEMI ifufuke,inakufa. Wakuu wa idara wamelala Sasa wanajua Hadi Rais awawajibishe na wanamwona alivyobusy.