Rais JK amsaliti mwl Nyerere

Rais JK amsaliti mwl Nyerere

rugumye

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
561
Reaction score
179
Katiba mpya kurudisha nchi ya Tanganyika ni kukijeri mawazo ya waasisi wa Muungano wazee wetu, Hayati Mwl J.K NYERERE na Hayati ABEID AMAN KARUME. Kwa sababu kama kutakuwa na Tanganyika hakuna JinaTanzania kwa sababu Tanganyika ni muunganiko wa maneno kutoka TANGANYIKA NA ZANZIBAR. Naomba kutofautisha mada ya serikali tatu katika katiba mpya na hii ya jina la Tanganyika. Kwaani hatuwezi kuwa na serikali tatu kwa kuendelea kuwa na majina ya nchi ya sasa? Kwa maoni yangu ziwepo serikali 3 yaani 1. Tanzania visiwani 2. Tanzania Bara na 3. Serikali ya Muungano.

Tuangalie madhara ya kubadiri jina la Tanzania.
1. Tutawachanganya wageni hasa watalii kwaani dunia nzima inatambua nchi
ya Tanzania.
2. Utalii unaweza kushuka kwaani jina la Tanganyika ni jipya.
3. Tunaharibu historia ya nchi yetu –Hasara kwa vizazi vijavyo.
4. Itabidi baadhi ya nyaraka zibadirishwe kama vyeti vya elimu na nk
5. Wapinga Muungano watakuwa wameshinda
6. Uongozi wa CCM awamu ya 4 kushindwa kulinda mchango wa waasisi
wa Muungano.
7. Historia itaandikwa kuwa Rais Kikwete ndiye aliyebadiri jina la
nchi ya Tanzania.
8. Rais Kikwete atakuwa msaliti kwa baba wa taifa.
9. Kuongeza gharama kwa walala hoi kuhudumia vingozi wastaafu.
10. Baadae iwapo ZNZ watapata rais mwingine jeshi linaweza kuwa lisiwe la muungano hivyo kuundwa majeshi ya JWT-Jeshi la wananchi Tanganyika, JWZ-jeshi la wananchi Zanzibar, lkn tukumbuke kuwa kwa sasa wanajeshi wa pande zote mbili yapo ndani ya JWTZ. je wale Wazenj waliomo ndani ya JWTZ watafungasha virago kurudi Zenj? vitega uchumi walivyowekeza bara kama majumba na nk itakuwaje? Viongozi kama maalim Seif mwenye uchu wa urais hataki muungano kwaani anajua ndania ya muungano hawezi kuwa rais wa Zenj. je akipata nafasi ya kuwa rais ataamuaje?

Mifano mingine: Marekani waliungana nchi nyingi zaidi lakini jina la USA linatumika mpaka kesho?

Mwisho: Naomba tuongeze kipengele kwenye katiba cha kuzuia kubadiri jina la nchi.
 
hivi aliependekeza serekali 3 ni jk au wananchi?
 
Hujui Historia wenye hekima zao walisema "No research no right to speak"Wewe peek yako huwezi kuwa na akili kuzidi tume na watanzania waliotoa maoni yao. Kumbuka zipo kanuni za maendeleo zinazizingatia wakati, mazingira na changamoto za wakati huo. Enzi za Karume na Nyerere fuatilia mazingira na changamoto zilizowapelekea kuunda muungano wa chapchap.
 
CCM mtahangaika sana, mmeiweka nchi yetu mfukoni kwa miaka mingi, its time for our mother land Tanganyika to be reborn!
 
hebu acheni kwanza twende likizo na hiki kitu kinaitwa muungano halafu tukirudi tutatia akili.
hebu fikiria wengine walikubali kuitwa tanzania bara ila wengine hawakukubali kuitwa tanzania visiwani sasa kuna dhambi gani sisi tusirudi kwenye utanganyika wetu.
malalamiko yamekuwa mengi na kila sehemu inaona ni ya msingi ni bora iwe hivyo.
ni rahisi kwa wazanzibar kujenga nyumba, kupata mashamba na kuajiriwa na kutumia vizuri raslimali za tanganyika lakini si kwa watanganyika walioko zanzibar.
wacha tuuvunje kwa kuwa tumeona busara tununue uhuru wetu kwa fedha na hasa ukichukulia wanaotuhitaji hawatuhitaji kwa sasa.
malalamiko yao ni madogo ukilinganisha na maslahi ambayo wao wanapata katika muungano , lakini ijulikane wazi kuwa hayo yote sio hitaji lao kwa sasa .wanachohitaji ni kujitawala zaidi na kuwa na mamlaka zaidi huenda wanaona wamebanwa. wapeni bana!
historia itakuwepo kwani kunauwezekano siku zijazo tukawa na nchi moja lakini kwa sasa wacha twende likizo.
 
Inavyoonekana ni kwamba hujasoma rasimu ya katiba na wala hukusikuliza hotuba ya mzee Warioba wakati akikabidhi rasimu ya katiba. Yale yaliyowekwa kwenye rasimu ni maoni ya wananchi sio matakwa ya JK wala Warioba. Na hii nchi ni ya wananchi sio ya Nyerere wala Karume. Kama walioamua wakati huo kwa niaba ya wananchi, sasa hivi wananchi wameamua wenyewe kwa faida yao.

Suala la majeshi liko chini ya muungano, hivyo hakutakuwa na kugawa jeshi kati ya jwt na jwz.

Kimataifa nchi itaendelea kuitwa Tanzania kwani mambo ya nje yapo katika muungano.
 
Nakuunga mkono. Ni wakati wa kuamua hatima yetu sisi wenyewe. Nashangaa wanaosema ni kusaliti mawazo ya waasisi! Wana macho na masikio ya kuona na kusikia kinachofanyika Zanzibar? Je Zanzibar aliyoiacha Karume ndo hiyo hiyo?? Watanganyika tukitaka Tanganyika inakuwa kusaliti fikra za waasisi!!!
 
Tatizo mnachanganya mada sijui tatizo nini? nani amesema hataki serikali 3? wapi nimeandika hivyo? nimesema serikali tatu ziwepo lakini tusibadiri jina la Tanzania, nani kasema Tanzania ni jina la wazanzibar? tubadiri mfumo siyo jina.
 
Inavyoonekana ni kwamba hujasoma rasimu ya katiba na wala hukusikuliza hotuba ya mzee Warioba wakati akikabidhi rasimu ya katiba. Yale yaliyowekwa kwenye rasimu ni maoni ya wananchi sio matakwa ya JK wala Warioba. Na hii nchi ni ya wananchi sio ya Nyerere wala Karume. Kama walioamua wakati huo kwa niaba ya wananchi, sasa hivi wananchi wameamua wenyewe kwa faida yao.

Suala la majeshi liko chini ya muungano, hivyo hakutakuwa na kugawa jeshi kati ya jwt na jwz.

Kimataifa nchi itaendelea kuitwa Tanzania kwani mambo ya nje yapo katika muungano.

Maoni ya watanzania wangapi? hiyo tume imefikia wananchi wangapi? unajua taratibu za kufanya research? walifanya sampling popoulation gani? kwa kutumia njia gani? siyo unaitisha watu 100 katika ya 100,000 unahoji 20 harafu unasema ni maoni ya watnzania wote.
 
Hujui Historia wenye hekima zao walisema "No research no right to speak"Wewe peek yako huwezi kuwa na akili kuzidi tume na watanzania waliotoa maoni yao. Kumbuka zipo kanuni za maendeleo zinazizingatia wakati, mazingira na changamoto za wakati huo. Enzi za Karume na Nyerere fuatilia mazingira na changamoto zilizowapelekea kuunda muungano wa chapchap.

unaiua reserch methodology? smapling ilifanyika kutoka kwenye population gani? unaitisha watu 100 kati ya 100,000 harafu una hoji watru 20 then una conclude kuwa ndiyo maoni ya watanzania. nani kapinga serikali 3? nimesema tuwe na serikali 3 lakini majina yabaki. jenga hoja km msomi siyo kutukana. kwani jina linabadiri nini?
 
Nadhani ulitakiwa kusema kua watanzania wamsaliti mwalim Nyerere.
 
Kwahiyo kuirudisha Tanganyika ni kumsaliti Mwalimu kumbe?

Vip Uwanja wa kimataifa wa ndege Dar ulipopewa jina la Mwalimu J.K.Nyerere na baadae ukabadilishwa eti kisa wazungu wanashindwa kutamka hilo jina haikuwa usaliti huo? na je ilo jina liliathiri uwanja kwa aina yoyote ile? huo kwako si usaliti na mbona haukuwahi kulisemea ama ni interest minded?
 
hebu acheni kwanza twende likizo na hiki kitu kinaitwa muungano halafu tukirudi tutatia akili.
hebu fikiria wengine walikubali kuitwa tanzania bara ila wengine hawakukubali kuitwa tanzania visiwani sasa kuna dhambi gani sisi tusirudi kwenye utanganyika wetu.
malalamiko yamekuwa mengi na kila sehemu inaona ni ya msingi ni bora iwe hivyo.
ni rahisi kwa wazanzibar kujenga nyumba, kupata mashamba na kuajiriwa na kutumia vizuri raslimali za tanganyika lakini si kwa watanganyika walioko zanzibar.
wacha tuuvunje kwa kuwa tumeona busara tununue uhuru wetu kwa fedha na hasa ukichukulia wanaotuhitaji hawatuhitaji kwa sasa.
malalamiko yao ni madogo ukilinganisha na maslahi ambayo wao wanapata katika muungano , lakini ijulikane wazi kuwa hayo yote sio hitaji lao kwa sasa .wanachohitaji ni kujitawala zaidi na kuwa na mamlaka zaidi huenda wanaona wamebanwa. wapeni bana!
historia itakuwepo kwani kunauwezekano siku zijazo tukawa na nchi moja lakini kwa sasa wacha twende likizo.
wanajua dunia ya leo nchi yao ikiwa na uchumi mkubwa watakuja kama wawekezaji na kuchukua maeneo yetu kama wawekezaji
 
Kwahiyo kuirudisha Tanganyika ni kumsaliti Mwalimu kumbe?

Vip Uwanja wa kimataifa wa ndege Dar ulipopewa jina la Mwalimu J.K.Nyerere na baadae ukabadilishwa eti kisa wazungu wanashindwa kutamka hilo jina haikuwa usaliti huo? na je ilo jina liliathiri uwanja kwa aina yoyote ile? huo kwako si usaliti na mbona haukuwahi kulisemea ama ni interest minded?

Me navyojua uwanja wa ndege Dar Unaitwa Mwl J.K NYERERE hata juzi nilikuwa safari matangazo yalikuwa sasa tunaelekea kutua ktk uwanja wa jk nyerere DSM. hata ukipita pale utaona jina uwanja juu ya paa.
 
Hiyo nchi ni ya kufikirika au imeshawahi kuwepo?? Nchi a, b na ab(c), nisaidieni mfano basi. Shirikisho la ujerumani, mamlaka ya falme za kiarabu, usa, russia haikurudi soviet union, uk, madagascar, sudan, eritrea, korea kusini, kaskazini. Ok basi tuanze kuunda tanganyika-ndio mwakani ???
 
Kwahiyo kuirudisha Tanganyika ni kumsaliti Mwalimu kumbe?

Vip Uwanja wa kimataifa wa ndege Dar ulipopewa jina la Mwalimu J.K.Nyerere na baadae ukabadilishwa eti kisa wazungu wanashindwa kutamka hilo jina haikuwa usaliti huo? na je ilo jina liliathiri uwanja kwa aina yoyote ile? huo kwako si usaliti na mbona haukuwahi kulisemea ama ni interest minded?

Hiyo ni U-turn kama ilivyokuwa multipartism b4 uhuru na 1992,kila wakati una yake.
 
Huo ni ujinga wetu, kwani tukibadiri jina ndiyo umasikini utaisha, mimi nimesema serikali 3 ni mhimu lkn Tanzania ibaki kwa ajiri ya kulinda historia ya nchi yetu. tutatumia pesa nyingi kutangaza jina la Tanganyika katika ramani ya dunia. Najua hili halitapita.
 
Back
Top Bottom