Rais Kabila amempa kila mchezaji gari aina ya Toyota yenye thamani ya dola 60,00

Ashura9

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2012
Posts
740
Reaction score
485
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Joseph Kabila amempa kila mchezaji wa timu ya taifa, gari aina ya Toyota yenye thamani ya dola 60,000, kwa kushinda michuano ya CHAN. Rais Kabila pia aliwapa medali za dhahabu. DRC waliichapa Mali 3-0 jijini Kigali na kuwa timu ya kwanza kushinda michuano hiyo mara mbili.



Image copyright AFP
Image caption DR Congo walilaza Mali 3-0 kwenye fainali
Image caption Kila mchezaji ametunukiwa gari la $60,000

Mwandishi wa BBC Mbelechi Msochi anasema mchezaji Heritier Luvumbu Nzinga aliyeumia kwenye michuano hiyo pia ameahidiwa kwamba atasafirishwa ng'ambo kwa matibabu.

Chanzo: BBC
 
F edha za uchaguzi hazipo DRC. What tears to cry for east and central now that we the people are no longer masters?
 
Prezidaa José Desire Kabila wa DRC, ametoa zawadi ya Gari yenye thamani ya US $60,000/= kwa kila mchezaji wa timu ya Taifa aliyecheza kufanikisha timu kuchukua Ubingwa wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza nyumbani (CHAN). DRC iliweza kubeba Kombe hilo baada ya kuitungua Mali mabao 3 kwa 0.

Nchi ya DRCongo ambao ni majirani zetu, timu yake TP Mazembe ndio Klabu Bingwa ya Africa. Timu yake ya Vita nayo inafanya vizuri kwenye mashindano ya vilabu vya Afrika. Muundo wa wachezaji wa DRC kutoka Ligi bora, ilitabiriwa mapema Kombe kuchukuliwa na DRC.
Taifa Stars tujitahidi, siku moja tutalibeba na kila mchezaji atapewa zawadi ya......

Hongera sana Democratic Republic of the Congo (DRC).
République démocratique du Congo (French)
Repubilika ya Kôngo ya Dimokalasi (Kongo)
Republíki ya Kongó Demokratíki (Lingala)
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Swahili)
Ditunga dia Kongu wa Mungalaata (Tshiluba)
 

Hapa kuna kitu cha kujifunza kwa nchi inayopenda na kuendekeza siasa kwenye kila sekta kama Tanzania. Kila kitu sisi tunakifanya kisiasa siasa tu! full ubabaishaji.

Mungu Ibariki Tanzania. One day yes!!
 

Huku kwetu tungeishia kuwapa mifuko tu ya mboga mboga za MATEMBELE.
 
Naona tunazidi kujidhalilisha tu kwa gari Kama Hilo serikali ya Tanzania inauziwa kwa 250million Na DT Dobie au mzabuni yoyote Yule aliyeshinda Tenda Hiyo ingawa gari za serikali hazilipiwi kodi hiyo bei sijui wanitoa wapi?!!!! Hii sheria ya manunuzi ni JIPU lingine kubwa kama kitambi cha Mzee Wasira
 
Hpa kweli unaweza kusema pesa hiyo ilikuwa kwenye mpango? imetolewaje?.....ukienda mbele zaidi ...unaona afadhali hatawao ambao wanawapa wachezaji wanaoiletea heshima nchi kuliko sisi!! Ufisadi tuuuu...mpira wenyewe hatujui , amani tunayojidai nayo feki pia...!!
 
Mmmh hapo kwenye kitambi cha Wassira unamtafuta ubaya mzee wa porii.. A.k.a tyson
 
angewapa mawili mawili nchi tajiri kama congo kabila kawabania tu ila kidogo ni cha mwenye haki
 
DUUUH!! Bravo President Kabila!! Bonge La Motisha Kwao!!!
 
Africa maajabu huwa hashaishi, Nchi inashindwa kufanya uchaguzi sababu haina fedha, lakini fedha za kununulia magari ya zawadi ipo. Africa kazi tunayo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…