Rais Kagame ateua mwanamke kuongoza Idara ya Intelejensia

Rais Kagame ateua mwanamke kuongoza Idara ya Intelejensia

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wakati hapa nyumbani kundi la wagombea wa kiume limepita bila kupingwa huku wanawake wakiendelea na uchaguzi na wengine kuenguliwa, kule Rwanda Rais Kagame amemteua mwanamama kuongoza idara ya Intelejensia ya nchi hiyo.

Wanaume tukiendekeza kitonga akina Ummy ndio watakaobeba mikoba siku za usoni kwa sababu wanajijengea ujasiri kwa kupambana na mambo magumu.

Akina baba tunakumbushana tusijisahau sana.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kuna siku huwa unajitoa akili mpaka unakera. Lakini wewe niwanaCCM pekee JF mwenye akili timamu, wengine anatembea nazo Polepole na inategemea siku hiyo kaamkaje.

Ulichoandika kwa jicho la Mwewe ni kizito sana, lakini Nani anakusikiliza huko CCM. Kuna wilaya mkoani Rukwa katibu wa CCM anamuuliza DED, imekuwaje kata zote 18 za wilaya hii hakuna hata moja tuliyopita bila kupingwa?

Ni aibu kubwa kwa mtu Kama NAPE kujipitisha bila kupingwa, mwangalie January, Kigwangala!! Mengine ni aibu!!!!!!!
 
Wanaume wengi wa Kitanzania ni majinga
 
Asili ya wanaume wa Tanzania wanapenda kulialia angalia Lissu anavojiliza Uraisi unadhani atauweza?
 
Kama lissu anataka apewe urais kwa kua tu alipigwa risasi

Na wewe kapigwe risasi 16 utibiwe nje ya nchi kwa miaka mitatu kisha urudi kukabiliana na aliyekupiga risasi huku akiwa anamiliki vyombo vyote vya ulinzi na usalama,mahakama,NEC nk. Fukiria kwa makini halafu uone kama ni jambo rahisi kama ilivyo rahisi kuandika hapa JF ukitumia false identity.
 
Wanaume wanatia aibu yani wanajitengenezea viti maalumu kwa mgongo wa kupita bila kupingwa.​
 
Wanaume wa CCM ndio wenye uwezo wa kubaka demokrasia. Akina Ummy mwalimu wako kazini kuendelea kuomba Kura pamoja na umahiri wake
 
Mkuu mbona hata hapa kuna Dr. Makakala wa Uhamiaji ?? Hiyo itakua mpya huko Rwanda ila sio hapa nyumbani.
 
Wanawake washapewa nafasi za ubunge wa viti maalum hii ipo fair, kama ndio ivi basi mnavyotaka kuwe na wabunge wengi wa kike basi kuwe na utaratibu wa kuwa na jinsia tofauti kati ya mbunge na mbunge viti maalum
 
Back
Top Bottom