Rais Kagame katupa taulo, shujaa wa Hotel Rwanda, Paul Rusesabagina kuachiliwa huru

Kukichwa kutapambazuka...!
 
Kwenye hili mwana majanga naungana na wewe
 
Malango ya gereza yamefunguka mjini Kigali, Rwanda kwa ajili ya Paul Rusesabagina, mwanaharakati na mpinzani mkali wa serikali ya Paul Kagame.

Siku 939 zimepita tangu Paul Rusesabagina akamatwe katika uwanja wa ndege wa Kigali. Ni baada ya ndege aliyopanda huko Dubai kutua mjini Kigali badala ya kuelekea Burundi alikoalikwa kuzungumza katika kabisa moja la kiinjili. Baadae waziri wa sheria wa Rwanda, Johnston Busingye alikiri kwamba serikali ya Rwanda ilifanya malipo kwa ndege ya GainJet ili itue Rwanda badala ya Burundi, lengo likiwa ni kumkamata Paul Rusesabagina.

Mashtaka aliyopewa ni pamoja na ugaidi na uhaini.

Serikali za Marekani na Qatar ziliingilia kati na hatimaye Paul ameachiwa huru baada ya miaka karibu mitatu. Atarudi Marekani yalipo makazi yake ya kudumu, ingawa ni raia wa Rwanda na Ubelgiji.

Paul anajulikana kwa ushujaa wake wa kuwaokoa Wanyarwanda takribani 1200 wakati wa mauji ya halaiki ya 1994. Aliwaficha wananchi hao katika hoteli aliyokuwa akifanya kazi kama Meneja. Tukio hilo liliwashawishi watu wa Holywood kutengeneza filamu iliyoitwa 'Hotel Rwanda', ikieleza mauaji ya halaiki ya 1994 nchini Rwanda.

Mwaka 1996, Paul alinusurika kuuawa nchini Rwanda na kukimbilia Ubelgiji ambako alifanya kazi kama Dereva Taxi. Baadae alihamia nchini Marekani na huko alipewa tuzo za hadhi ya juu chini ya Rais George Bush.
Mwaka 2012 alianzisha chama cha siasa kiitwacho Party for Democracy in Rwanda (PDR) kwa lengo kuu la 'kupinga udikteta nchini Rwanda'.

Rwanda ipo katika mchakato wa kuboresha mahusiano yake na Marekani ambayo yamedorora hivi karibuni. Wakati huohuo Rwanda ipo katika mchakato wa kushirikiana na Qatar katika biashara ya usafiri wa anga.
Mamlaka za Marekani na Qatar ndizo zilizoshawishi kiachiwa kwa Paul Rusesabagina.

Ni sahihi kusema Rwanda imemuachia huru Paul Rusesabagina kwa faida za kidiplomasia na kiuchumi.
 
Dr. Chris Cyrilo

Inapendeza, alikamatwa kwa sababu za kumkosoa vikali mara kwa mara Rais Kagame...
 
Nakala kwa: GENTAMYCINE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…