Rais Kenyatta aruhusu Watanzania kuanza kufanya kazi na biashara Kenya bila kuwa na Work Permit wala Business visa

Rais Kenyatta aruhusu Watanzania kuanza kufanya kazi na biashara Kenya bila kuwa na Work Permit wala Business visa

Piga kelele kwa Kenyatta akee๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜

Seriously, EA hatutakiwi kuwa na barrier zozote za kibiashara. Tuna custom union ya maneno tu lakini haifanyi kazi. Tunazuia na kubania biashara za Kenya huku tukijaza masoko kwa bidhaa za India na China. EA inatakiwa kufunguka, iwe kama nchi moja. Hapo ndiyo tunaweza fikia shirikisho la kisiasa
Acha kuweweseka mkuu, wakenya ni zaidi ya uwajuavyo...anachokisema sicho anachotenda.

Mkenya akikuangalia machoni na kukuchekea usikenue kwanza..angalia nyuma yako kujiridhisha.
Hawa jamaa nimefanya nao kazi. Ninawafahamu vilivyo.
 
Nakushauri, kamwe usikubali kujiaminisha hiki kitu. ni watu wakawaida tu.
mkuu ungeona jinsi wanavyokabili matatizo yao kitaalamu usingesema kitu hapa ,
kenyans ni smart kuliko sisi no doubt.
leo sisi tumejenga barabara kituko ubungo kibaha , zebra kibao kwenye super highway, matokeo yake ni ajali za waenda kwa miguu na boda boda kila siku , na matokeo yake foleni sasa imeahamia kibaha to mlandizi, angalia thika highway uone kama kuna makosa kama hayo,
sijui nani katushauri kuweka barabara za zege vituoni, kongowe kwa mfano, angekuwa mkenya pale angeweka under pass kwa gharama hizo hizo zetu na akatatua tatizo for good.
 
ni kweli mkuu..
lengo lake ni tanzania iseme the same, ili pia waje wafanye biashr upande wa pili bila permit..

na sisi tukifuata hilo, wakenya watakuwa wame win
Sasa kwanini muogope kufanya biashara?
 
It is sir. And i think we both told the same thing, look kufiri nje ya box ni kule kule tu kuwa na high intelligence. So the question comes kufikiri nje ya box kwa jicho gani ? Kenyans think out of box on wining us

Hii taasis ya Equity na KCB si ni za Kenya ? Surprisingly wataka occupy hizi huduma za kibank nchini. Siunaiona CRDB Sasa ?
kufikiri nje ya boksi si lazima uwe intelligent. anybody with thinking capacity ya kawaida anaweza fanya hivyo. na hiyo creativity which sio lazima uwe na higher intelligence.

ukiwa na exposure or experience na international business world. simply unaweza kuona.
 
Majinga nyinyi sukuma gang,, Jiwe aliharibu mahusiano mazuri na majirani zetu,
Angalia maneno unayoyatumia. Nina hisi huna uzoefu wa mambo mengi hasa ya Siasa. Tangazo la kwanza la Kenyata kuruhusu wana East Africa kuingia Free nchini kwake ilikuwa siku anapoapishwa kwa muhura wa pili. Sasa nini kilimfanya aanze kuwazuia Waganda na Watanzania? Mtu asiye na taarifa kama wewe anadhani maamuzi ya Kenya yalikuwa Tanzania pekee na Uganda pia. Tuache akili za Kitumwa kama zako.
 
Acha kuweweseka mkuu, wakenya ni zaidi ya uwajuavyo...anachokisema sicho anachotenda.

Mkenya akikuangalia machoni na kukuchekea usikenue kwanza..angalia nyuma yako kujiridhisha.
Hawa jamaa nimefanya nao kazi. Ninawafahamu vilivyo.
Watanzania ni watu wavivu sana kwenye sehemu zao za kazi, bora jiwe alivyo ondoka na makampuni nyingi na taasisi binafsi sasa ma CEO watakuwa wa Kenya

Watanzania ni wavivu na wazembe wanawaza kupiga tu ma deal...
 
mifumo yetu ya kodi ilio kandamizi na isiyo rafiki kwa wafanya biashar, hasa kwa miaka 5 nyuma, kwa mwendo wa mama itarekebiaka..

kufanya biashra ama kuwekeza kenya kama mtanzania hilo sahau, labda kuuza mitumba au kuimpot bidhaa zao za viwanda kuja kuzitupia huku
sijaelewa unazungumzia mazingira gani ya biashara ,
watanzania tupo gifted na rasiamali pamoja na ardhi nzuri , hii ni default .Mazingira ya kibiashara yakiboreshwa mtanzania anaweza kupeleka products zetu kenya moja kwa moja na kupata soko huko , kumbuka bidhaa zetu nyingi kenya zinajiuza zenyewe ,
 
sema hawa jamaa sjawahi kua na imani nao, uwekezaji ni muhimu sawa ila sheria ziwekwe nzuri haya mambo ya kubrand mlima kilimanjaro kenya iwe mwisho
swala la ku brand ni sisi wenyewe tumezubaa miaka mingi. tulikuwa hatufany serious publications za huu mlima.

Imagine mpaka ghana wanadhan mlima uko kenya kumbe uko tz. na sisi tuliridhika tukabweteka tu kwa vile ulikuwa kwetu
 
Amesemea hilo pia kuwa nchi zetu zisiwe na mentality ya kuwa sisi ni washindani bali wanaoshirikiana sio wanaoshindana .Tukijuana kama wanaoshirikiana watakaofaidi ni wananchi wetu wa nchi zote mbili
Alipaswa kwenda mbali zaidi na kusema ni kwa nini hasa mahindi ya Tanzania na Uganda yamezuiliwa kuingia nchini kwake. Ametoa siku mbili yaruhusiwe kuingia. Je, baada ya hizo siku mbili hayatakuwa na hiyo sumu kuvu tena?

Naona fedhaha nchi yangu kuyumbishwa yumbishwa na hao manyang'au. Naona wameshika hatamu tena. Tunacheza ngoma yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sijaelewa unazungumzia mazingira gani ya biashara ,
watanzania tupo gifted na rasiamali pamoja na ardhi nzuri , hii ni default .Mazingira ya kibiashara yakiboreshwa mtanzania anaweza kupeleka products zetu kenya moja kwa moja na kupata soko huko , kumbuka bidhaa zetu nyingi kenya zinajiuza zenyewe ,
sisi tunauza kwao raw products wao wanaziproces, kisha kuja kuziuza tena huku mara nne ya bei walionunulia huku..
nje ya mazao na malighfi hatuna finished products zenye soko la hakika kenya..

tushukur Mungu sheria ya ardhi inayozuia mgeni kumiliki ardhi, tungeisha. Na wao hawaipendi mnoo hii sheria yetu..
 
Hapa tumetupiwa ndoano, tukiingia tumenasa na mwisho wake ni mgogoro mkubwa sana...

Labor force ya Tanzania ni unskilled, Kenya wanalabor force kubwa skilled hapa tumeumia.
Makampuni mengi ya kimataifa, kienglish aka kiingereza aka kikristo ndio priority kwenye kutoa ajira, hapa wabongo tutapigwa maana wengi wasomi kiingereza cha kuunga unga...
Sasa huoni tukipata skilled labour faida ni kwetu sisi?
 
Precision air inamilikiwa na kenya airways..huwezi kulinganisha na ATCL
Sasa kama inamilikiwa na Kenya Airways na bado inafanyiwa figisu. Nini kinakuaminisha kuwa ATCL kwenye route hiyo itapata huruma kibiashara?.
 
mkuu , wakenya sio wajanja ila wapo smart kichwani na wengi shule imewasaidia .
huku kwetu mtu level ya phd anafanya vitu hata mganga wa kienyeji anashangaa halafu unataka mtu huyu apate attention level za international?
Hujakosea ndiyo vizuri itatupa changamoto ili nasi tushindane tuwe smart kichwani kuliko wakenya.
 
Speak for yourself not for the rest of us. Kama wewe unajions hauko intelligent pambana na hali yako. Tupo ambao tunashindana na wakenya ligi moja na tunawazidi
Safi sana. Hili jiwe limempata tena la kwenye paji la Uso.
 
sisi tunauza kwao raw products wao wanaziproces, kisha kuja kuziuza tena huku mara nne ya bei walionunulia huku..
nje ya mazao na malighfi hatuna finished products zenye soko la hakika kenya..

tushukur Mungu sheria ya ardhi inayozuia mgeni kumiliki ardhi, tungeisha. Na wao hawaipendi mnoo hii sheria yetu..
Nadhani kuprocess na kuuza bidhaa zetu kwetu kwanza na kisha Kenya inawezekana tukiamua. Kama ni kufurika soko na finished products tufurike na za kwetu pia na tuuze kwao kwa bei nafuu kuliko vya kwao wenyewe. Hawa watu siyo wa kuwaamini ila siyo wakuwaogopa pia. Kazi kwetu wenyewe kujihakikishia tunawea kushindana.
 
Back
Top Bottom