Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Wewe una akili fupi kiasi fulani.Pedi zenyewe kwanza zina ubora? Mabinti wetu wasije wakageuzwa jalala la bidha feki toka ng'ambo. Tanzania wanachanja mabinti wao chanjo dhidi ya Cervical Cancer, kenya inaidhinisha matumizi wa pedi feki zinazochochea kuugua Cervical Cancer!
Naona umechanganya mambo hapa.
Hakuna uhusiano wowote kati ya Pedi na kansa ya shingo ya kizazi(Cervical Cancer). Kama kuna watanzania wanaamini kuna pedi zinaleta Saratani hao watakuwa mataahira, na wakenya watazidi kutudharau sana.
Chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi ipo duniani kwa zaidi ya miaka 30 sasa, majaribio ya mwanzo kabisa kutolewa kwa Kenya yalifanyika zaidi ya miaka 10 iliyopita. Kwa Kenya hiyo chanzo imekuwa ikitolewa kwenye hospitali nyingi miaka mingi sana kwa kulipia pesa kabla hata serikali ya Kenya kuja kuanza kuitoa bure.
Kuna mambo tunaweza kujaribu kushindana na Wakenya lakini sio kwenye Elimu, Uchumi, Afya na Demokrasia. Katika hayo wakenya wako mbali mno. Wakenya wanapambana kufikia na kuzipita nchi kama South Afrika na Ghana lakini sio Tanzania. Tanzania bado sana.