Rais Kenyatta: Hatuwezi kuendelea na lockdown

Rais Kenyatta: Hatuwezi kuendelea na lockdown

Kenya wala hawaigi umagufuli. Msingi mkuu wa umagufuli ni kuzuia data, ili watu waseme Korona hakuna Tanzania. Kenyatta ametoa data kama anavyofanya daima. Hajafukuza wataalamu wa afya. Sisi tuko wenyewe tu, sema kidoogo tunafanana na Brazil. Sema nao hawajazuia data
Hahahahaha... Mbowe, Zitto na Membe wanaumbuka vibaya!
Wote hawa walisema tutatengwa na majirani, na majirani wenyewe ndio hawa!

Mtu una maambukizi 10 unafungia watu, yamepanda hadi 1200 unawatoa nje, hizi akili au matope?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania ni independent thinkers Wakenya akili zao zimeshikwa na wazungu. Tanzanias we are not copy cats hatu copy na kupaste solution za corona za wengine because we are independent thinkers tukiongozwa na independent thinker Genious Raisi Magufuli
ili andiko lako naliandika kwenye pvc laini pana sana naprint alafu nalifunga mtaani juu ya nguzo za umeme linakatiza mtaa uku na uku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hiyo 'curfew' na lockdown ilikuwa na kazi gani? sometimes sisi binadamu tunakuwa kama wajinga vilee..haina maana kutesa watu bure sasa hivi watu wanarudi kuchangamana kama kawa,hata kama hakuambukizwa kipindi cha 'curfew', ataambukizwa sasa.


Mnyonge mnyongeni lakini Magufuli ni genious.
Kwanini taarifa zinafichwa na watu walikuwa wanazikwa usiku?
 
Kenya wala hawaigi umagufuli. Msingi mkuu wa umagufuli ni kuzuia data, ili watu waseme Korona hakuna Tanzania. Kenyatta ametoa data kama anavyofanya daima. Hajafukuza wataalamu wa afya. Sisi tuko wenyewe tu, sema kidoogo tunafanana na Brazil. Sema nao hawajazuia data
Nae itafika mahali hutasikia data wala bando.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli oyeeeeee. Trump naye kakiri kuwa kuna Mungu. Uhuru naye Kaduna na kufungia watu ndani
- Rais alisema serikali imeafikia uamuzi wa kuwa haiwezi kuendelea kuwafungia watu.

- Alisema sasa itafikia wakati wa watu wenyewe kujilinda dhidi ya maambukizi ya coronavirus

- Nchi jirani ya Tanzania ni mojawapo wa zile ambazo hazikufunga shughuli zake za kuchapa kazi kwa ajili ya covid-19

Rais Uhuru Kenyatta ameashiria huenda 'curfew' iliyowekwa ikafunguliwa baada ya kukamilika wiki ijayo siku 21 zilizowekwa zikikamilia.

"Tumeona sisi kama serikali kuwa hatuwezi kuendelea kuwa na lockdown . . . na 'curfew'. Sasa ni lazima Wakenya warudi kwenye makazi yao na shughuli zao," Rais alisema.

Rais alisema sasa nijukumu la Wakenya kuhakikisha kuwa maambukizi ya coronavirus yanakabiliwa wakati ambapo taifa litafunguliwa.

"Sasa kwa sababu hatuwezi kuendelea na kufunga, tukifungua, halafu ugonjwa huu uendelee ujue ni wewe, na mimi na Matiang'i kuhakikisha kuwa tunalinda kila mmoja," alisema Rais.

Rais Uhuru Kenyatta alisema serikali imeafikia uamuzi wa kuwa haiwezi kuendelea kuwafungia watu.

"Nimewaeleze hawa mawaziri, haswa wa Afya kuwa Wakenya sasa wajue ni wakati wa kulindana.

Wewe ukienda kazi ni wajibu wako kulinda mama na watoto, kama serikali zile zingine kila pahali hatuwezi kuendelea kufungia watu," aliongeza Rais.

Rais alisema hayo wakati ambapo idadi ya maambukizi imefikia watu 1192 na watu 50 kufariki.

Wakenya wamekuwa kwenye kafyu ya kutokuwa nje ifikapo saa moja usiku kwa siku 28.
Kaunti tano za Nairobi, Mombasa, Kwale, Kilifi na Mandera pia zilifungiwa kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi.
Mitaa ya Eastleigh Nairobi na ule wa Kale Mombasa pia ilifungwa na hakuna watu kuingia au kutoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni sehemu ya hotuba ya Rais wa Uhuru Kenyatta mapema leo kwa wananchi wa kenya dhidi ya covid-19.
...
Aidha, rais amesema kuwa taifa hilo haliwezi kuendelea kuchukua hatua za kusalia ndani milele.

''Sisi kama serikali, kama serikali zingine, mataifa yote dunia zimeanza kuona, hatuwezi kuendelea kusema wakenya tukae nyumbani, hatuwezi kuendelea kusema tu wakenya msiende kufanya biashara, musiende makazi, namna hio."

Aliendelea kusema "lakini, ile kitu ambayo itatusaidia pia kwa kikamilifu kuhakikisha ya kwamba tumeweza tena kufungua uchumi wetu na wananchi waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida."

"Nimewaambia wenzangu, hii haitakuwa kwa sababu ya yale serikali itatenda, itakuwa kwa sababu ya yale kila mmoja wetu kwa kibinafsi atafanya''.
...

Nadhani kuna haja ya kumwambia bila haibu as "Mheshimiwa rais Magufuri wewe uliona mbali yapasa tujifunze kutoka kwako".

Ila wanaona haibu kumtaja.


NOTE:
Mwingine naye huko ughaibuni comrade Trump ameruhusu nyumba zote za ibada zifunguliwe na watu wamuombe Mungu na sehemu zote za ibada kuwa sehemu maalum.
 
Back
Top Bottom