Rais Kenyatta: Hatuwezi kuendelea na lockdown

Hahahahaha... Mbowe, Zitto na Membe wanaumbuka vibaya!
Wote hawa walisema tutatengwa na majirani, na majirani wenyewe ndio hawa!

Mtu una maambukizi 10 unafungia watu, yamepanda hadi 1200 unawatoa nje, hizi akili au matope?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ili andiko lako naliandika kwenye pvc laini pana sana naprint alafu nalifunga mtaani juu ya nguzo za umeme linakatiza mtaa uku na uku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini taarifa zinafichwa na watu walikuwa wanazikwa usiku?
 
Nae itafika mahali hutasikia data wala bando.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli oyeeeeee. Trump naye kakiri kuwa kuna Mungu. Uhuru naye Kaduna na kufungia watu ndani
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni sehemu ya hotuba ya Rais wa Uhuru Kenyatta mapema leo kwa wananchi wa kenya dhidi ya covid-19.
...
Aidha, rais amesema kuwa taifa hilo haliwezi kuendelea kuchukua hatua za kusalia ndani milele.

''Sisi kama serikali, kama serikali zingine, mataifa yote dunia zimeanza kuona, hatuwezi kuendelea kusema wakenya tukae nyumbani, hatuwezi kuendelea kusema tu wakenya msiende kufanya biashara, musiende makazi, namna hio."

Aliendelea kusema "lakini, ile kitu ambayo itatusaidia pia kwa kikamilifu kuhakikisha ya kwamba tumeweza tena kufungua uchumi wetu na wananchi waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida."

"Nimewaambia wenzangu, hii haitakuwa kwa sababu ya yale serikali itatenda, itakuwa kwa sababu ya yale kila mmoja wetu kwa kibinafsi atafanya''.
...

Nadhani kuna haja ya kumwambia bila haibu as "Mheshimiwa rais Magufuri wewe uliona mbali yapasa tujifunze kutoka kwako".

Ila wanaona haibu kumtaja.


NOTE:
Mwingine naye huko ughaibuni comrade Trump ameruhusu nyumba zote za ibada zifunguliwe na watu wamuombe Mungu na sehemu zote za ibada kuwa sehemu maalum.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…