Rais Kenyatta na Raila Odinga wamekubaliana kumaliza mgawanyiko uliopo na kulifanya taifa hilo kuwa moja

Rais Kenyatta na Raila Odinga wamekubaliana kumaliza mgawanyiko uliopo na kulifanya taifa hilo kuwa moja

_100346249_kenya3976.jpg

<b>Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekutana na kiongozi wa muungano wa upinzani nchini humo Raila Odinga katika afisi yake Jumba la Harambee, Nairobi.</b>

Wawili hao wamekubaliana kuundwe mpango wa pamoja wa kuangazia utekelezaji wa malengo ya pamoja ya viongozi hao wawili, ambao utazinduliwa rasmi karibuni

Balozi Martin Kimani ataongoza kuundwa kwa mpango huo upande wa Rais Kenyatta naye mshauri wa Bw Odinga Paul Mwangi atawakilisha Bw Odinga, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotiwa saini na Bw Kenyatta na Bw Odinga baada ya mkutano huo.

Mkutano huo umefanyika muda mfupi kabla ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson kuwasili nchini humo kwa ziara ya siku nne.

Marekani imekuwa ikihimiza kufanyika kwa mazungumzo na mashauriano kutatua mzozo wa kisiasa uliokumba taifa hilo baada ya uchaguzi uliojaa utata mwaka jana.

Bw Odinga alitangulia kuhutubia taifa moja kwa moja na baadaye Bw Kenyatta akatoa hotuba yake.
_100346687_uhuruw.jpg


Bw Kenyatta amesema wamekubaliana na Bw Odinga kwamba taifa la Kenya ni muhimu kuliko mtu binafsi na kwamba lazima viongozi washirikiane.

Rais huyo amesema siku za usoni za Kenya haziwezi kuongozwa na uchaguzi ujao bali "uthabiti wa taifa."

"Demokrasia si mwisho wa kila kitu. Ni shughuli na nia ya wananchi lazima iongoze."

"Tumekubaliana tutaleta pamoja wananchi na kujadiliana kuhusu matatizo yanayoathiri taifa letu na wananchi, na kuunda taifa lenye umoja na lililo imara ambapo hakuna araia anayehisi ametengwa."

"Huu ni mwanzo mpya kwa taifa letu."

"Tunaweza kutofautiana lakini kusalia tukiwa tumeungana kama Wakenya."


Bw Odinga amesema kwa muda mrefu Kenya imeangazia kubadilisha taasisi na miaka saba iliyopita katiba mpya ilianza kutekelezwa.

"Sasa lazima tuwe na ujasiri wa kukubali kwamba hilo halijafanikiwa. Bado hatujabadilisha mengine," amesema Bw Odinga.

"Ndugu yangu na mimi tumekutana pamoja leo na kusema yamefikia kikomo. Tumekataa kuwa watu ambao chini yake Kenya imekuwa taifa lililofeli."

Bw Odinga amesema wamekubaliana kufanikisha mabadiliko yatakayofanikiwa mageuzi nchini humo, na pia kukomesha kulaumiana.

Amewataka Wakenya waunge mkono mpango wa viongozi hao wawili.

"Tumesafiri mbali sana kiasi kwamba hatuwezi kurudi tena bandarini. Isitoshe, hatuwezi kufika tunakoenda bila kufanya mabadiliko la sivyo tutazama baharini," amesema Bw Odinga.

"Tumekuja pamoja na ndugu yangu Kenyatta, tumeongea kwa kirefu na kukubaliana kwamba tunataka kuunganisha Kenya iwe taifa moja. Mgawanyiko ambao umekuwepo tangu uhuru utakwisha hapa na sisi. Tutembee pamoja," amesema Bw Odinga.

  • 8 Agosti, uchaguzi mkuu wafanyika ambapo Bw Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi
  • 1 Septemba, Mahakama ya Juu yabatilisha ushindi wa Bw Kenyatta katika kesi iliyowasilishwa na Bw Raila Odinga, na kuagiza uchaguzi urudiwe
  • 26 Oktoba, uchaguzi wa marudio wafanyika, huku upinzani ukisusia. Bw Kenyatta atangazwa mshindi.
  • 30 Januari, Bw Odinga ala kiapo kuwa 'Rais wa Wananchi' na kusisitiza kwamba hatambui Bw Kenyatta kama rais halali wa Kenya
  • 9 Machi, Bw Kenyatta akutana na Bw Odinga katika afisi ya rais Jumba la Harambee, wawili hao waahidi kushirikiana kuwaunganisha Wakenya.
Kushinikiza mageuzi
Bw Odinga alisusia kushiriki uchaguzi wa marudio uliofanyika 26 Oktoba mwaka jana akishinikiza mageuzi yafanywe kwanza katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Uchaguzi huo ulitokana na hatua ya Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 Agosti ikisema ulikuwa na kasoro nyingi.

Mahakama hiyo ilikuwa inatoa uamuzi katika kesi iliyokuwa imewasilishwa na Bw Odinga kupinga matokeo hayo.

Bw Kenyatta alishinda uchaguzi huo wa marudio kwa kura 7.5 milioni ambazo ni sawa na asilimia 98 ya kura zilizopigwa.

Idadi ya waliojitokeza ilikuwa ni asilimia 38.84 ya waliokuwa wamejiandikisha kushiriki uchaguzi huo.

Uchaguzi ulitatizika sana katika maeneo yenye wafuasi wengi wa upinzani. Katika majimbo manne magharibi mwa Kenya ambayo ni ngome ya Bw Odinga, uchaguzi uliahirishwa kwa siku kadha na baadaye haukufanyika.


Tanzania Kuna somo la kujifunza pande zote.
 
Wameiga alichokifanya magufuli kuonana na lowasa.

Magufuli oyeèeeeee
Chama cha mafisi CCM oyeèeeeeee
Ahad hewa oyeeèeeee
 
Kuna watu walipoteza maisha kisa odinga,kuna watu walifukuzwa nchi kisa odinga,kuna watu wamepata vilema vya maisha kisa odinga,kamwe sintokaa nimwamini mwanasiasa
Yaani wewe bado unaamini katika siasa za afrika? Tangu slaa ajiuzulu CDM nilishasignout politics za watu weusi
 
Tukutane kwa mazungumzo kwa isssue ipi sisi ni tofauti na Kenya kaka,Raila na Uhuru wanakutana kutokana na mapungufu yaliyotokana na uchaguzi uliorudiwa je hapa Tanzania ni kipi cha kuzungumza na wapinzani,hakuna mgogoro na uchaguzi ulishapita salama salimini,au unataka wakutane for the sake of kukutana tu kisa Raila na Uhuru wamekutana?
Wapinzani wanauawa kila siku wewe huoni kama hilo ni tatizo? Basi Rais wenu anahusika
 
Wakati mgombea urais wa UKAWA mzee Lowassa alipozuru Ikulu ya magogoni vijana wa Ufipa walitoa povu sana wakimshutumu kwa kitendo kile. Leo Rais Uhuru ambaye ni swahiba wa Lowassa ( siyo Chadema) amempokea kiongozi wa upinzani na kuweka tofauti zao pembeni ili kuinusuru Kenya. Chadema wanapaswa kujifunza kuwa siasa sio uadui hivyo wanapaswa kushirikiana na Lowasa katika jitihada zake za kumuunga mkono mh Rais Magufuli. Ahsante!
 
Huyu odinga kuna watu wameumia kwa ajiri yake,

Huyu odinga kuna watu wamekufa kwa ajili yake.

Huyu odinga kuna watu wapo wamefugwa jela kwa ajiri yake

Huyu odinga wamepata vilema kwa ajiri yake .

Yaaani hawa watu kama wasingemuunga mkono odinga au wangejitenga na siasa za odinga leo hiii wasingekuwa vilema,wasingefungwa jelaa, wasingekufa,wasingeumia badala yake wangeishi kama malaika tuu.

Onana sasa waliyemuangaikia odinga dhidi ya kenyata wanaishi kwa shida wakati mwenzao amekutana na kenyatta leo wakizungumza jinsi gani ya kugawana keki ya taifaaa.

Poleni sana wakenya odinga alichikuwa anakitafuta sasa amekipataa vifo vyenu nyinyi na matatizo mliyoyapata ndio alichokuwa anakitaka odinga nyinyi mfeee kwa ajili yake kwa manufaa yake
 
Tukutane kwa mazungumzo kwa isssue ipi sisi ni tofauti na Kenya kaka,Raila na Uhuru wanakutana kutokana na mapungufu yaliyotokana na uchaguzi uliorudiwa je hapa Tanzania ni kipi cha kuzungumza na wapinzani,hakuna mgogoro na uchaguzi ulishapita salama salimini,au unataka wakutane for the sake of kukutana tu kisa Raila na Uhuru wamekutana?
Kwahiyo maalim hana mgogoro hadi kususia uchaguzi

Kwahiyo chadema hawana mgogoro wa uchaguzi ilihali hapo nyuma tumeona wakisusia chaguzi

Wapinzani wana madai mengi tu hasa katiba mpya yenye tume huru na mfumo bora wa uchaguzi achilia mbali uhuru wa kisiasa na haki za vyama vingi to mention a few

Tusipende kukejeli kila kitu wenzetu wakenya wamefanya la maana sana tuige itapendeza
 
Wakati mgombea urais wa UKAWA mzee Lowassa alipozuru Ikulu ya magogoni vijana wa Ufipa walitoa povu sana wakimshutumu kwa kitendo kile. Leo Rais Uhuru ambaye ni swahiba wa Lowassa ( siyo Chadema) amempokea kiongozi wa upinzani na kuweka tofauti zao pembeni ili kuinusuru Kenya. Chadema wanapaswa kujifunza kuwa siasa sio uadui hivyo wanapaswa kushirikiana na Lowasa katika jitihada zake za kumuunga mkono mh Rais Magufuli. Ahsante!
Usilinganishe.... Lowassa alienda ikulu bila kuwasiliana na upinzani ila odinga alishakubaliana na kina musyoka get the difference

Pia lowassa hakusema wamemaliza tofauti alisema TUMUUNGE MKONO bila kusema jinsi gani watasuluhisha difference zetu ila odinga na uhuru wamesema wazi watakuja na ACTION PLAN so at least wapinzani wa kenya watagain something as in malalamiko yao hayajaenda bure

So kuna difference kubwa sana all in all odinga kafanya la maana
 
Raila na Uhuru ni viongozi wa kweli, wanaangaliana kwa macho na kuitana ndugu yangu. Huu ndo ukomavu wa kisiasa tunaoutaka. Hamna haja ya chuki zisizokuwa na tija. Kenya hoyee!
Heri yenu mna viongozi wenye akili, bongo wamebeba vifuu vya nazi mukichwa.
 
Tanzania magufuli na lowasa walikutana na kuongea, kilichofuata ni kumponda lowasa mzee watu akaona aii isiwe shida akajikalia kimya, leo utasikia tuinge Kenya wakati Tanzania yameshatokea tukatukana.
Hawakuongea lolote kuhusu maslahi ya upinzani na kumaliza mgogoro wa upinzani na serikali zaidi alitangaza kumuunga mkono juhudi zake sasa ulitaka wapinzani washabikie ilihali lissu kamiminiwa risasi na ben saanane hajulikani alipo

Ila magu and lowassa wangesema wamemaliza TOFAUTI ZA UPINZANI na kwamba MADAI yao atayafanyia kazi kila mtu angepongeza mazungumzo yale kiufupi hayakuwa na faida yoyote kwa upinzani
 
Usilinganishe.... Lowassa alienda ikulu bila kuwasiliana na upinzani ila odinga alishakubaliana na kina musyoka get the difference

Pia lowassa hakusema wamemaliza tofauti alisema TUMUUNGE MKONO bila kusema jinsi gani watasuluhisha difference zetu ila odinga na uhuru wamesema wazi watakuja na ACTION PLAN so at least wapinzani wa kenya watagain something as in malalamiko yao hayajaenda bure

So kuna difference kubwa sana all in all odinga kafanya la maana
........hata Lowassa alifanya la maana!
 
Uhuru is ofcourse trying to secure his tartared legacy after mass murder and stolen elections.
Kenyans dont care of "talks" or lack of them as long as Jubilee keeps stealing and being stupid economically. Despot uhuru must fall
What is Raila(biggest watermelon) trying to achieve or secure? and what is the way forward for the other now insignificant ANASA principals, the likes of Watermelon Kalonzo, Mdvd and Weta?
 
I pity those who had invested so much in NASA. The likes of Sam 999 alienda wapi? He used to swear in the name of Raila. Pathetic.
 
What is Raila(biggest watermelon) trying to achieve or secure? and what is the way forward for the other now insignificant ANASA principals, the likes of Watermelon Kalonzo, Mdvd and Weta?
The problem with you is that you do t seperate Politics and Reform agenda. It does not matter whether Uhuru &Raila are now sleeping in the same bed dry frying each others' mattacore. if the reform agenda is abandoned from these deliberations, we shall own it we the people and pursue it.
 
Back
Top Bottom