Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Manyerere uko sahihi kabisa na hii ndio hoja ambayo watu wengi tunaoangalia mambo objectively tuliyo nayo. Huyu ndio Kikwete katika rangi zake halisi. Na hii inathibitisha kuwa Tanzania Mwenyezi Mungu anatupenda sana - yaani kama nchi/jamii tumeweza ku-survive miaka kumi tukiwa mikononi mwa binadamu wa aina hii. Ninasisitiza neno 'tume-survive' kwa maana tumepita kwa kudura za Mwenyezi Mungu. Na kama tungekuwa binadamu wenye fikira za kawaida, tulipaswa kutoa adhabu kwa kuikataa, hapana, niseme kwa kuipumzisha ccm. Lakini tuko namna tofauti - wanazuoni wa nchi za magharibi inabidi wa-design tafiti za aina ya pekee kutu-study tu binadamu wa fikira zipi.Sheria inaendana na busara. Dibagula, alipofungwa kule Morogoro, sheria ilifuatwa. Akahukumiwa; lakini mazingira ya uvunjifu wa amani uliifanya Mahakama ya juu ione busara ya kufuta kabisa ile hukumu kwa mkosaji. Unachoona hapo ni kwamba pamoja na sheria kuwa ilitumika vizuri, bado busara ilitawala na ikaifanya nchi ikatulia.
Kwa hili la JK kuendelea na uteuzi hadi dakika za majeruhi ni kweli Kikatiba yuko sahihi, lakini busara inagoma kabisa! Huwezi kuwa unajindaa kuondoka madarakani wiki moja ijayo halafu ukaunda safu unazotaka wewe. Hii ni gharama. Kumbuka, huyo anayekuja anaweza kupangua wote hao, na wakalipwa mafao! Mzigo ni kwa mwananchi maskini. Yeye atakuwa anakula maisha yake ya ustaafu kama kawaida. Fikiria, mtu dhaifu kabisa kama Kipande anampa madaraka baada ya kuvuruga Bandari! Huyu Rais ni wa pekee, si kwa Afrika Mashariki na Kati pekee, bali ulimwengu mzima. Tulipomuunga mkono mwaka 2005 hatukujua tunaunga mkono aina hii ya kiongozi! Mungu atusamehe. Watanzania watusamehe, na zaidi ya wote; Dk. Salim Ahmed Salim atusamehe!!
Somaibara ya 42 (3)(a) ya katiba ya jamhuri ya muungano uone madaraka ya rais yanakomea wapi .na kama huju hata kesho anaweza kufanya uteuzi hata mara baada ya kura kupigwa
na ndio msngi wa rasimu pendekezwa ya Wananchi (sio hii ya change)....Kuondoa uozo kama huu...Siyo kosa kikatiba
hajakiuka katiba..kulikuwa kuna ulazima gani kama si fadhila na kuanza kumpangia safu Magu(ambaye naye Kaunda tume ya kuja kumshauri)Ibara ya 42 (3) kifungu a kinampa ruhusa kufanya hivyo
''circumstantial evidence'' proves otherwiseNa hakuna mahusiano yoyote kati ya uchaguzi huu na uteuzi wa vyeo hivyo
Mzee Mwinyi ndiye best of all times.
Nadhani wewe hiyo kikwete ni mpwao. Kafanya hata Mwigulu aone naye anaweza kuwa rais wa Tz, hii ni fedheha sana.
Acha kutugawa wananchi Watanzania ,Chadema asilia ndio mdudu gani huyo.Haya makundi ndio sababu ya kufeli katika kila kitu.Wewe unafurahia tu kodi zetu kutumika vibaya?.Katiba inayomfanya binadamu kuonekana kama Mungu mtu wew unaifurahia tu...
mnaona uchungu mlitaka nafasi zote wapewe wa kaskazini jk bado ni rais
Hatunywi sumu hatunyongi............ccm mbele kwa mbele !
Na mvimbe mpasuke .......mtajijua wenyewe ! Salary Slip
Walimpigia JK kwa style hii hii ya Lowasa. Mihemko ilitawala hivihivi na mainjinia wa mihemko hiyo walikuwa ni Rostam na Lowasa. Baada ya JK kuchukua nchi wakasuka dili la RICHMOND/DOWANS kurudisha gharama walizotumia kutengeneza mihemko. Na kwa kuwa serikali ilikuwa mikononi mwao wakatengeneza mazingira ya serikali kushindwa kesi na Rostam akalipwa Bil 120 na ndizo sasa wamezitumia kuwanunua akina Mbowe na kutengeneza mihemko mitaani. Ikiwa lowasa ataingia madarakani hizo gharama lazima zirudi. Rostam hajawahi fanya kazi za hasara. Unakumbuka KAGODA, na DEEPGREEN aliyechota Bil 40 kaunta za CRDB alikuwa nani?
Hivi hapati ushauri toka kwa mkewe.
JK ATEUA MAKATIBU WAKUU WANNE NA MANAIBU KATIBU WAKUU WATANO WAPYA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa Ijumaa, Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara mbali mbali.
Aidha, Rais Kikwete amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya watano, amewateua Makatibu Tawala wa Mikoa wawili na pia amewahamisha Naibu Makatibu Wakuu wawili.
Kwa mujibu wa uteuzi huo,
Rais Kikwete amemteua Ndugu Hab Mkwizu kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo; Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mhandisi Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.
Aidha, kwa mujibu uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Mhandisi Paul M. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini; Dkt. Maria Mashingo kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Ndugu Zidikheri M. Mundeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Wengine walioteuliwa kuwa Naibu Makatibu Wakuu ni Ndugu Tixon T. Nzunda ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ndugu Emmanuel Kalobelo ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Walioteuliwa kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa ni Ndugu Eliakim Maswi ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Mhandisi Madeni Kipande ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Katibu Mkuu ambaye anahamishwa ni Bibi Sihaba Nkinga ambaye anakwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Naibu Makatibu Wakuu wanaohamishwa ni Ndugu John T. Mngodo ambaye anahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya kutoka Wizara ya Uchukuzi na Ndugu Mwamini Juma Malemi ambaye anakwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Wateuliwa hao wote wataapishwa asubuhi ya leo, Jumamosi, Oktoba 24, 2015, Ikulu mjini Dar es Salaam.
nilishasema mtavimba mpaka mtapasuka bure,,,,na mkiindeleza kilomolomo atateua hadi tarehe 30,,,,just to prove a point...
nilishasema mtavimba mpaka mtapasuka bure,,,,na mkiindeleza kilomolomo atateua hadi tarehe 30,,,,just to prove a point...