Sheria inaendana na busara. Dibagula, alipofungwa kule Morogoro, sheria ilifuatwa. Akahukumiwa; lakini mazingira ya uvunjifu wa amani uliifanya Mahakama ya juu ione busara ya kufuta kabisa ile hukumu kwa mkosaji. Unachoona hapo ni kwamba pamoja na sheria kuwa ilitumika vizuri, bado busara ilitawala na ikaifanya nchi ikatulia.
Kwa hili la JK kuendelea na uteuzi hadi dakika za majeruhi ni kweli Kikatiba yuko sahihi, lakini busara inagoma kabisa! Huwezi kuwa unajindaa kuondoka madarakani wiki moja ijayo halafu ukaunda safu unazotaka wewe. Hii ni gharama. Kumbuka, huyo anayekuja anaweza kupangua wote hao, na wakalipwa mafao! Mzigo ni kwa mwananchi maskini. Yeye atakuwa anakula maisha yake ya ustaafu kama kawaida. Fikiria, mtu dhaifu kabisa kama Kipande anampa madaraka baada ya kuvuruga Bandari! Huyu Rais ni wa pekee, si kwa Afrika Mashariki na Kati pekee, bali ulimwengu mzima. Tulipomuunga mkono mwaka 2005 hatukujua tunaunga mkono aina hii ya kiongozi! Mungu atusamehe. Watanzania watusamehe, na zaidi ya wote; Dk. Salim Ahmed Salim atusamehe!!