Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,904
Rais Kikwete kuna mambo mengi aliyotaka kuyafanya katika uongozi wake kwa dhamira njema lakini kwa sababu ambazo mimi siwezi kuzielewa vizuri hakufanikiwa kabisa. Miongoni mwa mambo hayo ni;
1) JK alitangaza zaidi ya mara mbili mchakato wa kutungwa kwa sheria ya kutenganisha siasa na biashara. Wafanyabishara walio wengi ndani ya ccm wakamzidi ujanja. Rais pamoja na dhamira yake njema akaa kimya mpaka leo.
2)Rais aliunda kimya kimya kamati ya kuchunguza na kumshauri kuhusu Majaji waliomaliza muda wao wa ajira na kupewa mikataba mingine kama ni halali au si halali. Kamati iliyoundwa ikulu ikamshauri majaji hao si halali. Akakaa kimya. Ripoti hiyo ikamfikia Tundu Lissu akailipua Bungeni. Spika akamwambia ama Lissu akanushe au akalete ushahidi. Lissu akapeleka ushahidi wake kwa Spika. Ktk kumlinda Rais Spika akaamua kulikalia jambo hilo hadi kesho. Rais alikwama, sijui kilichomkwamisha.
Bunge liliunda tume ya kuchunguza kampuni ya Richmond na kupitisha mapendekezo kumi na kitu (17?). Mpaka Leo serikali haijaweza kutekeleza mapendekezo hayo yote kwa ujumla wake na hoja hiyo ikafungwa kisanii Bungeni. Rais hapo alikwama tena.
Baada ya hoja ya kelele nyingi sana kutoka kwa wananchi kuhusu madini, Rais aliunda tume ya Bomani. Tume ilipeleka mapendekezo mengi serikalini kuhusu secta ya madini kwa ujumla ambayo mengi mpaka leo hayajatelelezwa. Rais alikwama tena.
Mapambano dhidi ya madawa ya kulevya kuna kila dalili kuwa seriali yetu chini Rais JK nayo inaelekea kukwama pamoja na tatizo hili kutuchafua duniani. Hata yale majina yake ya wauza unga hakijaeleweka bado. Hii inatokana na ama Rais kutokuwa na dhamira ya dhati mwenyewe au kukwamishwa na mfumo.
Sasa kuna hili la katiba mpya. Rais anaonekana anataka kukamilisha lakini mawaziri wake wako busy kumkwamisha. Wakati Rais amekaa ikulu na viongozi wa vyama vya siasa ikiwepo CCM na kufikia mwafaka wa kurejeshwa kwa sheria hiyo Bungeni, mawaziri waliotoa kauli tata kama Lukuvi, wasira na Chikawe hawajakanusha kauli zao wako kimya. Mbaya zaidi wengine wameongeza kauli zinazopingana na dhamira na maafikiano ya Rais wenyeviti wa vyama vya siasa. Wako waliosema kwamba Serikali haina mpango wa kurekebisha sheria hiyo. Ndugai akaibuka na kusema kanuni haziruhusu.
Ni kwa sababu hiyo, ni ushauri wangu kwamba Rais afuate ushauri wa Dr Mkumbo Kitila kwenye gazeti la Raia Mwema kuwa, Rais lazima achague ama kuwafurahisha Chama chake na mawaziri wake au wananchi wa Tanzania wanaotaka katiba mpya. Lazima awe tayari kuchagua. Hawezi kushika vyote viwili kwa wakati mmoja. Hawezi kupata katiba mpya inayotakiwa na wanachi na isiyotakiwa na ccm na mawaziri wake na wakati huo huo ukafurahisha pande zote mbili. Haiwezekanai – ni ushauri wa Dr Mkumbo Kitila.
Rais akifuata ushari huu na katiba mpya ikapatikana maana yake atakuwa amefunika matatizo mengi sana ya uongozi wake. Hoja ya kutenganisha siasa na biashara, madawa ya kulevya, majaji wenye utata kisheria, mapendekezo ya Tume za Bunge kutokelezwa, ufisadi na madhaifu mengine mengi sana serikali yatakuwa yamemezwa na kufunikwa kabisa na katiba mpya kwa kuwa katiba mpya imetoa suluhisho la mambo hayo yote.
Nani ajuaye? Huenda katiba mpya ikampa JK kuwa mmoja washindani wakubwa wa Tuzo ya Ibrahim Mo akapata Mabilioni yote hayo.
Ushauri wangu,
JK kupanga ni kuchagua, katiba ni kete yako ya mwisho, kaza mwendo, tupate katiba mpya, vinginevyo, ukiwafurahisha akina wasira, chikawe, lukuvi na Ndugai utakuwa umepotea njia na wanao na wajukuu zako na watanzania tutakosa kitu kizuri cha kusema kuhusu uongozi wako. Ukileta katiba tutasema JK ndo Rais aliyeleta katiba. Kazi kwako.
Nawasilisha;
Aweda.