Rais Kikwete alimtuma Membe kwa Mwalimu Nyerere, Sehemu ya Pili (2)

GARETHBALE

Member
Joined
Dec 22, 2013
Posts
76
Reaction score
339
Jana niliahidi kuendelea na simulizi kuhusu mambo kadhaa yamhuhusuyo Ndugu Bernard Kamilius Membe na siasa za nchi yetu. Simulizi hizi zipo katika mtindo wa "series".Kila "episode" ya "series" hizi itahusisha matukio muhimu yasiyo maarufu kwa watu wengi lakini yana mvuto wa kipekee katika wasifu wa Ndugu Bernard Kamilius Membe.

Nitaendelea nilipoishia jana...

Baada ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kumpatia majibu Ndugu Bernard Kamilius Membe kuhusu swali la Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete juu ya ushiriki wa vijana kwenye kinyang'anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 uliojumuisha vyama vingi,likaibuka suala la ugonjwa na matibabu ya aliyewahi kuwa waziri wake wa fedha enzi za uongozi wake aliyeitwa Mzee Jamal.

Kwa vijana wa sasa wasiomjua Mzee Jamal huyu alikuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya uongozi wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Alikuwa na asili ya Kihindi. Lakini ni mzawa wa nchini Tanzania.

Alikuwa mfanyabiashara, raia mwema aliyeshiriki katika mapambano ya kupigania uhuru tangu enzi za TANU hadi pale ilipozaliwa CCM.

Baadaye aliachana na siasa. Akarejea katika shughuli zake binafsi na hata umri ulipomtupa mkono alisafiri kuishi na mwanaye nchini Canada hadi umauti ulipomfika. Alikuwa rafiki mkubwa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Wakati wa mazungumzo yao mengine, Ndugu Bernard Kamilius Membe alimjulisha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere juu ya hali ya afya ya rafiki yake wa muda mrefu Mzee Jamal.

Kwa wakati huo Mzee Jamal alikuwa akiumwa sana na gharama za matibabu zilikuwa juu sana nchini Canada hivyo kufanya familia yake kushindwa kuzimudu ipasavyo.

Pamoja na kuwa mfanyabiashara miaka ya nyuma na kuwahi kuwa waziri wa fedha enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lakini hakuweza kujilimbikizia mali wala kukwepa kodi.

Baada ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuelezwa na Ndugu Bernard Kamilius Membe kuhusu kuumwa kwa Mzee Jamal ilibidi Mwl. Julius Kambarage Nyerere aombe ofisi za ubalozi kupelekwa siku inayofuata kumwona na kumjulia hali rafiki yake Mzee Jamal.

Siku iliyofuatia alipelekwa akiambatana na Ndg. Bernard Kamilius Membe. Hali aliyomkuta nayo Mzee Jamal haikuwa nzuri sana.Mtoto wake alilia sana akiomba msaada wa kugharamiwa matibabu na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ubalozi uliopo Canada.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliumizwa sana na hali ile. Akamwagiza Ndugu Bernard Kamilius Membe kuzungumza na Balozi wetu wakati huo nchini Canada ili apate mihadi ya kuonana na waziri mkuu wa Canada wa wakati huo ambaye alikuwa na mahusiano naye mazuri. Nia ni kuzungumzia suala la matibabu ya Mzee Jamal.

Baada ya Waziri Mkuu wa Canada kuridhia kuonana na Mwl. Julius Kambarage Nyerere siku ilipowadia Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliambatana na Ndugu Bernard Kamilius Membe katika kikao kila na waziri mkuu wa Canada.

Mazungumzo yalikuwa na ajenda moja tu ya matibabu ya Mzee Jamal. Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliomba msaada wa matibabu bure kwa Mzee Jamal kwasababu familia yake haimudu gharama zake na hali ya Mzee Jamal inazidi kuwa mbaya kila siku iendayo kwa Mungu.

Waziri Mkuu wa Canada aliridhia kusaidia gharama za matibabu ya Mzee Jamal lakini akishauri kuwa kwakuwa nchini kwake matibabu ni bure (kwa wakati ule - sijajua kwasasa), lakini kwa mtu mwenye uraia. Hivyo basi, akaagiza Mzee Jamal apatiwe hati ya kusafiria ya Canada na uraia kamili wa Canada. Alifanya hivi kwasababu wao wanaridhia uraia pacha (dual citizenship) lakini kwakuwa Tanzania hatuna sera hii, basi ni lazima Mzee Jamal aukane uraia wake wa Tanzania na kupatiwa wa Canada.

Kwa mazingira ya wakati ule Mwl. Julius Kambarage Nyerere na familia ya Mzee Jamal hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kukubaliana na ushauri wa waziri mkuu wa Canada ili kuokoa maisha ya Mzee Jamal.

Baada ya kikao kile jukumu la kushughulikia suala la uraia wa Mzee Jamal likakabidhiwa kwa mamlaka husika ya serikali ya Canada na ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pale Canada ukawa na jukumu la kuwasilisha nyaraka muhimu za Mzee Jamal zitakazosaidia kuthibitisha uraia wake wa Tanzania kabla ya kuhamia katika uraia wa Canada. Na ubalozi ukampatia jukumu la kuratibu hili suala Ndg. Bernard Kamilius Membe.

Kwakuwa Mwl. Julius Kambarage Nyerere alikuwa na majukumu mengine katika hizo ziara zake ilimlazimu aendelee na majukumu hayo. Lakini aliambatana na Ndg. Bernard Kamilius Membe kwenda kumuaga Mzee Jamal na familia yake. Wakati akiwa uwanja wa ndege wa nchini Canada baada ya kutoka kumuaga Mzee Jamal na familia yake akielekea nchini Marekani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alimwambia Ndugu Bernard Kamilius Membe kuwa ipo haja ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuridhia suala la uraia pacha (dual citizenship) ambao wakati wa uongozi wake waliukataa lakini changamoto ya suala la matibabu ya Mzee Jamal limempa tafakuri kubwa sana.

Siku chache mbeleni tangu Mwl. Julius Kambarage Nyerere aondoke kuelekea nchini Marekani huku nyuma Ndg. Bernard Kamilius Membe kwa kushirikiana na serikali ya nchini Canada na ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada walifanikisha kupatikana kwa uraia kamili wa Canada wa Mzee Jamal na kuijulisha familia ya Mzee Jamal kuwa wamwandae baba yao kwa ajili ya kufuatwa akaanze matibabu chini ya uangalizi wa serikali ya Canada kwa maelekezo ya waziri mkuu wa Canada.

Siku ya kwenda kumchukua Mzee Jamal ili akaanze matibabu Ndugu Bernard Kamilius Membe akiambatana na ujumbe wa serikali ya Canada nyumbani kwa Mzee Jamal kwa bahati mbaya walipofika tu wakakuta msiba. Mzee Jamal alikuwa kafariki muda mchache kabla ya wao kufika pale. Lilikuwa ni pigo kubwa kwa familia, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Canada. Kubwa zaidi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliumia sana alipopata zile taarifa. Rafiki yake mkubwa alikuwa kaaga dunia.

Na hii ndiyo ikawa sababu kuu ya Ndugu Bernard Kamilius Membe kuwasilisha hoja kuwa katika mchakato wa katiba mpya wakati akiwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kiwepo kipengele kinachozungumzia suala la uraia pacha (dual citizenship).

Na alitoa sababu muhimu zenye mashiko ili uraia pacha (dual citizenship) iwe ni haki ya kila Mtanzania huku suala la Mzee Jamal ikiwa ni moja kati ya "precedents" zinayoishi hadi leo.

Nihitimishe kwa kusema tu kwamba uraia pacha (dual citizenship) haikuwa hoja binafsi ya Ndugu Bernard Kamilius Membe bali ilikuwa na chimbuko lake na uzuri wa hoja hii Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliweza kumshirikisha hata Mzee Kingunge Ngombale Mwiru miaka ile wakati akimwelezea hali aliyomkuta nayo Mzee Jamal nchini Canada kabla ya umauti kumfika.

Je, unajua kwamba "wanamtandao" walikuwa watano tu?

Tukutane tena kesho muda kama huu...
 
habe
Porojo za nini?

Uraia pacha hauna faida zozote kwa Mtanzania
Watanzania 99% wanaishi nchini na hata hao waliopo nje ya Nchi wengi ni wabeba boks

Uraia pacha unapigiwa sana chapuo na wahindi na waarabu sijui Kwanini

Tumwache Baba wa Taifa apumzike
have you ever made critical economic analysis or you are responding out of emotions!!😂😂😁😁
 
Uraia pacha hautakataliwa kila siku. Wakati umefika kufanya maamuzi sahihi kulingana na mabadiliko ya siasa, uchumi na kijamii zinazotamalaki ulimwenguni kwa sasa.
 
Nitatega sikio kesho kujua juu ya wanamtandao
 
Aisee, mambo mengine katika nchi hii yamefanywa kuwa siri sana, twashukuru kwa kutujuza mkuu.
 
Enzi hizo nchi haijaanza kutawaliwa na washamba by zito kabwe
 
Tunawasubiri. Ila ni vema ukaunganisha hii habari na ile part 1 ili tupate mtiririko mzuri
 
Hivi Nyerere day ya miaka 20 bila Mwl ilifanyika Lindi au Rondo? ? Mbona mtu wa karibu "saaana" na Mwl hakuhudhuria? ?
 
Alikuwa Burigi anafuga mbuzi. Samahani kama nimekukwaza ila huo ndio ukweli. By the way wananiita moron.
Sawa wewe wa Mjini, lakini u kumbuke walio wengi leo hii wametoka huko huko mashambani na wanaojidai wa mujini wengi ni darasa la saba la zamani maana from for four walipata four au yai
 
We vipi? Kwani mi nimemsema nani? Enzi za Nyerere watu wangapi walikuwa wanafuga mbuzi Burigi!
 
Back
Top Bottom