makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Wana JF,
Nimeonelea nilete mada hii ili kuonyesha namna kiongozi wetu Mkuu wa nchi Rais Jakaya Kiwete alivyo mnafiki,mwongo,kigeugeu na ndumila kuwili.Hoja yangu itazungumzia maeneo muhimu matatu ambayo Rais amewadhihirishia Watanzania na dunia yote kuwa ni mnafiki.
Kwanza wakti Rais Kiwete akiunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliutangazia umma wa Watanzania kwamba kuna haja ya kuwa na Katiba Mpya itakayoipeleka Tanzania kwa miaka mingine 50-100. Tume iliundwa alimaarufu kama Tume ya Warioba ambayo iliafanya kazi kwa umakini na ustadi mkubwa sana. Tume ikamaliza Rasimu zote 2 na hatimaye kumkabidhi Rais Kiwete na akaisifia sana Tume hiyo.
Lakini shida imeanza kuonekana baada ya Tume kukabidhi Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba na kufuatia kuundwa kwa Bunge Maalumu la Katiba-BMK na yeye kwenda Dodoma kulizindua Bunge hilo. Hapa ndipo Rais alianza kuonyesha rangi zake za undumila kuwili. Kile alichokizungumza Rais Kiwete Bungeni hakika hakikutarajiwa na Mtanzania yeyote mwenye kuitakia mema nchiu hii. Hotuba hii ambayo haikuwa hotuba baali kujibu mapigo kwa Tume ya Jaji Warioba na hotuba yake wakti akikabidhi Rasmu ya Tume yake.
Kila mtanzania alipigwa na bumbuazi kwa maneno hayo yaliyokuwa yamejaa kejeli,kebehi na dharau kwa Tume ya Jaji Warioba.Rais Kiwete aliisahmbulia kwa lugha ya kifedhuli na kukosoa mapendekezo yaliyomo kwenye Rasmu hiyo na hasa kipengele cha Muundo wa Serikali TATU na Ukomo wa Ubunge.
Jambo la lushangaza kabisa ni juzi alipokuwa London,Uingereza alipoongea na Watanzania na kuwaambia kuwa hana tatizo na Muundo wa Serikali 3 kama Watanzania wataamua hivo! Hapa ndipo penye unafiki wa Kiwete.Hii ilikuwa ni kauli ya ajabu sana maana ilikuwa inapingana na Hotuba yake ya Bungeni. Bungeni alitetea Serikali 2 kama msimamo wa CCM yake badala ya kutetea MAONI YA WATANZANIA 60% WANAOTAKA SERIKALI 3 KUPITIA TUME YA WARIOBA!!
Lakini pia kebehi,dharau na matusi ya Kikwete kwa Tume yaliendelezwa na Katibu wake Mkuu wa CCM Bwana Abdulrhaman Kinena alipohutubiwa wana CCM katika Viwanja vya Kidongo chekundu akihoji uhalali na umakini wa Tume ya Warioba ya kupendekeza Serikali 3. Kinena alisema kuwa kulikuwa ati na Mabaraza zaidi ya 110(ya CCM) yaliyopendekeza Serikali 2 lakini kwenye Rasimu ya Wariona haikuonyeshwa. Tume ikiulizwa inasema makabrasha yamepotea!!! Hapa Kinena alikuwa anaiponda Tume kwamba haikufanya kazi iliyotumwa baali imefanya kazi yake yenyewe!!!Ni dhahiri Kinena alikuwa nazungumza maneno haya kwa kujiamini kwa vile ndicho kilichomo ndani ya nafsi ya Kikwete!
Juzi Jaji Warioba ametupiwa virago kama kocha wa mpira aliyeshindwa kuifundisha Timu ya mpira. Ikulu ya Kiwete imedai kuwa Tume ilishamaliza kazi kwa hiyo kila mali waliyokuwa wakiitumia TUME yakiwemo magari virudishwe mara moja Ikulu.Je, kulikuwa na uharaka gani wa amri hizi za kibabe na kijeshi? Hivi kosa la Warioba na Tume yake ni kuingiza maoni ya Watanzania walio wengi kuwa wanataka Muungano wa Serikali 3?
Ni dhahiri kabiosa kuwa Kikwete na CCM yake wamewadhihirishia Watanzania na Dunia yote kuwa ni wanafiki na walitaka Tume ya Warioba iweke mapendekezo ya CCM kwenye Rasmu na siyo mapendekezo ya Watanzania walio wengi. Hii ni aibu kwa Kiwete, CCM na Serkali yake. Upuuzi huu ndiyo unaoendelezwa hata ndani ya BMK ya kutetea mawazo na maoni ya CCM na siyo mapendekezo ya Watanzania!!!
Tafakuri.