Mtoa mada una upungufu mkubwa sana wa ufahamu. Ngoja nikupe somo kidogo. Mada yako imejikita kwenye hoja ya katiba. Well umeelezea jinsi Rais alivyotangaza kuwa anadhamiria kuunda tume itakayokusanya maoni ya wananchi juu ya katiba mpya. Ukaeleza kuwa Jaji Warioba ndiye aliyepewa kazi hiyo. Well umeeleza kuwa Warioba amefanya kazi yake vizuri kiasi cha kupongezwa na Rais Kikwete. Well ukasema kuwa wakati anaenda kulizindua Bunge Maalum ndipo hali ya hewa ilipochafuka hasa baada ya Rais Kikwete kukosoa Rasimu hiyo. Well ukasema kuwa Rais alieleza akiwa London Uingereza kuwa hana matatizo na mfumo wa serikali tatu ikiwa wananchi wataamua. Hizo ndizo hoja zako juu ya Rais Kikwete.
kwanza, unapaswa kuelewa kuwa msukumo wa kuwa na katiba mpya haukutokana na utashi wa serikali. Msukumo huo ulitokana na tamaa za madaraka za viongozi wa vyama vya upinzani. Ukumbuke kuwa CHADEMA hawakubaliki Zanzibar. Kwao Zanzibar haina umuhimu wala faida kwao. CHADEMA hawana hata mbunge mmoja kule. CUF haikubaliki zaidi Tanzania Bara. Kwa sasa ina wabunge watatu tu ambapo wawili ni wa kuchaguliwa tena wote wakitoka mkoa mmoja tu wa Lindi na mmoja ni wa viti maalum. CUF nguvu yao kubwa ipo visiwani Zanzibar tena kwenye kisiwa cha Pemba tu. Unguja hawana kabisa nguvu. Hivyo shinikizo la vyama hivi juu ya katiba mpya hususan huu muundo wa serikali tatu linatokana na tamaa ya madaraka. CHADEMA wanaamini kuwa ikiwa kutakuwa na serikali ya Tanganyika, wao wanaweza kushinda kwa kile wanachoamini kuwa wanakubalika zaidi Tanzania Bara japo uhalisia uliopo ni kwamba hiki ni chama cha Kaskazini. CUF nao wanaamini kuwa ikiwa katiba mpya itapatikana yenye muundo mwingine zaidi ya uliopo, ni kwamba wao wanaweza kupata fursa ya kutawala Zanzibar na shauku yao kubwa ni kuwa na nchi huru ya Pemba. Katika mazingira hayo, ni wazi kuwa vyama hivi vilizunguka mlango wa nyima ili kuirubuni tume ya Warioba ikubaliane na matakwa yao. Hapo Rais Kikwete alikuwa na haki ya kuonesha wasiwasi wake juu ya hiyo tume.
kuhusu kuipongeza tume na baadaye kuikosoa, ni jambo la kawaida kumpongeza mtu unapomtuma kazi na akaimaliza. Sasa unapoiangalia kazi uliyomtuma halafu ukagundua kuwa ina mapungufu mengi na pengine ameenda kinyume na maelekezo yako, je utaendelea kumsifia? Ni wazi kwamba utaikosoa kazi hiyo na kuonesha mapungufu yaliyopo. Ndivyo alivyofanya JK. Aliipokea Rasimu ile na akaipongeza tume kwa kazi waliyofanya. Ila baada ya kuipitia, akagundua mapungufu kadhaa ambayo ni vema kuyaeleza tena kwenye bunge ambalo ndilo lenye maamuzi ya mwisho juu ya Rasimu hiyo. Ningemshangaa sana Rais Kikwete kama angeyaona mapungufu hayo halafu akayanyamazia.
Kuhusu kauli yake kuwa yupo tayari kuunga mkono muundo wa serikali tatu ikiwa wananchi wataamua, well. Namponyeza pia kwa uamuzi huo. Ikiwa wananchi wote au kwa kiwango kikubwa tumekubaliana kuunga mkono muundo huo, ni wazi kuwa hata yeye Rais ataungana nasi kwa vile anajua kuwa ni maamuzi ya wengi. Ila haiingii akilini kati ya watu laki tatu walioohojiwa na Warioba, watu 47,000 waonekane ni wengi kuliko wale 300,000. Hapa ni wazi kuwa Warioba na timu yake wameonesha udhaifu wa hali ya juu sana. Katika hali hiyo, ni wazi kuwa Warioba amejitakia kudharauliwa si na Rais tu bali na kila anayeitakia mema nchi hii.
Kauli ya kinana nayo ni ya kuungwa mkono. Mathalan, Kinana amehoji wapi zimeenda takwimu za mabaraza ya kata na wilaya. Mbona taarifa zake hazikutolewa? Ni wehu tu na watu wenye upeo mdogo wa kufikiri kama mtoa mada ndio watakaomshambulia Kinana