nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,801
Friday, May 27, 2011
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Alan Kijazi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Bwana Kijazi anachukua nafasi ya Bwana Gerald Bigurube ambaye alistaafu kwa hiari.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Kijazi alikuwa mfanyakazi wa TANAPA kama Mkurugenzi wa Mipango, Miradi ya Maendeleo na Huduma za Utalii.
Bwana Kijazi alisoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika fani ya Uendelezaji wa Maliasili (MSc. Management of Natural Resources). Awali Bwana Kijazi alipata elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alihitimu Shahada ya Mipango ya Mazingira (BA. Environmental Planning).
Kabla ya kujiunga na TANAPA Bw. Kijazi alifanya kazi katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, mwaka 1998 hadi 1999. Pia alikuwa Meneja wa Mradi wa Kuendeleza Uhifadhi wa Wanyamapori (African Wildlife Foundation), mwaka 1999 hadi 2003.
Uteuzi huo unaanza mara moja.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA TANAPA
Rais Jakaya Kikwete