Rais Kikwete amteua Prof. Mussa Assad kuwa CAG mpya akimrithi Ludovic Utoh

Rais Kikwete amteua Prof. Mussa Assad kuwa CAG mpya akimrithi Ludovic Utoh

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,501
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS



PRESIDENT'S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Assad alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bwana Ludovick Utouh ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.

Profesa Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na udhibiti wa fedha ambaye ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991.

Profesa Assad pia ana Stashahada ya Kitaaluma ya Uhasibu (Professional Diploma in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City mwaka 1990 na Shahada ya Biashara (Bachelor of Commerce) ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 1988.

Pamoja na uzoefu wa kitaaluma, Profesa Assad anao uzoefu mkubwa katika eneo la uhasibu na ukaguzi. Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) kwa miaka saba (2007 - 2014); ni Rais na Mjumbe wa Chama cha Wahasibu Afrika (Pan African Federation of Accountants) tangu mwaka 2012; na ni mjumbe wa Bodi kadhaa za Wakurugenzi nchini Tanzania.


Katika kumteua Profesa Mussa Juma ASSAD kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Rais anayo imani kubwa kuwa elimu, weledi, ujuzi na uzoefu ambao Profesa Assad anao utamwezesha kutekeleza vema majukumu ya nafasi hiyo muhimu sana katika utawala bora wa nchi yetu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
1 Desemba, 2014

 
CAG ndio alikuwa hajui kama pesa za escrow ni za umma? Bado Gavana wa BOT .
 
10313732_648287681948876_6001176764329198945_n.jpg
 
Francis aliyekuwa anakaimu kapigwa chino. Je ni kwa sababu ya taarifa ya escrow?

Lazima wapewe watu watakaoweza kulinda maslahi baada ya awamu .........................!! Anyway, sidhani kama ana CV kumshinda huyu bwana!!
 
Rais kikwete leo amemteua prof,Mussa J Assada kuwa mthibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali(CAG),ATAAPISHWA KESHO.Yamkini ndio jitahada zake za kujibu mapendekezo ya bunge lilimalizika mwishoni mwa wiki lilipita

Chanzo;ikulu
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Profesa Mussa Juma Assad, kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Novemba 5, 2014.

Assad, anachukua nafasi ya Bwana Ludovick Utouh, ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.
 
Nimepata tetesi kuwa kuna profesa kateuliwa kuwa CAG mpya wenye taarifa zaidi mtujuze
 
JK siku zote yuko makini anapofanya uteuzi isipokuwa wateuliwa baadae hufanya ya kwao na kusahau maagizo ya kiongozi.

VIVA ASSAD!
 
Back
Top Bottom